Jumatatu, 22 Agosti 2016

WENGER: ATOA MATUMAINI MAPYA KWA ARSENAL JUU YA USAJILI WA MUSTAFI

Arsene Wenger anaamini Arsenal watakamilisha usajili wa beki wa Valencia Shkodran Mustafi kabla ya dirisha kufungwa rasmi. Kwa muda mrefu Arsenal wamekuwa wakihusishwa na usajili wa beki huyo wa Kijerumani lakini dili hilo bado linaonekana kusuasua, hali iliyopelekea hali ya sintofahamu kwa mashabiki wa klabu hiyo kutokana na ukosefu wa usajili wa maana kwenye timu hiyo. Wenger amesisitiza bado maridhiano yanaendelea kati ya pande mbili lakini hakusita kuonesha kufedheheshwa na ukosefu wa wachezaji aliowahitaji. “Mustafi? Naamini tutakamilisha hilo suala,” alisema Wenger. “Bado tunapambana kuhakikisha tunapata wachezaji tunaowahitaji. “Ni moja ya wachezaji tunaowahitaji kwa kiasi kikubwa. Bado tunaendelea na maridhiano.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni