pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumamosi, 31 Desemba 2016
Naona niwe wa kwanza kama sio wa tatu kukutakia mema katika mwaka unaosogea kwa kasi, Nahofia msongamano wa msg za heri ya mwaka mpya inabidi nikutumie ujumbe huu mapema... Tunaposogea kuanza mwaka mwingine 2017 ina maana tunazimaliza Mbio za mwaka 2016 haikuwa safari rahisi, Vikwazo navyo havikuwa haba lakini TUMSHUKURU MUNGU KWA YOTE! Siku hazikuganda ndo maana tunahesabu masaa kuumaliza mwaka, Ni masaa machache yalobakia kuufungua Mwaka 2017... Umejifunza nini kwa mwaka 2016? Hiyo ibaki kuwa siri yako na uzitumie changamoto ulizopitia kwa mwaka 2016 kuwa chachu ya UKOMBOZI katika mwaka ujao wa 2017. Mungu wetu si muongo hata ashindwe kukufanya uwe kichwa na kukuondosha katika mkia, Kama kuna nzige, Mandumandu na palare wamekula miaka yako MUNGU ANAKWENDA KURUDISHA MIAKA HIYO! Mwaka 2017 uwe mwaka wa mavuno na ghara zako zijae na kufurika hata kumwagikia, Uwe mwenye afya njema pamoja na BARAKA TELE... Udumu katika NEEMA ZA BWANA zitakazokupa wepesi katika mipango yako mwaka 2017.
CHELSEA YASHINDA MECHI YA 13 MFULULZO LIGI KUU ENGLAND Wachezaji wa Chelsea wakishangilia ushindi wao wa 13 mfululizo katika Ligi Kuu ya England baada ya kuilaza 4-2 Stoke City leo Uwanja wa Stamford Bridge. Mabao ya Chelsea yamefungwa na Gary Cahill dakika ya 34, Willian dakika ya 57 na 65 na Diego Costa dakika ya 85, wakati ya Stoke City yamefungwa na Bruno Martins-Indi dakika ya 46 na Peter Crouch dakika ya 64
POGBA AIFUNGIA LA USHINDI MAN UNITED YAUA 2-1 ENGLAND Paul Pogba akiwaongoza wachezaji wenzake wa Manchester United kushangilia baada ya kufunga bao la ushindi dakika ya 86 katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Middlesbrough kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Old Trafford. Bao lingine la United lilifungwa na Anthony Martial dakika ya 85 kufuatia Grant Leadbitter kuwafungia wageni bao la kuongoza dakika ya 67
Ijumaa, 30 Desemba 2016
Taifa Jangombe imefanikiwa kupata ushindi kwenye uzinduzi wa Mapinduzi Cup Seif Hassan ‘Banda’ amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao kwenye michuano ya Mapinduzi Cup msimu huu baada ya kuifungia timu yake bao pekee la ushindi wakati wa mchezo wa ufunguzi kati ya Taifa Jang’ombe dhidi ya Jang’ombe Boys mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Amaan, Zanzibar. Banda aliifungia bao Taifa Jang’ombe dakika ya 83 na kuifanya timu yake iongoze Kundi A kwa kuwa na pointi moja mkononi baada ya kucheza mchezo mmoja. Mechi hiyo ilikuwa na upinzani mkubwa kutokana na timu zote kutoka mtaa mmoja hivyo kukamiana na kutambiana nje na ndani ya uwanja kulisababisha mechi hiyo kuwa ya upinzani mkali. Baada ya mchezo huo, Kesho (Jumamosi) hakutakuwa na mechi, Jumapili ratiba ya Mapinduzi itaendelea lakini mechi inayosubiriwa kwa hamu ni kati ya Taifa Jangombe dhidi ya Simba SC ambayo inatarajiwa kuwasili Zanzibar kesho (Jumapili).
Wenger aipa shavu Chelsea kubeba ndoo msimu huu. Manager wa Arsenal ambao na wao bado wapo kwenye mbio za kukimbiza ubingwa na kuacha tabia yao ya kuishia nafasi ya nne kila msimu, ameipa shavu Chelsea kushinda ubingwa wa ligi msimu huu. Wenger alikua kwenye mkutano na waandishi wa habari ambapo alisema kwa sasa anaipa nafasi kubwa Chelsea kushindwa ubingwa kwa mwenendo wao,“Kwa sasa Chelsea wana nafasi kubwa kwasababu wametengeneza utofauti mkubwa sana” Wenger aliendelea,“Lakini bado wanaweza kupoteza kama tunavyojua hapa England. Kwasasa wanaonekana kwamba wanaenda kushinda lakini wanaweza kupoteza hapo baadae. Wamejua matatizo yao vizuri na utampa sifa Conte kwa kutatua hayo matatizo”. Kesho Dec 31 Chelsea watakutana na Stoke City na kujaribu kuendelea kuvuna points muhimu ili wajiweke kwenye nafasi nzuri. Mechi kubwa kwa kesho ni kati ya Liverpool Vs Manchester City
2016 umekuwa ni mwaka bora kwa mwamuzi Muingereza, Mark Clattenburg, huenda ukawa ni mwaka ambao hatausahau katika career yake. Clattenburg ,41, ndani ya mwaka huu, ameweza kuchezesha michezo ya fainali tatu kubwa, Fainali ya Kombe la FA, Klabu Bingwa Ulaya pamoja na ile ya Euro kule nchini Ufaransa. Kuonesha kuwa huu umekuwa mwaka muhimu kwake, Clattenburg aliamua kuchora Tattoo za Fainali za UCL Milano na Euro 2016 France ambazo alizichezesha.
KOTEI WA SIMBA UTAMWELEZA NINI KUHUSIANA NA WALI MAHARAGE MWANANGU Kiungo mpya wa Simba, James Kotei, amesema kuwa moja ya vyakula ambavyo vinamfurahisha alivyokutana navyo Bongo ni pamoja na wali na maharage. Kotei ametua Simba katika usajili wa dirisha dogo akitokea nchini Ghana kwa lengo la kuongeza nguvu katika nafasi hiyo ikiwa ni pamoja na kuleta ushindani. Kotei ameeleza kuwa alikuwa na kazi kubwa ya kuzoea vyakula vya Tanzania lakini hicho kimepita bila kupingwa katika mwili wake. “Napenda sana wali na maharage, hicho ndicho chakula ninachokipenda kwa hapa tangu nimefika,” alisema Kotei. SOURCE: CHAMPIONI
KALI ONGALA AGOMA KWENDA AZAM, MAJIMAJI CHINI YA GSM YAMSHAWISHI KUBAKI SONGEA Kocha Kali Ongala ataendelea kubaki bosi wa benchi la ufundi la Majimaji. Tayari Kali alikuwa amemalizana na Azam FC na alitarajia kujiunga na timu hiyo leo kwa ajili ya safari ya Zanzibar. Azam FC iliamua kumchukua Kali kwa kuwa imemfukuza kocha wake Zeben Hernandez na jopo zima kutoka Hispania. Lakini Majimaji chini ya uongozi wa kampuni GSM, imefanikiwa kumbakiza Kali. Habari za uhakika kutoka Majimaji zimeeleza, uongozi wa klabu hiyo umefanikiwa kumshawishi Kali kubaki. “Kweli Kali anabaki na ataendelea kuwa kocha wa Majimaji,” kilieleza chanzo. “Juzi aliwaaga wachezaji kwa kuwa alikuwa ameishazungumza na Azam FC. Lakini baadaye uongozi umemuita na umefanikiwa kumshawishi abaki.” Kuhusiana na Kali, Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba alisema bado wako kwenye mazungumzo na Majimaji ili kumtwaa.
AZAM FC YAZINDUKA, YAILAZA 1-0 PRISONS CHAMAZI Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, usiku wa jana imeiadabisha Tanzania Prisons kwa bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Mchezo huo ulikuwa ni wa mwisho kwa Azam FC mwaka huu kabla ya kuukaribisha mwaka mpya ‘2017’, bao hilo pekee limewekwa kimiani na nahodha John Bocco ‘Adebayor’, dakika ya 40 baada ya kupokea pasi safi ya Joseph Mahundi na kuwahadaa mabeki wa Prisons kisha kupiga shuti la kiufundi lililojaa kimiani. Azam FC iliingia kwenye mchezo huo ikiwa na sura mpya kwenye benchi la ufundi lililosimamiwa na makocha wa timu yake ya vijana, Idd Nassor 'Cheche' na Idd Abubakar na hii ni kufuatia kuwasitishia mikabata wakufunzi kutoka Hispania wakiongozwa na Kocha Mkuu, Zeben Hernandez. Hiyo inamaanisha kuwa makocha hao wa muda wameanza kibarua chao vema kwa kujiandikia rekodi ya kuiongoza Azam FC kushinda mchezo wa ligi katika mechi yao ya kwanza wakiwa benchini. Mabingwa hao wa Ngao ya Jamii waliuanza mchezo huo vema wakifanya mashambulizi kadhaa langoni mwa Prisons, lakini safu yao ya ulinzi ilikuwa imara kuondoa hatari zote wakiongozwa na Salum Kimenya. Alikuwa ni Bocco aliyeihakikishia Azam FC bao la uongozi hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika. Kipindi cha pili Azam FC iliongeza nguvu kwa kuwaingiza Shaaban Idd, Himid Mao na Samuel Afful, lakini jitihada za kusaka mabao zaidi zilishindikana kutokana na uimara wa safu ya ulinzi ya Prisons. Kiungo Frank Domayo, alikaribia kuipatia bao la pili Azam FC dakika ya 50 akiwa anatazamana na kipa wa Prisons, lakini shuti aliloopiga lilitoka pembeni kidogo ya lango la wapinzani wao. Dakika moja baadaye mshambuliaji wa Azam FC, Yahaya Mohammed, alifanya jitihada binafsi za kuwatoka mabeki wa Prisons lakini shuti alilopiga lilitoka nje ya lango la Prisons. Prisons ilipata pigo dakika ya 69 baada ya kiungo wao mkabaji, Kazungu Mashauri, kuonyeshwa kadi nyekundu kufuatia kumfanyia madhambi ya makusudi winga wa Azam FC, Mahundi ambaye alishindwa kuendelea na mchezo huo na nafasi yake kuchukuliwa na nahodha msaidizi, Himid Mao. Hadi dakika 90 zimalizika ubao wa matokeo ulikuwa ukisomeka vilevile na hivyo kufanya Azam FC kuondoka na pointi zote tatu zinazoifanya kufikisha jumla ya pointi 30 katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikizidiwa pointi 14 na kinara Simba (44) na 10 kwa upande wa Yanga waliojikusanyia 40. Huo ni ushindi wa kwanza wa Azam FC kwenye mechi za mzunguko wa pili wa ligi baada ya kuanza vibaya kwa kutoka sare mechi mbili mfululizo dhidi ya African Lyon (0-0) na Majimaji (1-1). Azam FC kwa sasa inaelekea kwenye changamoto nyingine ya kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi, ambapo itaanza kufungua dimba Jumatatu ijayo kwa kucheza na Zimamoto saa 10.15 jioni ndani ya Uwanja wa Amaan, visiwani Zanzibar. Kikosi cha Azam FC leo; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Yakubu Mohammed, Stephan Kingue, Salum Abubakar, Frank Domayo, Yahaya Mohammed/Shaaban dk 64, John Bocco/Samuel Afful dk90, Joseph Mahundi/Himid dk 71.
Alhamisi, 29 Desemba 2016
NGASSA SASA RUKSA KUCHEZA MBEYA CITY, ITC YAKE YAFIKA Na Mwandishi Wetu, MBEYA KIUNGO Mrisho Khalfan Ngassa sasa yuko huru kuchezea klabu yake mpya, Mbeya City ya hapa baada ya kupatiwa Hati yake ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC). Mwenyekiti wa Mbeya City, Mussa Mapunda ameiambia Bin Zubeiry Sports - Online leo kwamba ITC ya Ngassa aliyekuwa anachezea Fanja ya Oman imefika nchini asubuhi ya leo. Mapunda amesema kwamba anawashukuru Fanja, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Chama cha Soka Oman (OFA) ambao kwa pamoja wamefanikisha kupatikana kwa ITC hiyo. Mrisho Ngassa sasa yuko huru kuchezea Mbeya City baada ya kupatiwa ITC yake “Ni kweli tumeipata, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Shirikisho la Soka nchini, TFF, Chama cha Mpira cha Oman, hakika wamefanya kazi kubwa kufanikisha kupatikana kwa ITC hii na pia naishukuru Fanja FC na watendaji wote kwenye timu yetu, tumekuwa na mawasiliano mazuri muda wote mpaka tumefanikiwa,” alisema. Mapunda alisema kwamba kuchelewa kufika kwa ITC hiyo hakukuwa na msuguano wowote baina ya klabu hizo mbili, bali kilichokuwa kinatokea ni tofauti ya wakati na siku za ufanyaji kazi kwenye ofisi kulingana na taratibu za nchi hizo mbili, yaani Oman na Tanzania. “Hakukuwa na msuguano wowote uliosababisha kuchelewa kwa ITC hii, kilichokuwepo ni utofauti wa taratibu za kiofisi, mara nyingi Oman siku za Ijumaa na Jumamosi inakuwa ni mapumiko na huku kwetu Jumapili inakuwa mapumziko, hapo ndipo palikuwa panatuletea mpishano, jambo jema ni kuwa tayari tumeipata na tunaweza kumtumia mchezaji kwenye michezo yote ya ligi na mingine ambayo inaihusu klabu yetu,” alisema. Katika hatua nyingine Mapunda alisema kwamba maandalizi kuelekea mchezo wao ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumamosi dhidi ya Mbao FC Uwanja wa Sokoine mjini hapa yanaendelea vizuri na lengo lao ni kushinda baada ya suluhu katika michezo yao miwili iliyopita.
SIMBA WALEEE, YANGA WANAISOMA NAMBA...RUVU AFA 1-0 BAO pekee la kiungo Mohammed ‘Mo’ Ibrahim limetosha kuipa Simba ushindi wa 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Ni ushindi huo ambao unaifanya Simba SC ifikishe pointi 44 baada ya kucheza mechi ya 18 na kuendelea kuogoza Ligi Kuu kwa pointi nne zaidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC. Mo aliyesajiliwa Simba SC msimu huu kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro, alifunga bao hilodakika ya 45 akimalizia krosi ya beki wa kulia, Janvier Besala Bokungu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Simba ilipata bao hilo, baada ya kukosa mengine zaidi ya matatu ya wazi na pongezi zimuendee kipa chipukizi wa Ruvu Shooting, Bidii Hussein aliyeokoa hatari nyingi.
LIVE KUTOKA UWANJA WA UHURU: RUVU SHOOTING VS SIMBA (MAPUMZIKO) MAPUMZIKO GOOOOOOOOO, Mpira wa krosi safi, Mo Ibrahim anaunganisha kwa shuti kali kabisa hapa -Kona safi inachongwa hapa, Banda anajitishwa vizuri hapa. Goal kick -Simba wanaingia vizuri kabisa, Zimbwe anapiga krosi lakini Makwaya anaokoa, konaaa DAKIKA 3 ZA NYONGEZA Dk 45 sasa, mpira mwingi unachezwa katikati zaidi Dk 43, nafasi nyingine kwa Simba, MZamiru anauwahi mpira ukizagaa anaachia shuti kali lakini unapita juuuu KADI Dk 41, kipa Bidii Hussuein analambwa kadi ya njano kwa kupoteza muda Dk 40, Simba wanapoteza nafasi nyingine ya wazi, Pastory anashindwa kulenga KADI Dk 38, Jabir Aziz Stima analambwa kadi ya njano kwa kumrushia daruga Athanas Dk 36, mkwaju wa adhabu wa Abdi Banda unapigwa na kupaa juu ya lango DK 32, Zimbwe anaingia vizuri lakini JKT wanakuwa wepesi kuokoa Dk 29, Shooting wanafanya shambulizi kali hapa, kona. Hii ni kona ya kwanza ya Ruvu leo Dk 26, Mo Ibarahim anaachia mkwaju mkali lakini Juhudi anadaka kwa ustadi mkubwa hapa Dk 20, Ruvu wanaonekana kuwa na kasi zaidi na kuanza ksuhambulia kwa kasi zaidi DK 14, krosi safi, mpira unapigwa na kugonga mwamba. Lakini sasa kipa wa Ruvu yuko chini akitibiwa Dk 13, Mo Ibra anaingia vizuri hapa ndani ya 18, Ruvu wanaokoa na kuwa konaaaaa Dk 11, mpira umesimama hapa Kisiga akiwa anatibiwa hapa Dk 9, Simba wanafanya shambulizi la haraka, Mwanjale anapanda akigongeana na wenzake, anatoa krosi safi kwa Pastory, yeye na nyavu anapaishaa buuuuu Dk 6, Simba wanaendelea kulisakama lango la Ruvu, Mo Ibra anaingia vizuri na kupiga shuti kali, kipa anadaka mpira unamtoka lakini anawahi Dk 4, krosi nzuri ya Kichuya, Athanas anaunganisha tena, lakini Shooting wanaokoa Dk 2, krosi safi ya Zimbwe, Athanas anapiga kichwa hapa lakini ni goal kick Dk 1, Simba wanaanza kwa kasi wakionekana wamepania kupata bao KIKOSI CHA SIMBA 1. Daniel Agyei 2. Besaka Bukungu 3. Mohammed Hussein 4. Abdi Banda 5. Method Mwanjale 6. Jonas Mkude 7. Shiza Kichuya 8. James Kotei 9. Pastory Athanas 10.Muzamiru Yassin 11. Mohammed Ibrahim
LIVE KUTOKA UWANJA WA UHURU: RUVU SHOOTING VS SIMBA DK 14, krosi safi, mpira unapigwa na kugonga mwamba. Lakini sasa kipa wa JKT yuko chini akitibiwa Dk 13, Mo Ibra anaingia vizuri hapa ndani ya 18, JKT wanaokoa na kuwa konaaaaa Dk 11, mpira umesimama hapa Kisiga akiwa anatibiwa hapa Dk 9, Simba wanafanya shambulizi la haraka, Mwanjale anapanda akigongeana na wenzake, anatoa krosi safi kwa Pastory, yeye na nyavu anapaishaa buuuuu]Dk 6, Simba wanaendelea kulisakama lango la Ruvu, Mo Ibra anaingia vizuri na kupiga shuti kali, kipa anadaka mpira unamtoka lakini anawahi Dk 4, krosi nzuri ya Kichuya, Athanas anaunganisha tena, lakini Shooting wanaokoa Dk 2, krosi safi ya Zimbwe, Athanas anapiga kichwa hapa lakini ni goal kick Dk 1, Simba wanaanza kwa kasi wakionekana wamepania kupata bao KIKOSI CHA SIMBA 1. Daniel Agyei 2. Besaka Bukungu 3. Mohammed Hussein 4. Abdi Banda 5. Method Mwanjale 6. Jonas Mkude 7. Shiza Kichuya 8. James Kotei 9. Pastory Athanas 10.Muzamiru Yassin 11. Mohammed Ibrahim
LIVE KUTOKA UWANJA WA UHURU: RUVU SHOOTING VS SIMBA. Dk 11, mpira umesimama hapa Kisiga akiwa anatibiwa hapa Dk 9, Simba wanafanya shambulizi la haraka, Mwanjale anapanda akigongeana na wenzake, anatoa krosi safi kwa Pastory, yeye na nyavu anapaishaa buuuuu]Dk 6, Simba wanaendelea kulisakama lango la Ruvu, Mo Ibra anaingia vizuri na kupiga shuti kali, kipa anadaka mpira unamtoka lakini anawahi Dk 4, krosi nzuri ya Kichuya, Athanas anaunganisha tena, lakini Shooting wanaokoa Dk 2, krosi safi ya Zimbwe, Athanas anapiga kichwa hapa lakini ni goal kick Dk 1, Simba wanaanza kwa kasi wakionekana wamepania kupata bao KIKOSI CHA SIMBA 1. Daniel Agyei 2. Besaka Bukungu 3. Mohammed Hussein 4. Abdi Banda 5. Method Mwanjale 6. Jonas Mkude 7. Shiza Kichuya 8. James Kotei 9. Pastory Athanas 10.Muzamiru Yassin 11. Mohammed Ibrahim
KIKOSI CHA RUVU SHOOTING IKIIVAA SIMBA LEO UWANJA WA UHURU KIKOSI 1. Bidii Husein 18 2. Abdul Mpambika 12 3. Yusuph Nguya 2 4. Damas Makwaya 20 5. Renatus Kisase 5 6. Baraka Mtuwi 15 7. Jabiri Azizi 25 8. Shabani Kisiga 10 9. Fully Maganga 28 10. Ismail Mgunda 27 11. Abdurahman Musa 17 Sub Elias Emanuel 30 Said Madega 19 Frank Msese 16 Shabani Msala 22 Chande Magoja 21 Ayoub Kitala 7 Said Dilunga 3
IDDI CHECHE APEWA MIKOBA YA ZEBEN HUKU AZAM IKIMSUBIRI KALI ONGALA Azam FC imekiri kuanza mazungumzo na Kocha Kali Ongala ili ajiunge na kuanza kufiundisha. Azam FC imemtimua kocha wake wake, Zeben Hernandez raia wa Hispania pamoja na jopo zima alilokuwa akiliongoza. Lakini kwa sasa kikosi chao kitanolewa na Iddi Cheche na Iddi Aboubakary wakati mazungumzo na Majimaji kumng'oa Kali yakiendelea. Cheche ni mmoja wa makocha wa timu ya vijana ya Azam FC. Pamoja na hivyo, uongozi wa Yanga umekiri kwamba unasaka kutoka nje. Taarifa zimeeleza, Azam FC imefanya mazungumzo na Lamine N'Diaye aliyewahi kuifundisha TP Mazembe na timu ya taifa ya Senegal.
RASMI CARLOS TEVEZ ATUA KLABU YAKE YA CHINI, NDIYE ANAYELIPWA ZAIDI Mshambuliaji Carlos Tevez sasa rasmi ni mchezaji wa Shanghai Shenhua ya China. Tevez atakuwa akilipwa pauni 615,000 kwa wiki na sasa ndiye mchezaji anayelipwa zaidi kuliko wote. Siku kadhaa zilizopita, Tevez aliyewahi kukipiga Manchester United aliaga kwenye klabu yake ya Boca Junior.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)