pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumatano, 31 Agosti 2016
KAKA YAKE POGBA ASAJILIWA UHOLANZI
ACACIA YAVUNJA RASMI MKATABA NA STAND UNITED, WALIOIKIMBILIA KAZI KWAO
WARAKA WA HART WENYE HUZUNI KUBWA KWENDA KWA MASHABIKI WA MAN CITY
OFFICIAL- STOKE CITY WAKAMILISHA USAJILI WA BONY
GENK YAITAHADHARISHA TFF JUU YA SAMATTA
ILE ISHU YA AZAM FC, YANGA YASEMA POA TU, IKO TAYARI KWENDA CHAMAZI
Matumizi ya fedha kwenye usajili katika Ligi Kuu ya England yamepita pauni BILIONI moja kwa mara ya kwanza. Hii inamaanisha timu 13 kati ya 20 ZIMEVUNJA REKODI ZAKE ZA UHAMISHO msimu huu. Ifuatayo ni orodha ya wachezaji na timu walizokwenda pamoja na ada ya uhamisho ambao umevunja rekodi za klabu katika kununua mchezaji mmoja. Manchester United: Paul Pogba (£93.25m) Liverpool: Sadio Mane (£36m) Crystal Palace: Christian Benteke (£32m) West Ham: Andre Ayew (£20.5m) Leicester: Ahmed Musa (£16m) Southampton: Sofiane Boufal (£16m) Swansea: Borja Baston (£15.5m) Bournemouth: Jordon Ibe (£15m) Sunderland: Didier N'Dong (£13.6m) Hull: Ryan Mason (£13m) West Brom: Nacer Chadli (£13m) Watford: Roberto Pereyra (£13m) Burnley: Jeff Hendrick (£10.5m)
MSUVA AZUNGUMZIA DAKIKA 540 ZA YANGA AMBAVYO NI MUHIMU ZAIDI
KOCHA MHISPANIA WA AZAM FC ASEMA MAREKEBISHO KIDOGO TU YANATAKIWA AZAM FC IANZE YAKE
Wanawake walioolewa au walio katika mahusiano mara kwa mara hulalamika juu ya vituko mbalimbali wanavyofanyiwa na mawifi zao ambavyo hupelekea kufarakana na waume zao. - Wachache sana huweza kuhimili maneno na visa vya mawifi. Mdau wetu wa JamiiForums anauliza ni mbinu ipi aitumie kumdhibiti wifi yake?
Nchi saba, ikiwemo wenyeji Uganda, watashiriki katika michuano ya Cecafa 2016 ya wanawake mwezi Septemba. Kenya, Burundi, Zanzibar, Ethiopia, Tanzania bara na Rwanda watashiriki. Michuano hii imethibitishwa na shirikisho la soka la Afrika Mashariki na Kati- Cecafa - mjini Kampala. Katibu mkuu wa Cecafa Nicholas Musonye amesema walitarajia kupata timu moja kutoka kusini mwa Afrika lakini hawakufanikiwa. Rais wa shirikisho la soka la Uganda Injinia Moses Magogo amesema: "Tumefurahi kuandaa michuano hii. Huu ni muendelezo wa mradi wa mkakati wa kukuza soka la wanawake nchini Uganda na katika eneo zima." Michuano hiyo itaanza Septemba 11 hadi 20 katika mji wa Jinja. Burundi na Zanzibar zitacheza katika mechi ya ufunguzi. makundi ni kama ifuatavyo. Kundi A: Uganda, Kenya, Burundi, Zanzibar Kundi B: Ethiopia, Tanzania bara, Rwanda.
KANUNI 30 KWA WANAWAKE NDANI YA NDOA 1). Usinyanyue sauti mbele ya mumeo kwa sababu yoyote ile. Hiyo ni ishara ya utovu wa heshima. 2). Usifichue udhaifu wa mumeo kwa familia na marafiki zako. Itakurudia. Wewe ni mlinzi wa mumeo, naye ni mlinzi wako. 3). Usitumie mhemko yako hasi kuwasiliana na mumeo, hujui namna mumeo atakavyoitafsiri. Wanawake wenye hulka ya kujihami huwatengenezi nyumba yenye furaha. 4). Usimlinganishe mumeo na wanaume wengine, hujui maisha yao halisi yalivyo. Ukiibomoa hadhi yake, upendo wake kwako utashuka. 5). Usiwatendee vibaya marafiki wa mumeo kwa sababu huwapendi, mtu anayetakiwa kuwa wa kwanza kujitenga nao ni mumeo. 6). Usisahau kuwa mumeo alikuoa, yeye si mfanyakazi wako au mtu mwingine tofauti. Tekeleza majukumu yako. 7). Usimpe mtu mwingine fursa ya kumhudumia mumeo, watu wanawaweza kufanya mambo mengine, lakini huduma za mumeo ni jukumu lako mwenyewe. 8). Usimlaumu mumeo akija nyumbani mikono mitupu. Badala yake mpe nguvu, mhamasishe na kumshajiisha. 9). Usiwe mke mwenye matumizi ya hovyo, jasho la mumeo halitakiwi kutumiwa hovyo. 10). Usijifanye kuwa mgonjwa kwa lengo la kumnyima tendo la ndoa. Mpe kwa namna apendavyo. Tendo la ndoa ni muhimu sana kwa wanaume, ukiendelea kumnyima haitachukua muda mrefu kabla mwanamke mwingine hajatimiza jukumu hilo. Hakuna mwanaume anayeweza kustahmili kukosa tendo la ndoa kwa muda mrefu. 11). Usimlinganishe mumeo na mwanaume wako wa zamani kitandani. Ukifanya hivyo, nyumba yako inaweza kupata mtikisiko wa aina yake. 12). Usijibishane na mumeo hadharani. Hilo litashusha hadhi na heshima yake. Hitajio namba moja la mwanaume ni heshima. 13). Usimpe changamoto mumeo mbele ya watoto. Wanawake wenye busara hawafanyi hivyo. 14). Usisahau kumuandaa mumeo na kuhakikisha kuwa yuko maridadi kabla hajatoka nyumbani. 15). Usiruhusu marafiki zako kuwa karibu mno na mumeo. 16). Usiwe na haraka unapokuwa bafuni na kwenye dressing table. Huko nje mumeo anakutana na wanawake ambao wanatumia muda wao kujiremba vizuri bila haraka yoyote ili waonekane maridhawa. 17). Wazazi au familia yako hawana uamuzi wa mwisho katika ndoa yenu. Endelea kuwaheshimu, lakini wasiwe na uamuzi wa mwisho kuhusu ndoa yenu. 18). Usiegemeze upendo wako kwenye vitu vya pesa. Endelea kumheshimu mumeo licha ya kwamba unapata pesa zaidi yake. 19). Usisahau kuwa mume anahitaji mtu anayemakinika naye na kumsikiliza vizuri, hivyo unapozungumza naye acha mambo mengine. Mawasiliano mazuri ndiyo msingi wa nyumba yenye furaha. 20). Iwapo mawazo yako yamefanikisha jambo kuliko mawazo yake, usijilinganishe naye. Bali ishini na mfanye kazi kama timu. 21). Usiwe msumbufu kwa mumeo. Hakuna mume anayependa mke msumbufu. 22). Mke mvivu hajali. Hata hajui kwamba anatakiwa kuoga na kuwa msafi. 23). Je, mumeo anapenda chakula fulani? Kuwa makini sana kwenye namna ya utayarishaji wa chakula. Hakuna mume anayefanya maskhara na suala la chakula. 24). Usiwe mtu wa kumkamua sana mumeo, ukataka kila kitu uwe nacho wewe. Furahia kile kinachopatikana kulingana na uwezo wake. 25). Ifanye glasi ya maji kuwa ukaribisho wa kwanza kwa mumeo na kwa kila mgeni anayeingia nyumbani kwenu. Ukarimu maridhawa ndiyo uzuri wa kweli. 26). Usisuhubiane na wanawake wenye mtazamo hasi na wa kimakosa kuhusu ndoa. 27). Ndoa yako itakuwa na thamani kama utaipa thamani. Uzembe na kutojali ni sumu ya ndoa. 28). Watoto ni zawadi adhimu kutoka kwa Mungu, wapende na uwafunze mambo mazuri. 29). Umri usiwe kikwazo cha kuwa na ushawishi kwenye nyumba yako. Kamwe usipunguze kiwango cha huduma kwa familia yako kwa hali yoyote ile. Ifanye huduma yako kuwa yenye kujaa ubunifu maridhawa. 30). Mke anayemuabudu Mungu ni mke maridadi, daima muombee mumeo na familia yako. Ninakutakia ndoa njema. Usisahau ku share na wenzako kusambaza ujumbe huu muhimu...
Jumanne, 30 Agosti 2016
MBEYA CITY NAO WAMO, WAFUNGULIWA KESI RUNDO ZA KUTOLIPA MISHAHARA
OFFICIAL- ARSENAL WAMEMSAJILI PEREZ KUTOKA DEPORTIVO LA CORUNA
BARCELONA WAMEKAMILISHA USAJILI WA MCHEZAJI MWINGINE
SIMBA KUMBURUZA KESSY MAHAKAMANI
FA YAMKUTA NA HATIA AGUERO, SASA KUPIGWA PINI MECHI TATU
HAZARD AMFANANISHA KANTE NA PANYA
Eden Hazard amemfananisha kiungo mpya wa Chelsea N’Golo Kante na panya kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuzunguka uwanja mzima pindi awapo uwanjani . Nyota huyo wa Ubelgiji amevutiwa sana na aina ya uchezaji wa Kante kutokana na matumizi yake makubwa ya akili na nguvu panapohitajika. Kante, ambaye ni raia wa Ufaransa msimu uliopita alishinda kombe la EPL akiwa na Leicester City kabla ya kuhamia Darajani msimu huu. Hazard aliimabia Chelsea TV: ‘Anatupa uwezo mkubwa wa kujiamini. Mara nyingi huwa tunajaribu kupiga chenga na kuwapita wapinzani, lakini huwa tunafanya hivyo tukiamini kwamba hata tukipoteza mpira kuna mtu yupo nyuma yetu kwaajili ya kutulinda. ‘Ni mchezaji wa aina yake. Ni kama panya vile, anazunguka uwanja mzima na ana fikra za upambanaji sana, kwa ufupi ni mchezaji wa kiwango cha juu kabisa. ‘Mara nyingi ni faraja sana kucheza na wachezaji wa kiwango cha juu.’