Beki mtata wa Liverpool, Mamadou Sakho amerejea mazoezini chini ya Kocha Jurgen Klopp baada ya kuwa nje kwa muda kutokana na kuwa majeruhi ambapo mpaka sasa ameshakosa mechi mbili za Premier League za timu yake. Beki huyo ambaye amekuwa katika mvutano na klabu yake kutokana na matukio yake ya kuonyesha utovu wa nidhamu ikiwemo kufukuzwa katika kambi ya timu hiyo ilipokuwa Marekani, alionekana katika mazoezi ya leo akiwa na wenzake sambamba na straika wa timu hiyo, Sadio Mane ambaye alikuwa majeruhi kwa kuumia bega. Sakho ambaye pia alikuwa na kashfa ya kutumia dawa za kuongeza nguvu michezo inaelezwa kuwa anaweza kuwa na wakti mgumu kupata namba kikosini hapo kutokana na kuonyesha kutoivana na bosi wake huyo wa benchi la ufundi. Sakho Wakati akiondolewa kambini Marekani, Klopp alilalamika tabia za beki huyo raia wa Ufaransa kuwa alikuwa akionyesha utovu wa nidhamu hadharani jambo ambalo lingeweza kuigawa timu wakati yeye anataka timu iwe kitu kimoja. Wakati huohuo kuna taarifa kuwa Liverpool inafanya mpango wa kumtoa beki huyo mwenye umri wa miaka 26 kwa mkopo kwenda timu nyingine. Dejan Lovren na Emre Can Klopp aliwasajili Joel Matip na Ragnar Klavan ili kuongeza nguvu katika safu ya ulinzi wa kati jambo ambalo linampa ugumu Sakho kwa kuwa pia bado Dejan Lovren ana uhakika wa kucheza katika nafasi hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni