Straika chipukizi wa Manchester United, Marcus Rashford amepigwa mkwara na kocha wa timu yake ya taifa ya England, Sam Allardyce kuwa anaweza kupoteza nafasi ya kumuita katika timu ya taifa ikiwa ataendelea kuwekwa nechi katimu klabu yake. Allardyce amesema hayo wakati huu ambapo anajiandaa kutangaza kikosi ambacho kitacheza dhidi ya Slovakia, mapema mwezi ujao. Rashford ambaye alionyesha uwezo wa juu msimu uliopita katika kikosi cha vijana kabla ya baadaye kufanya hivyo katika kikosi cha wakubwa cha Man United amekosa nafasi ya uhakika tangu msimu huu uanze chini ya Kocha Jose Mourinho ambaye amekuwa akimtumia zaidi Zlatan Ibrahimovic. Allardyce amenukuliwa akisema: “Ugumu ni kuwa Rashford hachezi inanipa wakati mgumu kumchagua. Naweza kufanya uamuzi wa kumwambia akacheze katika timu ya vijana ya U-21 ili azoee mikiki ya kimataifa, hiyo itamsaidia kupata nafasi hati katika klabu yake nma kisha timu ya taifa.” Kauli hiyo ni kama mwiba kwa chipukizi huyo kwa kuwa ili apate nafasi anatakiwa kufanya kazi ya ziada mbele ya mkongwe Zlatan ambaye tangu atue kikosini hapo ameonekana kuwa hatari katika kufunga. Aidha, Allardyce amesema kuwa anaweza kumpa nafasi Joe Hart lakini naye anatakiwa kupambana kupata namba kikosini kwake Manchester City ambapo amekosa uhakika wa kucheza tangu timu hiyo iwe chini ya Kocha Pep Guardiola. RATIBA YA MECHI ZA ENGLAND Septemba 4: Slovakia vs England Kufuzu World Cup Oktoba 8: England vs Malta Kufuzu World Cup Oktoba 11: Slovenia vs England Kufuzu World Cup Novemba 11: England vs Scotland Kufuzu World Cup Novemba 15: England vs Spain Kirafiki
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni