Jumatano, 24 Agosti 2016

BALE AMSOGELEA RONALDO KWA MSHAHARA MADRID

Gazeti la Marca limeripoti kwamba, Gareth Bale amesaini mkataba wa miaka mitano kuendelea kuitumikia Real Madrid, hiyo inamaanisha Bale anamkataba na Madrid hadi mwaka 2021. Cristiano Ronaldo alikubali kusaini mkata mpya mpya na Real Madrid ambao unatarajiwa kuwekwa wazi mapema mwezi September. Mkataba mpya wa Bale utamfanya awe mchezaji wa pili kulipwa kitita kikubwa cha pesa ndani ya Bernabeu, atakuwa akichukua euro milioni 10 kwa msimu sawa na nahodha Sergio Ramos huku wakiwa nyuma ya Cristiano Ronaldo. Nyota huyo wa Wales alikuwa na kiwango kizuri wakati wa michuano ya Euro 2016 na kuisadia timu yake kufika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo huku akianza vizuri pia msimu wa La Liga kwa kufunga magoli mawili ugenini dhidi ya Real Sociedad. Real Madrid imefanya usajili kwa wachezaji wachache katika dirisha la majira ya haya ya joto barani Ulaya, licha ya kumrejesha nyumbani Alvaro Morata kutoka Juventus baada ya kuwa katika kiwango kizuri katika Serie A. Kwa Florentino Perez kipindi hiki kimekuwa cha kawaida ambapo rais huyo wa Madrid hajaangalia jina kubwa katika usajili licha ya mwanzoni kuhusishwa na Paul Pogba. Inaonekana Madrid imejikita katika kuhakikisha wachezaji wake wenye majina makubwa hawatoki katika klabu hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni