Jumatano, 24 Agosti 2016

BAADA YA KUANZA MSIMU KWA KASI, AJIB AFUNGUKA: NIKIWA NA MAVUNGO MTATUKOMA

Mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu amefunguka kuwa anatarajia kung’aa zaidi msimu huu kutokana na ujio wa mshambuliaji kutoka Burundi, Laudit Mavugo. Ajibu amesema amekuwa akielewana vizuri sana kila anapocheza na Mavugo kwenye kikosi hicho cha Msimbazi. Akizungumza na Championi Jumatano, Ajib amesema, ujio wa Mavugo umesaidia kubadili upepo ndani ya kikosi hicho kufuatia kuwa tofauti na wachezaji wengine aliowazoea hivyo ana matumaini makubwa ya kuweza kufanya vyema msimu huu. “Tunafurahia kuona mechi yetu ya kwanza tumeweza kuibuka na ushindi lengo letu kubwa ni kuona tunafanikiwa kushinda katika kila mchezo. “Uwepo wa Mavugo katika kikosi chetu kunanisaidia kuwa na morali ya hali ya juu na kunipa hamasa pindi ninapokuwa naye uwanjani hivyo natarajia kuwa vizuri zaidi msimu huu tofauti na msimu uliopita. “Wanasimba watarajie kile ambacho wanakitarajia kukipata, kwani lazima tutatwaa ubingwa,” alisema Ajibu.  SOURCE: CHAMPIONI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni