Jumanne, 17 Januari 2017

Costa mambo yaenda kombo…Wachina watangaza kuachana na mpango wake. Sheria mpya iliyotambulishwa na ligi kuu nchini China imeifanya timu ya Tianjin Quanjian kubadili maamuzi kuhusu mchezaji wa Chelsea Diego Costa.Kwa muda mrefu sasa Costa amehusishwa na kuhamia China,na wiki hii tetesi hizo zilizidi kushika kasi baada ya kusemekana kwamba wawakilishi wa Diego Costa tayari wako nchini China kukutana na matajiri wa Tianjin. Lakini sasa wikiendi hii chama cha soka cha China kilileta sheria mpya katika ligi yao.China wameamua kuanzia sasa timu zote za nchi hiyo zitasajili wachezaji watano tu wakimataifa.Katika hao watano ni watatu tu ambao watacheza katika mechi.Baada ya sheria hiyo kupitishwa mmiliki wa Tianjin Quanjin amesema wazi walimtaka Costa lakini kutokana na sheria hiyo watabadili mchezaji wamtakae. Mmiliki wa timu hiyo bwana Shu Yuhui amesema sio Costa tu,bali pia walimtaka Cavani,Radamel Falcao na Karim Benzema lakini sasa inabidi waanze kufikiria upya.Alisema “habari zilizozagaa kuhusu sisi na Diego Costa zilikuwa ni za kweli lakini baada ya sheria hii sidhani kama hilo linawezekana,ingekuwa ni wachezaji watano uwanjani tungewekeza pesa kubwa katika usajili lakini watano hapana”. Inaaminika huenda hii inatokana na umri wa nyota hao wanaowataka,kutokana na wachezaji kupunguzwa timu za China zinaona ni bora kusajili wachezaji wenye umri mdogo ili hsta kama wakiwa wachache lakini waweze kudumu na kucheza kwa muda mrefu. Pia Yuhui amesema kilichowakwamisha kumchukua Costa ilikuwa ni kutokana na timu yake kutotaka kumuachia.Alisema wasingeweza kusubiri hadi mwisho wa msimu ndio wamsajili.Kwani walihitaji huduma ya mshambuliaji huyo katika raundi ya pili katika msimu wao China.Yuhui alikiri kukutana na wakala wa Costa Jorge Mendez siku chache zilizopita “alikuja kwangu siku chache zilizopita,wakati tunamzungumzia Costa,aliwazungumzia pia Radamel Falcao na Raul Jiminez wa Benfica ambao kila kitu kilikamilika na walitakiwa kusaini ndipo ikaja sheria hii na tulibadili mawazo”. Tianjin inayonolewa na nyota wa zamani wa Italia Cannavaro imeshafanikiwa kumchukua kiungo wa Ubelgiji Axel Witsel.Sheria mpya ya usajili wachezaji wanaotoka nje ya China inaonekana itavibana vilabu vya nchini humo na kupunguza msururu wa wageni uliokuwa unaelekea kupiga Soka China.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni