KABLA ya mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Mtibwa Sugar huko Manungu Complex, Turiani, Morogoro, ofisa habari wa timu ya Ruvu Shooting ya Pwani, Masau Bwire alipost picha katika akaunti yake ya facebook ‘akila muwa.’ Shooting ilikuwa ikicheza game yake ya kwanza baada ya kurejea ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Mtibwa. Bwire mtu mwenye kupenda utani na mwenye kupendelea kuisifia sana timu yake, aliandika pia katika picha yake hiyo: “Tutawatafuna kwa staili hii Mtibwa Sugar hapa Manungu Complex leo August 20, 2016,” na ndicho kilichokuja kutokea baada ya dakika 90.’ Wameendeleza rekodi ya kupoteza mchezo wowote, kati ya 15 waliyokwisha cheza. Hawakupoteza katika game zao zote za ligi daraja la kwanza msimu waliopita, na bao la mkwaju wa faulo la kiungo ‘maestro’ siku ya Jumamosi iliyopita lilitosha kuwapa ushindi wa kwanza katika VPL tena wakicheza ugenini dhidi ya mabingwa wa miaka ya 1999 na 2000, timu ya Mtibwa Sugar. Shooting imeendelea kucheza mechi za ligi za juu Tanzania Bara pasipo kupoteza. Mechi 15 mfululizo pasipo kupoteza, Ruvu Shooting wanaweza kushangaza msimu huu?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni