Jumapili, 21 Agosti 2016

UKWELI KUHUSU FARID MUSSA KUCHELEWA KWENDA KUKIPIGA HISPANIA KATIKA KLABU YA TENERIFE HUU APA

Baada ya ligi kadhaa kuanza barani Ulaya, yameanza kuibuka maswali kuhusu uwepo wa Farid Musa nchini ikiwa awali iliarufiwa kwamba kinda huyo wa Azam FC amefanikiwa kufuzu majaribio yake kwenye klabu ya Tenerife ya nchini Hispania. Klabu ya Tenerife iliridhia kumsajili Farid lakini kuna maswali mengi yamezuka baada ya nyota huyo kuendelea kuonekana nchini huku baadhi ya ligi zikiwa zimeshaanza kupigwa. Sports Extra ya Clouds FM ilimtafuta Farid kwa ajili ya kupata ufafanuzi wa jamo hili kwa kina zaidi na kipi kinachokwamisha yeye kwenda Hispania hadi sasa. “Taarifa niliyopewa na uongozi wa Tenerife ni kwamba, kila kitu wameshawasilisha Azam na wamemalizana kwa kila kitu kwahiyo ni jukumu la Azam kumaliza mambo yao na mimi namalizia baadhi ya mambo ubalozini,” amesema Farid wakati akizungumza na kituo hicho cha radio. Kuhusu yeye kutofanya mazoezi ya maandalizi ya pamoja na timu kwa ajili ya msimu mpya, Farid amesema hiyo sio changamoto kubwa kwasababu bado anaendelea kujifua na kujiweka fit wakati wote. “Mchezaji ni kujielewa, mimi najua kitu gani nafanya na nini nataka. Sibweteki tu nyumbani, naendelea kufanya mazoezi na Azam wakati mwingine nafanya mazoezi yangu mwenyewe ilimradi kuweka sawa kiwango changu.” “Kwasasa bado nipo chini ya Azam na bado wananilipa mshahara kama kawaida,” alimaliza Farid. Kwa upande wake mtendaji mkuu wa klabu hiyo Saad Kawemba amesema kila kitu kinakwenda sawa na tayari wameshasaini mikataba ya Farid kuihama Azam kwenda Tenerife na vimebaki vitu vichache tu kukamilisha dili hilo. “Mikataba yote ya yeye kuhama kutoka Azam kwenda Tenerife tumeshasaini, sasahivi Tenerife wanataka kuoiomba ITC yake ambayo ndiyo tunamalizia kuikamilisha na ndani ya siku chache wataiomba na wataipata halafu watatuma tiketi yake halafu Farid ataondoka,” amesema Kawemba. “Mashabiki wa mpirwa wa Tanzania waelewe kwamba Farid si mchezaji wa Azam kwa sasa na anaondoka wakati wowote.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni