Jumapili, 1 Januari 2017

VIGOGO HAWA NDIYO KIKWAZO CHA CHELSEA KUBEBA UBINGWA ENGLAND, IKIWEZA, BASI MAMBO KWA ULAINIIII Chelsea iko kileleni mwa Ligi Kuu England kwa tofauti ya pointi dhidi ya Liverpool wanaoshika nafasi ya pili. Lakini hiyo bado si sababu ya kuamini tayari wao wana nafasi ya kuwa mabingwa na hasa kama utazungumzia mechi za vigogo sita. Vigogo sita wa Premier League ni Manchester United, Liverpool, Arsenal, Chelsea, Manchester City na Tottenham. Hakuna ubishi hizi ndiyo timu sita zinazowania ubingwa na lazima bingwa atatoka miongoni mwao. Kama utaangalia mechi tano kwa kila timu baada ya kukutana na kigogo mmoja mara moja, Liverpool ndiyo haikupoteza dhidi ya kigogo yoyote. Lakini Chelsea ilipoteza mechi mbili, moja ikichapwa mabao 4-0 na Arsenal. Man City ilipoteza mechi tatu na zilizobaki zote zilipoteza mechi mbili. Katika mechi tano dhidi ya vigogo wenzake, kama utatengeneza msimamo wa vigogo tu, Liverpool ndiyo inaongoza kwa kukusanya pointi 11 katika mechi hizo tano ikifuatiwa na Chelsea yenye pointi 9. Man Cityi imekusanya 6 huku Arsenal, Spurs na Man United kila mmoja imekusanya pointi 5 ikiwa ni wastani wa pointi moja kwa kila mechi sawa na sare 5. Hii inaonyesha bado kuna ugumu wa juu kwa Chelsea na analazimika kufanya vema katika mechi 5 dhidi ya vigogo wenzake ili kujihakikishia ubingwa. MECHI ZIJAZO ZA VIGOGO SITA: Jan 4: Tottenham v Chelsea Jan 15: Man United v Liverpool Jan 21: Man City v Tottenham Jan 31: Liverpool v Chelsea Feb 4: Chelsea v Arsenal Feb 11: Liverpool v Tottenham Feb 26: Man City v Man United Mar 4: Liverpool v Arsenal Mar 18: Man City v Liverpool Apr 1: Arsenal v Man City Apr 5: Chelsea v Man City Apr 15: Man United v Chelsea Apr 29: Tottenham v Arsenal May 6: Arsenal v Man United May 13: Tottenham v Man United

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni