Ijumaa, 30 Septemba 2016

MADOGO WA SERENEGETI BOYS WAKO TAYARI KWA KIBARUA CHA KESHO DHIDI YA "MZIGO WA MNYAMWEZI"

Kumekuwa na hofu kwamba Congo wanachezesha vijeba katika mechi zao za vijana chini ya umri wa miaka 17 kuwania kucheza Kombe la Mataifa Afrika. Lakini timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, iko tayari kwa kazi hiyo ngumu unayowezeka kuilinganisha na mzigo wa Mnyamwezi. Kesho Jumapili inacheza mechi muhimu ya kuwania kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Vijana 2017 dhidi ya Congo Brazzaville. Mchezo wa marudiano utachezwa kwenye Uwanja wa Alphonse Massamba Debat na katikati atasimama mwamuzi Pacifique Ndabihawenimana wa Burundi akisaidiwa na Pascal Ndimunzigo na Gustave Baguma. Serengeti Boys inayonolewa na Bakari Shime inacheza mechi hiyo baada ya awali kushinda mabao 3-2 nyumbani kwenye Uwanja wa Taifa, na ikiitoa Congo itakuwa imefuzu kucheza fainali hizo za Afrika. Kikosi cha timu hiyo tayari kipo Congo baada ya kuwa kambini nchini Rwanda kujiandaa na mchezo huo. Serengeti ikifanya vizuri itafuzu kushiriki fainali hizo za 12 za michuano hiyo ya vijana. Fainali hizo zitashirikisha timu nane za Afrika wakiwemo wenyeji Madagascar na michuano imepangwa kuanza Aprili 2 hadi 16, 2017 katika miji miwili ya nchi hiyo.

OKTOBA 1: YAMKUDE NIHAYA ANAVYOWASHANGAA YANGA NA KUTAKA KUWAPIGA HAT TRICK YA VIPIGO

Mara ya tatu? Haiwezekani. Hiyo ni kauli ya nahodha wa Simba, Jonas Mkude, akisema hawapo tayari kufungwa mara ya tatu mfululizo na Yanga wakati timu hizo zinapokutana leo. Yanga na Simba leo zinacheza mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku kukiwa na kumbukumbu ya Simba kufungwa na Yanga mechi mbili zilizopita. Mkude ambaye amekuwa nguzo muhimu kwenye kiungo cha Simba, alisema mchezo wa leo ni muhimu zaidi kwao na wana lengo la kushinda. “Haitapendeza kuona tunapoteza mechi hii dhidi ya Yanga kutokana na mambo mawili yaliyopo mbele yetu, kwanza tunataka ubingwa, hivyo tumekubaliana kushinda kila mechi ikiwemo hii na Yanga. “Pili, hatuwezi kukubali kufungwa mechi ya tatu mfululizo na Yanga kwani msimu uliopita wametufunga mechi zote mbili, hii inatuumiza na tumepanga kufuta vipigo hivyo,” alisema Mkude. “Tumefanya maandalizi ya kutosha, tutaingia uwanjani tukiwa na ari ya kupambana kutokana na matokeo ya mechi zetu za nyuma na tuna morali ya kuwa kileleni, hivyo hatutaki kupoteza mechi.” “Hakuna namna, lazima tushinde mchezo huu ili kufikia malengo tuliyojiwekea, kama tukifungwa itakuwa aibu kwetu kufungwa na Yanga mechi tatu mfululizo,” alisema Mkude.

OKTOBA 1: SIKIA HII KUTOKA KWA MSUVA AMTANGAZA ZIMBWE JR WA SIMBA KUWA NDIYO NJIA YAKE YA MAFANIKIO LEO MSUVA AMTANGAZA ZIMBWE JR WA SIMBA KUWA NDIYO NJIA YAKE YA MAFANIKIO LEO

Beki wa kushoto wa Simba, Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jr’, maarufu kama Tshabalala, amesema ataweka ulinzi mkali kwa mawinga wa Yanga wasipite kwake leo, lakini Simon Msuva amesema atapita hukohuko katika upande wake. Yanga na Simba zinacheza leo mchezo namba 43 wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo tayari Tshabalala ameshapiga mkwara kwamba hataruhusu mtu kupita upande wake. Kwa upande wake, Msuva ambaye ni winga anayemudu kucheza upande wa kulia, alisema: “Nimemsikia Tshabalala akitamba kuwa hatuogopi, mimi namwambia tutaonana uwanjani “Ninaamini nitafanya kazi yangu kama kawaida na nitapitia hukohuko alipo yeye (Tshabalala) kwani nimefanya mazoezi makali kujiandaa na mchezo huu.” Msuva alisema hapendi kumzungumzia mchezaji wa timu pinzani, lakini amelazimika kutoa kauli hiyo kwa Tshabalala ili kuwatoa hofu mashabiki wa Yanga wanaodhani anaweza kuzuiwa na beki huyo. “Tshabalala yeye kama anaongea hivyo, mwacheni tu, lakini kikubwa anatakiwa kutambua kuwa soka linachezwa uwanjani na siyo mdomoni,” alisema Msuva ambaye hadi sasa ana bao moja katika ligi.

EPL Leo. BBC Ulimwengu wa Soka itakutangazia mechi kati ya Hull v Chelsea







NIWAKATI WA MADRID SASA SITA WA MADRID WAITWA TIMU YA TAIFA HISPANIA NA KUWEKA REKODI NYINGINE

Wachezaji sita wa Real Madrid wameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Hispania na kuweka rekodi. Takribani miaka 13 sasa, haiku rahisi wachezaji wengi wa Madrid kuitwa kwa wingi lakini safari hii Kocha Julen Lopetegui kwaida sita timu hiyo maarufu kama Los Bloncos. Sita walioitwa na Lopetegui ni Isco, Alvaro Morata na Lucas Vazquez kwa ajili ya ushambulizi, halafu Nacho, Sergio Ramos na Dani Carvajal katika ulinzi. Wachezaji hao ni kwa ajili ya maandalizi ya mechi mbili, kwanza Italia halafu Albania.  Mara ya mwisho wachezaji sita wa Madrid kuitwa kwa wakati mmoja ilikuwa mwaka 2003 walipoitwa akin Iker Casillas, Ivan Helguera, Raul Bravo, Michel Salgado, Guti na Raul.

JOTO LA OKTOBA 1 VIFAA VYA SANGOMA VYANASWA UWANJA WA TAIFA, YANGA, SIMBA WATUPIANA MZIGO

Unaweza kusema utamu kunoga! Mechi ya watani, Yanga na Simba haikosi vituko. Kuna taarifa kwamba kuna vitu vinavyoashiria hali ya kishirikina vimekamatwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kabla ya mechi ya watani, Yanga na Simba, kesho. Wakati vimekamatwa jana, lakini kila upande unatupa mpira kwa upande mwingine, kwamba ndiyo chanzo au unahusika. Yanga wanasema ni Simba, nao Simba wanasema ni Yanga. Basi ili mradi siku zinasogea na inaendelea kuthibitika kwamba mechi hizo hasa za watani, watu ndiyo riziki zao.

#MTI WANGU, Wana Dar es Salaam Tukutane Oktoba Mosi 1 , Katika Jiji la Mbabe wa Vita Rc.@ Paul C. Makonda


LUIS SUAREZ AANZA TENA MAMBO YAKE MATATANI TENA, ATUHUMIWA KUMTUPIA MATUSI MWAMUZI MSAIDIZI

Mshambuliaji nyota wa Barcelona, Luis Suarez ameingia matatami tena baada ya kukumbana na tuhuma za kumtukana mwamuzi msaidizi, Damir Skomina. Suarez anatuhumiwa kumtukukana mwamuzi huyo wakati wa mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakicheza dhidi ya Borussia Monchengladbach ya Ujerumani na kupata ushindi wa mabao 2-1 wakiwa ugenini Ujerumani. Mruguay huyo inaonekana akizungumza kwa jazba wakati akipinga uamuzi wa mwamuzi huyo na inaonekana alitukana au kutumia lugha chafu. Bado haijathibitika na ikiwa hivyo, basi Suarez atakumbana na adhabu huku kukiwa na kumbukumbu ya matukio kadhaa aliyowahi kufanya yakiwemo yale ya kuwauma mabeki.

OKTOBA 1 YANGA TAYARI WAKO MJINI TAYARI KWA DHIDI YA SIMBA

Kikosi cha Yanga kimerejea jijini Dar es Salaam tayari kwa kazi ya kuwania pointi tatu dhidi ya watani wao Simba. Yanga walikuwa kambini mjini Pemba kujiandaa na mechi hiyo ya leo dhidi ya Simba. Simba waliokuwa Morogoro ndiyo walikuwa wa kwanza kufika jijini Dar es Salaam na wakafanikiwa kufanya mazoezi ya mwisho asubuhi. Mechi hiyo inasubiriwa kwa hamu na presha imezidi kuwa juu zaidi huku kila upande ukionkena kujiamini kwamba una nafasi ya kushinda.

OKTOBA 1 LEO ULINZI MKALI UWANJA WA TAIFA USIKU WA KUAMKIA LEO, MASHABIKI YANGA, SIMBA TAFRANI TUPU

Kumekuwa na tafrani kubwa katika vipindi kadhaa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, hasa usiku huu. Mashabiki na wanachama wa Yanga na Simba, wameendelea kuulinda uwanja huo, kila mmoja akiwa na hofu na mwenzake. Umakini umeongezeka huku kila upande ukiwa na hofu ya mwingine ‘kummaliza’ mwenzake. Pamoja na kulindana, makundi yote yamekuwa yakionekana kutoamini jingine na mara kadhaa wamekuwa wakirushiana maneno. Jana, baadhi ya mashabiki na wanachama wa Yanga, walimpa wakati mgumu mmoja wa wanachama wa Simba aitwaye Makoye wakimtuhumu kuwazidi ujanja na “kufanya mambo yake”. Hali ambayo imesababisha wengi kuwa makini na wakali huku upande wa Simba nao wakijibu mapigo. Suala la ushirikina, limekuwa tatizo kubwa. Pamoja na maandalizi ya vikosi, suala la kutoaminiana na hofu ya kufanyiana ushirikina, imekuwa kubwa sana kila inapofika mechi ya Yanga na SImba.

Yanga SC v Simba SC: ‘Wekundu wa Msimbazi’ watapigwa kwa mara ya 3 mfululizo VPL

KUHUSU kikosi cha Yanga SC kuelekea game ya Jumamosi hii vs Simba SC wala sina shaka nacho, nadhani huu ni wakati wa Simba SC kuendelea kuishi katika mashaka ya ‘Dar es Salaam-Pacha’. Miaka 8 mfululizo pasipo kupoteza game ya mahasimu hao kwa kandanda nchini upande wa Simba ‘imekwishapita’ na ndani ya uwanja wapo katika nyakati ngumu dhidi ya mahasimu wao ambao wameshinda VPL mara tatu ndani ya misimu minne ya mwisho, huku wakipoteza mara moja tu pambano la ‘Watani hao wa Jadi.’ Ndani ya uwanja, Yanga wana timu ‘kabambe’ kuliko Simba inayopewa sifa nyingi katika vyombo vya habari. Katika uchambuzi wa kwenye makaratasi Simba wanaweza kuonekana ni wazuri lakini wanavyocheza hawaonekani kuwa kucheza kitimu zaidi. Ndiyo, wana wachezaji wenye majina, lakini dhidi ya timu inayocheza kitimu kama Yanga watapata shida. Kuna mengi yamebadilika katika timu ya Yanga tangu Mei 7, 2012 walipofungwa 5-0 na mahasimu wao hao, na hilo pia lipo katika timu ya Simba. Yanga wamepandisha kiwango zaidi wakati Simba wamekuwa wakiteremka
. Msimu wa 2012/13 game mbili walizokutana, Yanga walipata ushindi mara moja na kulazimisha sare. Na ushindi pekee wa Simba tangu 2012 ni ule wa 1-0, Machi mwaka uliopita huku Yanga wakishinda tena mara mbili msimu uliopita. Kwa sasa Yanga wapo katika daraja la juu na siri kubwa ya mafanikio yao ni kucheza kitimu licha ya kwamba wana wachezaji wenye uwezo binafsi. Ibrahim Ajib, Laudit Mavugo ‘hawatengenezeani’ nafasi za kufunga, hili ni tofauti kabisa na Amis Tambwe na patna wake Donald Ngoma ambao wamekuwa wakicheza kwa ushirikiano mkubwa na kila mmoja ni mtengenezaji wa magoli ya mwenzake. Viungo wa Simba, Mwinyi Kazimoto na Jonas Mkude, sawa si wachezaji wabaya ila upigaji wao wa pasi ni tofauti kabisa na wale wa Yanga. Pasi nyingi za wachezaji wa kati mwa uwanja upande wa Simba si makini na mipira yao mingi hupotea. Thaban Kamusoko na Haruna Niyonzima wamekuwa na viwango bora katika upigaji wa pasi na jambo hilo litaendelea kuibeba timu timu yao. Beki ya Simba haina kasi na uwepo wa Saimon Msuva, Deus Kaseke, Juma Mahadhi na Geofrey Mwashuiya ni tatizo kwao. Viungo hao wa pembeni wa Yanga watanufaika na kasi yao. Majuto pekee kwa Yanga itakuwa ni kushindwa kufunga katika nafasi watakazotengeneza kwa sababu safu ya ulinzi ya Simba haina uwezo wa kucheza mipira ya juu na Yanga wako vizuri katika mipira hiyo. Yanga inazidi kuwa imara ndani ya uwanja na hilo limekuwa likiwaogopesha hadi wapinzani wao. Watashinda mechi ya 3 mfululizo ya Dar-Pacha, sina shaka na hilo. Wanazuia vizuri, wanashambulia vizuri na wana wafungaji wawili bora wenye usongo na umakini wa kutumia nafasi zinazopatikana. Huu ni wakati wa Yanga kuendelea kuwaweka katika mashaka ya ‘Watani wa Jadi’ mahasimu wao ambao walishindwa kuwafunga katika ligi kwa misimu nane mfululizo miaka ya nyuma (2000-2008). Kupoteza mara moja tu katika misimu minne iliyopita dhidi ya Simba ni hatua, pia dalili za kuashiria wamebadilisha mambo mengi mabaya na kuyageuza kuwa mazuri katika ‘Dar es Salaam-Pacha.’ Yanga v Simba, mwisho wa kuandikia mate ni kesho Jumamosi katika uwanja wa Taifa, ushindi nawapa Yanga SC.

Jumatano, 28 Septemba 2016

Matokeo UEFA Champions League PIQUE SHUJAA, APIGA BAO LA PILI FC BARCELONA IKIIMALIZA MONCHEGLADBACH BAO 2-1 KWAO LIGI YA MABINGWA

B. Gladbach (4-2-3-1): Sommer, Christensen, Wendt, Korb, Elvedi, Kramer, Dahoud, Hazard (Herrmann 80), Stindl (Hahn 83), Traore, Raffael (Johnson 48) Subs not used: Sippel, Vestergaard, Jantschke, Hofmann Goal: Hazard 34  Barcelona (4-3-3): Ter Stegen, Pique, Mascherano, Alba, Roberto, Rakitic (Turan 59), Busquets, Iniesta, Luis Suarez, Neymar, Alcacer (Rafinha 59) Subs not used: Cillessen, Digne, Mathieu, Denis Suarez, Gomes Goals: Turan 65, Pique 74 Booked: Pique, Mascherano, Neymar Referee: Damir Skomina

Matokeo UEFA Champions League CARRASCO AFANYA YAKE ATLETICO MADRID IKIITULIZA BAYERN KWA BAO 1-0 LIGI YA MABINGWA ULAYA

Atletico Madrid: Oblak, Juanfran, Godin, Savic, Luis, Carrasco (Gameriro), Fernandez, Niguez, Koke, Torres, Griezmann Unused subs: Correa, Vrsaljko, Gomez, Thomas, Gaitan, Moreira Goals: Carrasco Bookings: Niguez Bayern Munich: Neuer, Lahm, Boateng (Hummels), Martinez, Alaba, Alonso, Vidal, Thiago (Kimmich), Muller (Robben), Lewandowski, Ribery Unused subs: Rafinha, Ulreich, Coman, Kimmich, Sanches Bookings: Lahm, Thiago

Matokeo UEFA Champions League CELTIC YAING'ANG'ANIA MAN CITY YA GUARDIOLA, YALAZIMIKA KUSAWAZISHA LIGI YA MABINGWA KUWA 3-3

CELTIC (4-2-3-1): Gordon 7; Lustig 6.5, Toure 6.5, Sviatchenko 7.5, Tierney 7; Brown 6.5, Bitton 6 (Griffiths 84); Forrest 6.5 (Roberts 80), Rogic 7 (Armstrong 57), Sinclair 7.5; Dembele 8 Subs not used: De Vries, Simunovic, Gamboa, McGregor Scorers: Dembele 3, Sterling (OG) 20  MAN CITY (4-1-4-1): Bravo 5.5; Zabaleta 6, Otamendi 5.5, Kolarov 5.5, Clichy 6 (Stones 73, 6); Fernandinho 6; Nolito 6.5 (Fernando 76, 6), Gundogan 6, Silva 7, Sterling 7; Aguero 6 Subs not used: Caballero, Sagna, Navas, Sane, Iheanacho Scorers: Fernandinho 12, Sterling 28, Nolito 55 Referee: Nicola Rizzoli (Italy) 7 Star man: Moussa Dembele

Kocha wa Chelsea Antonio Conte, mguu upande mguu sawa

Gascoigne Brian Bado naisubiri kuiona movie yake wapi itakapoishia, maana movie yake imeanza kunoga hata katikati haijafika. Mmoja kati ya wanadamu wanaoamini ulinzi kuliko unyumbulifu wa Hazard, ataamini vurugu za Zuma kule nyuma kuliko ubunifu wa Fabregas. Wakati mwingine udhaifu wa mwanadamu unatokana na kile anachokiamini yeye mwenyewe. Anahitaji sana utulivu wa Terry pale nyuma ili aweze kurudi katika hali ya kimchezo, ila Conte kumbuka maneno ya mwigizaji wa kiingereza mwanamama Audrey Hepburn aliposema NOTHING IS IMPOSSIBLE THE WORD ITS ELF (HAKUNA KITU KIGUMU KAMA NENO LENYEWE). Ulimsikia Conte alichokiongea baada ya kipigo dhidi ya Arsenal? Alisema wachezaji wa Chelsea ni wa makaratasi akiwa na maana ya kuwa wachezaji wake unaweza kuwaogopa wakiwa katika orodha ila si uwezo wakiwa ndani ya uwanja. Naomba uyakumbuke maneno ya Audrey Hepburn. Yule Kante na Matic lazima ukubali kumfunga mmoja mnyororo ili uwiano katika kikosi uwepo. Yule Cahill taratibu anaanza kupoteza kujiamini ndio maana kila wakati anakuwa na makosa mengi pale nyuma. Hesabu hazidanganyi na muda ni wakati nasubiri kuona ujio wa zuma na Terry pale nyuma tuone kitu gani kitatokea pale nyuma naona muunganiko wa Cahill na D.Luiz pale nyuma bado aujawa vizuri. Conte hakikisha miguu yako unaiweka sawa ili uweze kuwa katika mikono salama. Yule Abramovich mmoja kati ya wanadamu wachache sana wanaothamini ubora ulionao kuliko kusubiri utimilifu wako Conte njia pekee ya wewe kukaa salama katika mikono ya Abramovich ni kumpa furaha katika kikosi chako. Yule Kante taratibu ameanza kuchoka sijui kwasababu ya kutumika sana msimu ulioisha, najaribu kuwaza hata sijapata jibu lililo hai dhidi yake.Yule Matic sio wa misimu miwili nyuma ameanza kuchoka kuanzia mwili mpaka miguu yake pia imeonyesha kuanza kuchoka naisubiri sana kuiona hii movie ya Conte dhidi ya wachezaji wake. Nafasi ya yeye pekee kuweza kubaki ubora wake ni kuamua kubadilika kutoka kwenye ugumu na kuja kwenye kunyumbulika ndio sehemu ambayo Abrahimovich anaiwaza kila siku kuona Chelsea ikicheza soka la kuvutia. Ivanovic nilianza kukusahau kuelezea mapungufu yako wewe ndio matatizo zaidi kule nyuma. Conte akiamua kufumba macho na kufumbua jicho la ziada wewe ndio mtu wa kwanza kuondoka katika kikosi mmoja kati ya mchezaji unaekosa usawa dhidi ya wachezaji waliopo pale darajani.

KOCHA WA YANGA AFUNGUKA HII NDIYO KAULI YA PLUIJM KUHUSIANA NA YANGA VS SIMBA

Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm ameibuka na kusema kuwa, mchezo wao na Simba utakuwa mgumu kutokana na kila timu kuhitaji kushinda siku ya Jumamosi. Yanga walipoteza mchezo uliopita baada ya kufungwa bao 1-0 na Stand United ya mkoani Shinyanga na hivyo watakuwa na hasira kwenye mchezo huo wa Jumamosi kutokana na Simba wao kushinda kwa mabao 4-0 dhidi ya Majimaji wikiendi iliyopita. Pluijm amesema, mtazamo wake wote kwa sasa ni kwenye mechi ya watani wa jadi kwa kuona ni jinsi gani timu yake inaweza kufanya vizuri huku akieleza kuwa anahitaji kuweka presha kubwa katika mchezo huo kwa kuwa anaamini kikosi chake kipo vizuri, ingawa mechi ijayo itakuwa ngumu sana. “Bila ya kutarajia tumepoteza mchezo wetu wa kwanza nje ya nyumbani dhidi ya Stand United, nimesikitishwa na matokeo kwa kuwa tulijiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huo na tuliuanza vizuri mchezo. “Stand walicheza kwa mtindo wa kuzuia ambapo wachezaji wao tisa wote waliwaweka nyuma hivyo kufanya washambuliaji wangu kuwa katika wakati mgumu wa kuweza kufunga ikiwa ni pamoja na ubovu wa kiwanja pia ulichangia kufanya mchezo kuwa mgumu. “Tulitengeneza nafasi tatu katika kipindi cha kwanza na vilevile katika kipindi cha pili tulipata nafasi kama hizo lakini hatukufanikiwa kupata nafasi ya kufunga na iwapo tungefunga katika kipindi cha kwanza ingetusaidia, Stand walipata nafasi mbili katika kipindi cha pili na walifanikiwa kufunga bao moja kutokana na makosa yaliyofanywa na safu yangu ya ulinzi , lakini huo ndiyo mpira. “Mpira siku zote ni mchezo wa makosa na timu itakayofanya makosa machache ndiyo inayoshinda lakini kwa sasa naangalia mechi dhidi ya Simba ambayo ni mchezo mwingine utakaokuwa mgumu unaokutanisha timu mbili ambazo zote zinahitaji kushinda. “Nimekiandaa vizuri kikosi changu kuelekea mchezo huo, sihitaji kuweka presha kubwa kwa wachezaji wangu kueleka mchezo huo naamini tutafanya vizuri lakini wote kwa ujumla wapo fiti,” alisema Pluijm.

OKTOBA 1, UTAM KUNOGA HAYA NDIYO ALIYOYASEMA HAJI MWINYI KUHUSIANA NA MECHI YAO NA SIMBA

Wakati zikiwa zimesalia siku mbili pekee kutoka leo kabla ya mechi ya Yanga dhidi ya Simba, beki wa kushoto wa Wanajangwani, Haji Mwinyi, amesema kuwa kwa uzoefu alionao wa mechi za kimataifa mpaka sasa, kamwe hawezi kuwa na presha na Simba aliyoiita ni nyepesi zaidi msimu huu. Mwinyi ameeleza zaidi kuwa, kutokana na mechi ngumu walizocheza kwenye michuano ya kimataifa ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf) na kukutana na timu vigogo Afrika kama Al Ahly ya Misri, hawezi kuhofia Simba inayoongozwa na wachezaji kama Ibrahim Ajibu, Laudit Mavugo na Shiza Kichuya. “Nani? Hao kina Ajibu ndiyo watutishe sisi, wakati tushacheza mechi nyingi kubwa kuliko hiyo ya Simba, tumekutana na watu wapo vizuri huko kwenye mechi za kimataifa, mtu unacheza mpaka na mastraika wa Al Ahly halafu leo uhofie hawa wa Simba? “Huo mchezo utakuwa na hadhi na presha yake kwa kuwa ni mchezo wa watani wa jadi, lakini tofauti na hapo, Simba yenyewe naona ni ya kawaida tu msimu huu tofauti na kipindi kile kuna akina Kessy (Hassan),” alisema Mwinyi na kuongeza: “Unajua watu wasipate shida na kuona Simba imeifunga Majimaji mabao 4-0. Sisi tulipocheza na Majimaji tuliwafunga 3-0 pale Uhuru, sasa tungecheza nao Uwanja wa Taifa kama walivyocheza Simba, tungewafunga hata sita wale (Majimaji), watu wasiwe na presha, watulie.” Yanga na Simba zinatarajia kukutana katika mechi ya kwanza msimu huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, Jumamosi hii huku kukiwa na kumbukumbu ya Simba kufungwa nje ndani katika mechi mbili za msimu uliopita. Kila mechi walifungwa mabao 2-0. SOURCE: CHAMPIONI

KUEREKEA OKTOBA 1 KASI YA SIMBA YASUKUMA PRESHA KAMBI YA YANGA PEMBA

Kasi ya ushindi kwenye mechi za Ligi Kuu Bara wanayoendelea nayo Simba, imezua hofu kwenye kambi ya Yanga waliyoweka huko Pemba kujiandaa na mchezo wa watani wa jadi utakaopigwa Jumamosi wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga iliingia kambini huko Pemba juzi Jumatatu mchana wakitokea Shinyanga kuvaana na Stand United, katika mechi ya Ligi Kuu Bara ambayo ilimalizika kwa kufungwa bao 1-0. Simba hadi hivi sasa imecheza michezo sita ikishinda mitano huku mmoja wakitoka suluhu na JKT Ruvu wakati Yanga yenyewe imecheza mitano ikishinda mitatu, ikitoa suluhu na Ndanda FC huku ikifungwa mmoja na Stand United. Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano kutoka ndani ya kambi hiyo, hofu kubwa imetanda ya kupoteza mechi hiyo kutokana na mwenendo mzuri wa matokeo wanayoendelea kuyapata Simba. Mtoa taarifa huyo alisema, presha imeongezeka zaidi mara baada ya kipigo walichokipata dhidi ya Stand United hali inayosababisha kuzuka hofu kubwa ya kufungwa katika mchezo huo. "Tupo kambini Pemba, lakini presha imeongezeka kwa kiwango kikubwa kutokana na matokeo mazuri ya ushindi wanayoendelea kuyapata watani wetu Simba. "Kiukweli kabisa, wachezaji wetu wanahitaji somo la saikolojia ili kurejesha morali ya timu iliyopotea baada ya kufungwa na Stand, tunajua siyo kazi rahisi lakini tutahakikisha tunafanikisha hilo. "Uongozi umepanga kukutana na wachezaji siku moja kabla ya mechi kwa ajili ya kuzungumza nao na kikubwa kutuliza presha ya mechi hiyo ili tushinde na hilo linawezekana kutokana na ubora wa kikosi chetu,"alisema mtoa taarifa huyo. Alipotafutwa Kocha Mkuu wa timu hiyo Mholanzi, Hans van Der Pluijm kuzungumzia hali hiyo, alisema kuwa: "Siku zote zinapokaribia mechi za watani wa jadi presha inakuwa kubwa kwenye timu kwa kuanzia viongozi, kocha hadi wachezaji, lakini nikwambie kitu tu, wao wenyewe wanatuogopa sisi.”

Jumanne, 27 Septemba 2016

KOCHA MPYA WA ENGLAND KWA MUDA BAADA YA BIG SAM KUBWAGA MANYANGA, HUYU HAPA AKIWA NA SALEHJEMBE

Aliyekuwa kocha msaidizi wa timu ya taiga ya England, Gareth Southgate ndiye anachukua jukumu la kuinoa timu hiyo. Southgate, anachukua nafasi huyo baada ya Sam Allardyce kuamua kuachia ngazi katakana na kashfa iliyomkumba. Allardyce maarufu kama Big Sam amedumu kwa sikh 61 baada ya kupata mkataba mnono wa kuinoa England.  Kocha huyo mwenye umri wa miaka 61, ameingia kwenye mtego na kurekodiwa akipiga dili ya upindishaji wa sheria za FA. Southgate ambaye aliwahi kufanya mahojiano na Salehjembe, wakati akiwa kocha wa Middelesbrough, ataanza kuiongoza England katika mechi yake dhidi ya Malta Oktoba 8.  Imeelezwa kocha huyo ataingoza England kwa mechi nne kabla ya uamuzi wa suala la kocha mpya kupitishwa.



BIG SAM ALIKOROGA, AINGIA MTEGO WA TAMAA, ALAZIMIKA KUACHIA NGAZI ENGLAND

Kocha Sam Allardyce ameachia ngazi ya kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya England. Allardyce maarufu kama Big Sam amedumu kwa siku 67 baada ya kupata mkataba mnono wa kuinoa England ambao thamani yake ulikuwa pauni milioni 3. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 61, ameingia kwenye mtego na kurekodiwa akipiga dili ya upindishaji wa sheria za FA. Katika dili hiyo, Big Sam angefanikiwa kupata pauni 400,000 lakini alitegewa kamera ambayo picha zake zilisambazwa akijiachia, jambo ambalo limemfanya mwenye akubali kuachia ngazi.

MATOKEO UEFA CHAMPIONS LEAGUE DORTMUND YAILAZIMISHA MADRID SARE YA BAO 2-2 LIGI YA MABINGWA ULAYA

Mechi ya Real Madrid dhidi ya wenyeji Borussia Dortmund imeisha kwa sare ya mabao 2-2. Mechi hiyo ilikuwa kali baada ya wenyeji kulazimika kusawazisha mara mbili dhidi ya mabingwa hao wa Ulaya. Cristiano Ronaldo ndiye alianza kufunga kwa upande wa Madrid, PierreAubameyang akasawazisha dakika ya 43. Kipindi cha pili Raphael Varane akaifungia Madrid tena dakika ya 68 lakini ‘jioni’ kabisa katika dakika ya 87, Andre Schuerrle akaifungia Dortmund bao la kusawazisha.