pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumapili, 1 Januari 2017
WEWE BISHA LOLOTE KUHUSIANA NA SCORPION KICK ZA MKHITARYAN NA GIROUD, LAKINI HUU NDIYO UKWELI Siku sita zilizopita, kiungo Henrikh Mkhitaryan wa Man United alifunga bao safi wakati timu yake ikivaa Sunderland. Bao hilo lilikuwa gumzo na kupewa jina la Scorpion Kick. Lakini siku sita baadaye unaweza kusema amepata jibu. Olvier Giroud wa Arsenal naye amefunga bao linalofanana na hilo katika mechi dhidi ya Crystal Palace ambayo Arsenal imeibuka na ushindi wa mabao 2-0. Sasa ni gumzo, kwamba bao hilo la Mhkitaryan raia wa Armenia na lile la Giroud kutoka Ufaransa. Lipi kali hasa? Kila mmoja anaweza kuwa huru kupitia maoni yake pamoja na ushabiki. Lakini ukweli ni hivi; bao la Mkhitaryan lilikuwa bora la funga mwaka 2016 na lile la Giroud limekuwa bora la fungua mwaka 2017.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni