pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumanne, 31 Januari 2017
BAADA YEYE NA KLOPP "KUSHINDWANA", SAKHO SASA ANUKIA CRYSTAL PALACE Klabu ya Crystal Palace imeonyesha nia ya kumpata beki Mamadou Sakho. Liverpool intake kulipwa pauni milioni 20 ili kumuachia beki huyo raia wa Ufaransa. Sakho na Kocha Jurgen Kloop aria wa Ujerumani wanaonekana kutoelewana kabisa. Wakati dirisha la usajili linakwenda ukingoni , inaonekana juhudi zinafanyika.
BAADA YA SIMBA KUITOLEA NJE, MAMELODI SASA KUIVAA AZAM ALHAMISI Baada ya kikosi cha Simba kutoa nje kucheza na Mamelodi, ssa timu hiyo itashuka dimbani Alhamisi, kuivaa Azam FC. Taarifa zinasema, Mamelodi wataendelea na maandalizi kwa ajili ya mechi dhidi ya Azam FC hiyo Alhamisi, mechi inayotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Awali, Mabingwa hao wa Afrika walitakiwa kucheza kesho dhidi ya Simba, lakini klabu hiyo imeona ina majukumu ya maandalizi dhidi ya Majimaji mjini Songea, wikiendi hii. Lakini pia kumekuwa na taarifa kwamba waandaaji wa mechi hiyo hawakuwa na maandalizi mazuri kati yao na uongozi wa Simba kuhusiana na mechi hiyo. Hata hivyo, mmoja wa waandaaji amesema, Simba walikuwa na taarifa za kutosha lakini wamegeuka huenda inatokana na wao kupoteza mechi dhidi ya Azam FC Jumamosi na Yanga ikaishinda Mwadui FC na kukwea kileleni.
Jumatatu, 30 Januari 2017
MAMELODI SUNDOWNS FC WATUA DAR KUZIFUATA SIMBA, AZAM Msafara wa kikosi cha Mamelodi Sundowns FC ya Afrika Kusini umewasili leo Jumatatu mchana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuweka kambi kwa muda kisha kucheza mechi mbili za kirafiki. Mamelodi wamewasili Dar es Salaam wakiwa na jumlaya watu 42 huku ikielezwa kuwa wengine 10 wanatarajiwa kuingia kesho Jumanne. Ikiwa Dar es Salaam, Mamelod inatarajiwa kucheza mechi za kirafiki dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa kisha dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa Azam Complex wiki hii kabla ya kuondoka Jumamosi ijayo.
DIMITRI PAYET JEURI SANA, AKAMILISHA DILI LA UHAMISHO, AWATOLEA KAULI WEST HAM Dimitri Payet ametangazwa rasmi kuwa mchezaji wa Marseille ya Ufaransa akitokea West Ham United ya England kwa ada ya pauni 25m lakini kuna neno ametoa kuhusu timu yake ya zamani. Payet ambaye alitolewa lugha nyingi kali na mashabiki wa West Ham walimuona kama msaliti kwa kugoma kucheza akitaka auzwe amesaini mkataba wa miaka minne na nusu na klabu yake hiyo ya nyumbani na kuamua kuzungumzia kilichotokea. Akizungumzia kuhusu tabia yake iliyojitokea mpaka dili hilo linakamilika, Payet amesema: "Sina haja ya kuthibitisha au kufafanua kuhusu tabia yangu. Slaven Bilic (kocha wa West Ham) tulizungumza na tunajua kilichotokea. “Sina cha ziada kuzungumzia kuhusu suala hilo, naona bora nitahifadhi hayo, nitayazungumza siku nyingine lakini siyo sasa, kwa ufupi nilihitaji sana kurejea Ufaransa hasa Marseille."
Watoto wa baba mmoja wameipeleka Ghana nusu fainali AFCON 2017 Watoto wa baba mmoja Jordan Ayew na Andre Ayew kila mmoja alifunga goli kuichapa DR Congo 2-1 na kuihakikishia Ghana kucheza nusu fainali ya kombe la mataifa ya Afrika. Jordan Ayew ambaye ni mshambuliaji wa Aston Villa alizifungua nyavu za DR Congo dakika ya 62 kwa kuuzungusha mpira ambao ulijaa moja kwa moja kwenye nyavu za goli la the Leopards. Paul-Jose M’Poku akaisawazishia DR Congo kwa mkwaju mkali akiwa nje ya box. Mshambuliaji wa West Ham Andre Ayew akafunga goli la ushindi kwa the Black Stars kwa mkwaju wa penati na kuifanya Ghana ifuzu moja kwa moja kucheza nusu fainali ya AFCON 2017. Ghana imefuzu kwa mara ya sita mfululizo kucheza nusu fainali ya michuano ya AFCON huku wakitafuta kumaliza ukame wa taji hilo walilolitwaa mara ya mwisho miaka 35 iliyopita.
Jumamosi, 28 Januari 2017
Azam wameihuzunisha tena Simba baada ya siku 15 Azam FC wamerudia kile walichokifanya Zanzibar kwenye fainali ya Mapinduzi Cup kwa kuitungua tena Simba kwa bao 1-0 kwenye mechi ya ligi kuu Tanzania bara iliyochezwa kwenye uwanja wa taifa. Goli pekee lililoipa Azam ushindi na pointi tatu limefungwa na nahodha John Bocco ‘Adebayor’ dakika ya 69 kipindi cha pili na kuimaliza Simba. Ushindi kwa Azam unamaanisha Simba inaendelea kubaki na pointi 45 baada ya kucheza mechi 20 ikiwa mbele ya Yanga kwa pointi mbili pekee lakini ‘wakimataifa’ wanamchezo mmoja mkononi. Endapo Yanga watapata ushindi kwenye mchezo wao wa kesho dhidi ya Mwadui FC wataiondoa Simba kileleni kwani watafikisha pointi 47, lakini kama watapata sare ya aina yoyote watafikisha pointi 45 na kuwa sawa na Simba lakini bado Yanga wataongoza ligi kwa uwiano wa magoli. Hadi sasa Yanga wana wastani wa magoli 31 wakati Simba wao wana wastani wa magoli 24. Hiki ni kipigo cha pili mfululizo kwa Simba kutoka kwa Azam ikiwa ni siku 15 zimepita baada ya timu hizo kukutana kwenye mchezo wa fainali ya Mapinduzin Cup ambayo ilichezwa January 13, 2017. Kikosi cha Simba Daniel Agyei, Javier Bokungu, Mohamed Hussein, Abdi Banda, Method Mwanjale, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Pastory Athanas, Said Ndemla, Jamal Mnyate na Juma Liuzio. Kwenye benchi Peter Manyika, Vicent Costa, Novalty Lufunga, Laudit Mavugo, James Kotei, Ibrahim Ajib, Shiza Kichuya Kikosi cha Azam Aishi Manula, Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Yakub Mohamed, Himid Mao, Stephen Kingue,Frank Domayo, Ramadhan Singano, Joseph Mahundi na John Bocco Kwenye benchi Metacha Mnata, David Mwantika, Abdallah Kheri, Shabani Idd, Masoud Abdala, Mudathir Yahaya na Yahaya Mohammed.
PRISONS "WAITUMBUA" MBEYA CITY SOKOINE, MECHI YA NANGWANDA YASOGEZWA MBELE Prisons imeendeleza ubabe wake kwa Mbeya City baada ya kuitwanga kwa bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, leo. Prisons ilionyesha soka safi tokea mwanzo, lakini Mbeya City wakafanya mashambulizi mengi ingawa kipa wa Prisons akawa kipingamizi kikubwa kwao kupata bao. Wakati Prisons wakiitwanga Mbeya City, upande mwingine mechi iliyokuwa ipigwe Nangwanda Sijaona mjini Mtwara kati ya wenyeji Ndanda FC na Majimaji Majimaji ambao ni majirani wa Ndanda, walichelewa kufika mjini Mtwara na sasa mechi hiyo itapigwa kesho.
SERENA NA VENUS, HATA BAADA YA FAINALI UNDUGU NDIYO UNACHUKUA SURA ZAIDI Serena Williams alimshinda dada yake Venus Williams na kubeba taji la Australian Open. Ushindi huo dhidi ya Venus ambaye ni dada yake inakuwa ni Grand Slam ya 23 kwake. Serena alishinda kwa seti mvili moja kwa moja yaani 6-4, 6-4 lakini kivutio zaidi ni dada hao walivyokuwa baada ya mechi. Kumbuka makombe ya bingwa na mshindi wa pili yanakwenda kwenye familia moja. Wawili hao walioanza tenisi kocha akiwa baba yao mzazi, walionekana ni wenye furaha, waliokuwa wakitaniana na hakuna aliyeonekana kuwa na masikitiko au furaha zaidi ya mwenzake. Baada ya fainali, mambo yalivyokuwa ni kama hakukuwa na chochote kilichopita na kila mmoja alionekana ameridhika kabisa.
LIVE KUTOKA UWANJA WA TAIFA: SIMBA 0 VS 1 AZAM FC (KIPINDI CHA PILI) Kipa Manula yuko chini pale akitibiwa DAKIKA 4 ZA NYONGEZA Dk 90, Simba wanafanya shambulizi hapa, Mavugo anatwanga kichwa lakini Manula anaokoa na kuwa kona hapa, sasa Azam FC wako nyuma wote Dk 88, Simba wanapoteza nafasi nzuri kabisa, mpira wa adhabu wa Kichuya, Mavugo yeye na lango anapaisha hapa Dk 85, Azam FC wanaonekana kuzidi kuimaisha ulinzi kwa kuwa wachezaji sita sasa wanabaki nyuma kufanya ulinzi SUB Dk 83, Abdallah Kheri, kinda matata huyu anaingia kuchukua nafasi ya Bocco ambaye ameshindwa kurejea baada ya kuumia KADI Dk 82 Mwamuzi Onoka wa Arusha anamlamba kadi ya njano Aishi Manula kwa kupoteza muda Dk 80, Bocco yuko chini hapa akiwa ameshika paja lake Dk 78, Zimbwe anapokea pasi na Mavugo, anawatambuka mabeki wa Azam na kuachia mkwaju lakini hakulenga lango SUB Dk 76, Simba wanamuingiza Mudathir kuchukua nafasi ya Kingue ambaye ameumia Dk 73, Stephan KIngue wa Azam yuko chini anatibiwa hapa, anatolewa nje na huenda
LIVE KUTOKA UWANJA WA TAIFA: SIMBA 0 VS 1 AZAM FC (KIPINDI CHA PILI) GOOOOOOOOOOO Dk 70, Bocco anamtambuka MWanjale na kuachia mkwaju mkali wa chinichini na kuandika bao kwa Azam FC Dk 68, Simba wanafanya shambulizi tena, krosi nzuri, Ajib yeye na lango anashindwa kupiga kichwa kulenga. GAoal kick Dk 68, Yahaha anaingoia vizuri hapa lakini hata spidi hapa, mpira unawahiwa na Agyei Dk 67, Simba wanafanya shambulizi kali hapa lakini shuti la Kichuya linatoka na kuwa goal kick Dk 66, Kichuya anageuka na kuachia mkwaju hapa lakini Manula anaudaka vizuri hapa
LIVE KUTOKA UWANJA WA TAIFA: SIMBA 0 VS 0 AZAM FC (KIPINDI CHA PILI) SUB Dk 62, Yahaya Mohammed anaingia kwa upande wa Azam FC kuchukua nafasi ya Singano Dk 60, Ajibu anapata pasi nyingine nzuri, lakini mwenyewe anaupoteza tena mpira huo SUB Dk 59, Simba wanamtoa Boukungu na nafasi yake inachukuliwa na Ibrahim Ajibu ambaye mpira wa kwanza tu, anapoteza hapa DK 58, Zimbwe wa Simba yuko chini hapa anatibiwa na Himid Mao ambaye tayari ana kadi ya njano Dk 54, mechi imesimama kwa dakika moja baada ya Bocco kumtwanga teke Boukungu wakati akiachia shuti kwa lengo la kufunga. Inaonekana ilikuwa ni bahati mbaya Dk 51, mpira unaonekana kuchangamka sasa, timu zinaanza kufunguka na kucheza mipira mirefu na kufanya mashambulizi Dk 48, Simba wanafanya shambulizi kali, Liuzio anaachia mkwaju mkali hapa, Manula anauficha SUB Dk 46, Simba inafanya mabadiliko ya kwanza, Shiza Kichuya anaingia kuchukua nafasi ya Jamal Simba Mnyate
LIVE KUTOKA UWANJA WA TAIFA: SIMBA 0 VS AZAM FC 0 (MAPUMZIKO) MAPUMZIKODAKIKA 2 ZA NYONGEZA Dk 45, Bokungu anapiga krosi maridadi hapa ya outer lakini Aishi anadaka vizuri kabisa Dk 44, Manula anafanya kazi nzuri kwa kutokea na kuudaka mpira wa krosi kabla haujamfikia Athanas KADI Dk 43, Singano naye analambwa kadi ya njano kwa kucheza faulo dhidi ya Banda Dk 41, Athanas anamgeuza Yakubu ndani ya boksi, anaachia mkwaju unagonga mwamba kwa juu na kuwa goal kick Dk 39, Simba wanaingia eneo la hatari la Azam, Muzamiru anaachia shuti lakini linakuwa nyanya hapa kwa Manula
LIVE KUTOKA UWANJA WA TAIFA: SIMBA 0 VS AZAM FC 0 Dk 36 sasa, bado si mechi ya kuvutia sana kama ambavyo ilikuwa imetarajiwa KADI Dk 33, Erasto Nyoni analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Pastory Athanas, hii ni kadi ya kwanza ya njano ya mchezo huu Dk 30, hakuna timu iliyogusa nyavu na mpira unaendelea kuchezwa katikati zaidi ya uwanja na tahadhari kubwa yenye uoga ikiendelea kuchukua nafasi Dk 23, Yakubu anautoa mpira nje na kuwa kona ya kwanza ya mchezo ambao wanaipata Simba. Inachongwa hapa Azam FC wanaokoa DK 20 sasa, kila timu iko makini sana. Maana walinzi ni wanne kwa kila upande na kila timu inaposhambuliwa inakuwa na walinzi zaidi ya watano Dk 15, Mahundi anapoteza nafasi nzuri ya kwanza baada ya kuupata mpira kwenye boksi la Simba mabeki wakiwa wamezubaa, anapiga shuti la chini, mpira unampita Agyei na kuwa goal kick Dk 13, Bocco anajaribu hapa katika lango la Simba lakini Agyei anakuwa makini na kuudaka mpira huo Dk 9, Bukungu anaachia shuti kali lakini linatoka nje. Kinachoonekana timu hizi kila mmoja imejaza watu wengi zaidi nyuma, hivyo kufanya kusiwe na ladha ya juu ya ushambulizi Dk 6 sasa, hakuna shambulizi hata moja kali. Zimbwe wa Simba anatolewa nje baada ya kugongana na Mhundi, anapatiwa matibabu Dk 2, Azam FC wanakuwa wa kwanza kufika lango la Simba lakini shuti la Mahundi, linadakwa kwa ulaini na kipa Agyei Dk 1, mechi imeanza taratibu kabisa huku kila timu ikionekana inataka kuusoma mpira au mbinu za mwenzake kabla ya kuzipambanua zake HEAD TO HEAD SIMBA VS AZAM FC Kutana mara 17 Simba shinda mara 8 Azam Mara 4 Sare 5
NYUMA YA PAZIA : Coutinho katika ile biashara ya nipe nikupe Alikuwa ametoka katika kasheshe la kutakiwa na Arsenal. Miezi saba baada ya kusaini mkataba mpya, Julai Mosi 2014, Luis Suarez alikuwa akisaini mkataba mpya wa miaka mitano na Barcelona. Alikabidhiwa jezi namba 9 na kuwa mmoja kati ya wachezaji ghali dunia. Maisha yana haraka zake siku hizi. DESEMBA 20, 2013 siku tano kabla dunia haijasherehekea Sikukuu ya Krismasi 2013, au unaweza kusema miaka 14 baada ya Wareno kuwakabidhi Wachina Kisiwa cha Macau walichokuwa wanakikalia, Luis Suarez alikuwa akigonga mlango wa Ofisi za Liverpool Melwood kusaini mkataba mpya wa miaka minne Anfield. Alikuwa ametoka katika kasheshe la kutakiwa na Arsenal. Miezi saba baada ya kusaini mkataba mpya, Julai Mosi 2014, Luis Suarez alikuwa akisaini mkataba mpya wa miaka mitano na Barcelona. Alikabidhiwa jezi namba 9 na kuwa mmoja kati ya wachezaji ghali dunia. Maisha yana haraka zake siku hizi. Juni 2006, siku chache baada ya Arsenal kufungwa mabao 2-1 na Barcelona katika pambano la fainali Ligi ya Mabingwa wa Ulaya pale Paris, Thierry Henry alikuwa akisaini mkataba mpya na Arsenal ambao ungemwweka klabuni hapo kwa miaka mitano zaidi. Miezi 12 baadaye, alikuwa akisaini mkataba wa miaka minne na Barcelona katika dili la Euro 24 milioni. Alipewa jezi yake ile ile namba 14 aliyokuwa anatumia Arsenal. Jezi ambayo aliitendea haki kuanzia Highbury mpaka Emirates. Novemba 2008, Cristiano Ronaldo alikuwa akisaini mkataba mpya na Bosi Mtendaji wa Manchester United, David Gill. Julai 2009, miezi tisa baadaye, alikuwa akisaini mkataba wa miaka mitano kuichezea Real Madrid huku akivunja rekodi ya uhamisho wa dunia. Mifano ya namna hii ipo mingi. Ni maisha ya kawaida kwa wanasoka wa kisasa na klabu za kisasa. Usishangilie sana unaposikia mchezaji wako mahiri amesaini mkataba mpya klabuni. Hauna maana yoyote kwa siku hizi. Wakati mwingine ni maandalizi ya biashara nzuri ya miezi michache ijayo. Kwa mfano, Philippe Coutinho amesaini mkataba mpya Anfield Jumatatu wiki hii. Kama shabiki wa Liverpool unaweza kuachia meno nje. Katika soka la kisasa, kwa sisi tunaofahamu vyema, mkataba huo mpya hauna maana kubwa sana kumzuia Coutinho asiondoke Anfield. Klabu huwa zinatengeneza dili na mchezaji ambaye anatakiwa na ni muhimu sana klabuni. Mkataba mpya unazinufaisha pande zote mbili. Unamnufaisha Coutinho na unamnufaisha mwajiri wake Liverpool. Huwa inatumika akili rahisi tu. Kwa upande wa Coutinho ni kwamba mshahara wake utaongezeka maradufu mpaka siku ambayo ataondoka. Mkataba huu unamaanisha kwamba kwa sasa atapata pesa nyingi zaidi kwa sababu anastahili na anafurahia soka lake Anfield. Kwa upande wa Liverpool ni kwamba mkataba huu unawaweka katika nafasi nzuri zaidi ya kumuuza Coutinho kwa pesa nyingi kuliko ambavyo wangemuuza katika dirisha hili au mwishoni mwa msimu. Moja kati ya thamani kubwa ya mchezaji ni kuwa na mkataba wa muda mrefu. Hili ndilo ambalo haswa wamelitafuta Liverpool. Hawana uhakika sana na maisha ya Coutinho pale Anfield. Wachezaji wakubwa wa uwezo wake wakiamua kulazimisha kuhama inakuwa vigumu kuwabakiza. Kwa kumpa mkataba mrefu unakuwa katika nafasi nzuri ya kumuuza kwa bei unayotaka. Kinachofanyika kwa sasa ni nipe nikupe. Coutinho amewapa Liverpool nafasi nzuri katika maongezi kama akihitajika na watu wanaojifanya wana pesa na yeye wamempa mshahara mkubwa ambao ataufahidi mpaka hapo litakapokuja dili la klabu inayomtaka. Haya ndio maisha ya kisasa.
Homa ya Sadio Mane Liverpool si kitu kabisa inapocheza bila huduma ya staa huyo wa Senegal. Kukosekana kwa Mane klabuni Liverpool ni majanga makubwa, homa kali. HOMA ya maradhi mpya imeibuka huko Anfield inayoitwa ‘Ukosefu wa Mane!’ Mane? Ndiyo, ni yule staa wao Liverpool na timu ya taifa ya Senegal, Sadio Mane. Liverpool si kitu kabisa inapocheza bila huduma ya staa huyo wa Senegal. Kukosekana kwa Mane klabuni Liverpool ni majanga makubwa, homa kali. Ukitaka kujua hilo, tazama takwimu hizi. Liverpool kwa sasa inakosa huduma ya mchezaji huyo, ambaye amerudi Afrika kucheza michuano ya Afcon 2017 huko Gabon. Na tangu akosekane, imekuwa ni kupatwa kwa Liverpool. Wametupwa nje kwenye Kombe la Ligi na wakifungwa pia nyumbani Anfield na vimeo, Swansea City. Ipo hivi, kabla ya Mane kwenda Afcon, akiichezea Liverpool timu hiyo imeshinda mechi 17 kati ya 24 ilizocheza, lakini tangu aondoke, kwenye mechi sita ilizocheza Liverpool wameshinda moja tu. Kipindi ambacho Mane yupo, Liverpool ilikuwa na uhakika wa kushinda mechi zake kwa asilimia 71, lakini baada ya kuondoka, hali imeshuka na kuwa asilimia 17 tu. Wakati Mane akiwa kwenye kikosi, Liverpool ina uhakika wa kufunga mabao zaidi ya mawili, lakini bila ya huduma yake, wastani unaonyesha ni bao moja tu. Mane ametupia wavuni asilimia 33 ya nafasi zote alizopata kwenye Ligi Kuu England msimu huu, wakati fowadi mwingine Roberto Firmino ana asilimia 16 tu ya kutumbukiza wavuni nafasi alizopata kwenye ligi hiyo msimu huu. Hii ina maana Liverpool inakuwa hatari sana kwenye fowadi yake inapokuwa na huduma ya Mane.
Huyu Diego Costa ameshindikana, eti kaibuka na staili mpya ya kufunga! Viungo vitatu vinavyotumika mara nyingi kufunga. Lakini, hivi karibuni alionyesha kali huko mazoezini Chelsea. Alifunga bao kwa makalio. Ndiyo kwa makalio! DIEGO Costa kwenye Ligi Kuu England msimu huu amefunga mabao ya staili zote. Amefunga kwa mguu wa kushoto, amefunga kwa mguu wa kulia na amefunga pia kwa kichwa. Viungo vitatu vinavyotumika mara nyingi kufunga. Lakini, hivi karibuni alionyesha kali huko mazoezini Chelsea. Alifunga bao kwa makalio. Ndiyo kwa makalio! Tena magoli yale madogo madogo wanayofanyia mazoezi. Wakiwa mazoezi huko kwenye uwanja wao wa Cobham, straika Costa alipokea pasi kutoka kwa Nemanja Matic na wakati akikimbiliwa na beki Gary Cahill akamkabe, fowadi huyo aliutuliza mpira, kisha akauweka sawa kabla ya kuamua kufunga kwa makalio na kuwaacha wenzake wakimshamngaa tu. Chelsea iliamua kuiweka video ya bao hilo kwenye ukurasa wao wa Facebook jambo ambalo linatafsiriwa kwamba, huenda ni mkwara tu kwa wapinzani wao kwenye mbio za ubingwa kuwa Costa anafunga tu mabao kwa namna anavyojisikia. Kwenye ligi staa huyo kwa sasa amefunga mabao 15 akiwa amefungana kileleni na Alexis Sanchez wa Arsenal mwenye idadi kama hiyo ya mabao. Costa baada ya kuripotiwa kutibuana na benchi la ufundi, aliporudi uwanjani kwenye mechi dhidi ya Hull City alitikisa wavu wakati Chelsea ilipoibuka na ushindi na kuweka pengo la pointi nane kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu England. Kiungo N’Golo Kante alikoshwa sana na bao hilo la Costa alilofunga mazoezini.
Tutawaonyesha tofauti ya bonanza Lakini Simba wakajibu kwamba kelele zote za Azam zitaishia Taifa na wanataka kuwathibitishia kwamba kuna tofauti kati ya ligi kuu na Kombe la Mapinduzi huku kiongozi mmoja akikejeli kuwa lilikuwa ni kama bonanza ndio maana hawakulitolea macho sana. SIMBA na Azam ziko Uwanja wa Taifa leo Jumamosi. Sasa sikia. Azam wamewaambia Simba kwamba watawapiga mabao matatu safi tena mapema kabisa. Lakini Simba wakajibu kwamba kelele zote za Azam zitaishia Taifa na wanataka kuwathibitishia kwamba kuna tofauti kati ya ligi kuu na Kombe la Mapinduzi huku kiongozi mmoja akikejeli kuwa lilikuwa ni kama bonanza ndio maana hawakulitolea macho sana. Lakini kituko kinachoweza kutokea leo uwanjani ni mashabiki wa Yanga kuishangilia Azam, ili iifunge Simba. Ikumbukwe Azam ilimchapa Yanga mabao 4-0 kwenye Mapinduzi na kuwafanya Jangwani wapachikwe jina la 4G. Mchezo wa Simba na Azam umeibua hisia za wengi na kutabiriwa kuwa na ushindani wa nguvu kutokana na historia ya vikosi hivyo. Mapema mwaka huu Simba walichapwa 1-0 mechi ya fainali ya Kombe la Mapinduzi wakakosa taji. Simba ambayo itawakosa, Mkongo Besala Bokungu, atakuwa jukwaani kwa kuwa ana kadi tatu za njano na Mohammed Ibrahim ‘Mo’ ambaye ana maumivu ya kifundo cha mguu, inajifua kwa hasira kuhakikisha wanalipiza kisasi. Kocha wao Mcameroon Joseph Omog ameahidi kutorudia makosa na ametamba kuwafunga Azam timu aliyoifundisha miaka ya nyuma na kuipa taji la ligi kuu msimu wa 2013-2014. Omog alisema: “Mechi itakuwa ngumu, itakuwa tofauti na ya Zanzibar kwani sasa nawajua vizuri wapinzani wangu tofauti na ilivyokuwa awali.” “Azam nimewaangalia kwa umakini ni wazuri hasa kwenye ulinzi walipo, Aggrey Morris, Shomari Kapombe, Gadiel Michael na yule Mcameroon (Stephan Kingue) ingawa katika ushambuliaji wachezaji John Bocco ‘Adebayor’ na Mohammed Yahya si wa kuwapuuzia ,” alisema Omog na kufafanua nafasi ya Bokungu na Mo itazibwa na wengine aliowaandaa. Kwa upande wa Azam iliyotamba kuwapiga 4GB wakiwa na maana 3-0, Kocha Msaidizi, Idd Cheche alisema: “Tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunaifunga Simba. Mechi itakuwa ngumu na tutaingia na mbinu mpya ili kufanikisha yetu.” Simba na Azam zimeshakutana mara 24, Simba wanatesa kwa kuifunga Azam mechi za ligi na Lambalamba wakisumbua kwenye mashindano mengine. Kwenye Ligi Kuu Bara wamekutana mara 17 Simba wameshinda mara nane, Azam walishinda nne wakati sare ni tano. Wamekutana mara moja kwenye mechi ya Ngao ya Jamii na Simba ndiyo alishinda mabao 3-2. Timu hizo zilikutana kwenye Kombe la Mapinduzi mara tatu, Azam alishinda mbili 2-0 mwaka 2011 na 1-0 mwaka 2017 na moja walitoa sare ya 2-2 mwaka 2012. Walikutana kwenye Kombe la Kagame mechi ya robo fainali, Azam alishinda 3-1, kombe la ujirani mwema mara moja wakamaliza kwa sare na Super 8 mara moja Simba ilishinda 2-1 mechi ya nusu fainali.
Ijumaa, 27 Januari 2017
Borussia Dortmund na ukuta wa Donald Trump Donald Trump ameingia madarakani rasmi,tayari Trump ameanza kutengeneza vichwa vya habari.Na jambo kubwa linalozungumzwa hivi sasa ni ujenzi wa ukuta mkubwa ambao utaitenganisha nchi ya Marekani pamoja na ile ya Mexico. Trump anaamini katika ukuta huo,ukuta huo wenye kilomita zaidi ya 3100.Trump anaamini ujenzi wa ukuta huo utapunguza baadhi ya mambo maovu nchini mwake.Mexico ni kati ya nchi zinazoongoza kwa biasharabya madawa ya kulevya na Trump anauona ukuta huo utapunguza uingizaji haramu wa dawa za kulevya na pia wahamiaji haramu toka Mexico. Obama anaamini katika ukuta huo,lakini ni tofauti kwa Borussia Dortmund.Borussia Dortmund wanaamini katika ukuta mmoja tu dunia mzima nao ni ule UKUTA WA NJANO(YELLOW WALL).Ukuta huu una zaidi ya mashabiki 25,000 na kila siku ya mechi huvalia jezi zao za njano na kuishangilia timu yao.Kupitia ukurasa wao wa twittet Borussia Dortmund wamemjibu Trump kwa kuonesha kwba wao na mashabiki wote wa Dortmund ikiwemo walioko Mexico na Marekani wanaamini katika ukuta mmoja tu nao ni YELLOW WALL na sio mwingine. Sio Dortmund tu wanaoonekana kuupinga ukuta huo.Lakini mchezaji wa zamani wa timu ya Monaco na Barcelona Rafael Marquez ambae ni raia wa Mexico anaonekana kukerwa na ukuta huo,kupitia ukurasa wake wa Twitter Marquez aliweka video ya goli lake alilowafungia Barcelona na kuandika “hakuna ukuta unaoweza kutusimamisha kama tunaweza kujiamini”.Ujumbe huo unaonekana ni kwa ajili ya raia wa Mexico akiwataka wajiamini na wasitishiwe na ukuta wa Trump. Tayari raisi wa Mexico Enrique Pena Nieto ameshasema hakubaliani na ukuta huo.Trump alipanga kukutana na Nieto wiki hii kujadili ujenzi wa ukuta huo.Lakini Nieto amesema Mexico haiamini kuhusu ukuta huo na hatakwenda Marekani kuonana na Trump
Uamuzi mpya wa serikali kuhusu matumizi ya uwanja wa Taifa Leo January 27, 2017 serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetangaza kuufungua uwanja wa taifa ilioufunga kwa muda usiojulikana. Waziri wa Wizara hiyo Mh. Nape Nnauye alitanga kufungwa kwa uwanja wa taifa baada ya uharibifu uliotokea wakati wa mechi ya Simba na Yanga iliyochezwa October 1, 2016. Mh. Nnauye amesema, ameridhishwa na ukarabati wa miundombinu ya uwanjani hapo uliofanywa kwa gharama za vilabu vya Simba na Yanga ndio maana ameamua kuufungua kwa ajili ya shughuli za kimichezo sambamba na matukio mengine ya kijamii.
Shekhan Rashid: ‘Ulimwengu atafanikiwa Sweden kama ilivyokuwa kwa Michael Olunga…Miezi 18 iliyopita mshambulizi raia wa Kenya, MichaelOlunga aling’ara katika michuano ya Cecafa Kagame Cup 2015 jijini Dar es Salaam na baada ya Mkenya huyo aliyekuwa akichezea Gor Mahia kuibuka mfungaji bora wa michuano ile ya Julai, 2015 klabu kubwa nchini za Yanga SC na Simba SC zilishindana kuhakikisha zinamnasa Olunga lakini hazikufanikiwa kutokana na mchezaji mwenye na klabu yake wakati huo kuhitaji kiasi cha zaidi ya milioni 100 ili kucheza ligi kuu Tanzania Bara. Baadae, Olunga alisajiliwa na klabuya Djurgardens ya Sweden ambayo kwa msimu mmoja alifanikiwa kufunga zaidi ya magoli kumi katika michezo 27 aliyochezea timu hiyo ya Sweden. Olunga ameondoka Sweden na kujiunga na klabu ya Guizhou Zhicheng ya China kwa usajili wa rekodi katika soka la Sweden-Dola million 40 zaidi ya bilioni 80 za Kitanzania. Olunga alicheza michezo michache sana hasa katika duru la pili kwenye ligi kuu ya Sweden msimu uliopita na kuifungia timu yake magoli muhimu. Sasa anaenda China kuvuna pesa nyingi. Nakubaliana na wewe kuhusu ulichoandika (niliandika namna nilivyoshangazwa na usajili wa Thomas Ulimwengu kutoka TP Mazembe na kujiunga na klabu ya AFC ya Sweden ambayo imepanda daraja msimu huu na itacheza ligi kuu.)” “Ni kweli Mazembe ni klabu kubwa ila napenda kukuambia Ulaya ni Ulaya tu, hata kama Mazembe wangekuwa wakimpa pesa nyingi, ila ujio wa Ulimwengu hapa Sweden nimzuri sana. Ataonekana zaidi kuliko akibaki kucheza Afrika. Narudia tena kusema, hata kama AFC watakuwa wanamlipa pesa ndogo kuliko Mazembe lakini Ulaya ni Ulaya tu kama ukiwa na malengo,” nasema kiungo wa zamani wa Kimataifa wa Tanzania, Shekhan Rashid ambaye kwa sasa anaishi nchini Sweden. Ulimwengu ameanza mazoezi katika klabu yake mpya AFC ambayo imesaini kwa mkataba wa miaka miwili kufuatia kushindwa kupata ofa alizotaraji kutoka klabu za Uturuki, Ubelgiji, na sehemu nyingine duniani. Ikumbukwe Ulimwengu aliichezea AFC mwaka 2010 akiwa kama mchezaji wa timu ya vijana katika klabu hiyo ya Sweden. “Nafasi kama hii siyo mbaya ikiwa amekosa ofa kutoka katika klabu za nchi nyingine kubwa kama Ufaransa ila kwa hapa Sweden akijituma kidogo tu atakwenda kwenye hizo nchi zenye ligi kubwa. “Kikubwa ni kumpa sapoti ili afanikiwe katika malengo yake,” anasisitiza Shekhan mchezaji wa zamani wa Singida United, Simba SC, Mtibwa Sugar, Moro United na Azam FC.
Alhamisi, 26 Januari 2017
EVRA HUYU HAPA, KAAMUA KUONDOKA JUVENTUS NA KUREJEA KWAO UFARANSA Beki wa kushoto wa zamani wa Man United, Patrice Evra sasa amerejea kwao Ufaransa. Evra amejiunga na Marseille ya kwao Ufaransa akitokea Juventus ya Italia. Klabu hizo mbili zimekubaliana mkataba wa miezi 18 baada ya Evra kuwa amekaa Juventus kwa takribani miaka mitatu akitokea Man United.
Jumatano, 25 Januari 2017
KAMA WEWE UNA PRESHA KUHUSIANA NA YANGA, BASI OMOG ANAWAZA MENGINE KABISA Kocha Mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog ametamba kwamba hatishwi na hali ya wapinzani wao Yanga kuwakaribia kileleni kwani kikosi chake bado kinaongoza kwenye ligi. Omog mpaka sasa ameisaidia Simba kukwea kileleni mwa ligi wakiwa na pointi 45 mbele kwa pointi mbili ya mahasimu zao Yanga ambao wanakamata nafasi ya pili wakiwa na pointi 43. Kocha huyo wa zamani wa Azam amesema kwamba kwake hatishwi na hali ya kukaribiwa na Yanga katika mbio za kuwania ubingwa kwa sababu bado kikosi chake kipo mbele na kinaongoza ligi. “Hatutishwi na Yanga kusogea karibu yetu badala yake ndiyo wanatupa hali ya kufanya vizuri kwenye mechi zetu zijazo ili tuweze kuwakwepa na mwishowe tuweze kutwaa ubingwa. “Wanachotakiwa kutambua kwamba sisi tuko mbele yao na mikakati yetu ni kuona hatuondoki kwenye nafasi hiyo mpaka mwisho wa msimu lakini tunatakiwa kuongeza juhudi zaidi kwenye mechi zetu zinazokuja kwa kupata ushindi,”alisema Omog. SOURCE: CHAMPIONI
CREDO MWAIPOPO AMTAKA MSUVA ACHANGAMKE SASA, NDIYO WAKATI WAKE WA ULAYA Kiungo wa Yanga anayefanya vizuri hivi sasa akiwa na kikosi cha timu hiyo, Simon Msuva huenda akatimka klabuni hapo mara baada ya kumalizika kwa mkataba wake baada ya kiungo wa zamani wa Yanga, Credo Mwaipopo kumtaka amfuate Ulaya. Msuva amebakiza mwaka mwaka mmoja na nusu kwenye mkataba wake wa kuitumikia Yanga. Credo ambaye anafanya shughuli zake nchini Sweden amesema kwa kiwango cha mchezaji huyo anatakiwa kuondoka hapa nchini na kwenda nchini humu kwani uwezo wake ni mkubwa. Mwaipopo, alisema kuwa kutokana na uwezo wa juu wa kucheza soka alionao hivi sasa Msuva hastahili kuendelea kucheza Ligi Kuu Bara bali akajaribu bahati yake ya Ulaya. “Nimekuwa nikifuatilia Ligi Kuu Bara na Msuva ni mmoja kati ya wachezaji ambao wanafanya vizuri, nimekuwa nikiwasiliana naye muda mrefu na kumwambia kuwa hatikiwi hivi sasa kuwa hapa nchini kutokana na uwezo wake. “Soka hivi sasa linalipa na kwa uwezo wake alionao hastahili kuwa hapo na ukizingatia umri wake bado mdogo ambao ndiyo unaohitajika zaidi Ulaya, Watanzania wengi tumeshindwa kufanya vizuri huko kutokana na kuchelewa kutoka nchini hivyo tulipofika huko tayari umri ulikuwa umeshatutupa mkono. “Naamini kabisa Yanga ni waelewa watamruhusu aondoke akajaribu bahati yake katika kipindi hiki ambacho bado umri wake unamruhusu na sisi tupo huko tunajua jinsi gani ya kumsaidia akishakwenda Sweden. “Nafikiri huyu ni Mtanzania na sisi kama Watanzania ni jukumu letu kumsaidia,” alisema Mwaipopo. Alipoulizwa Msuva kuhusiana na suala hilo alisema: Ushari wake huo nimeusikia ni mzuri na ameutoa muda mzuri ambao na mimi nilikuwa na ndoto za kwenda huko mara tu baada ya kumalizika kwa mkataba wangu na Yanga.” Msuva ambaye amekuwa msaada mkubwa kwenye kikosi cha Yanga kwa sasa ana mabao tisa sawa na kinara Shiza Kichuya kwenye Ligi Kuu Bara.
MWAMUZI ATAKAYEWECHEZESHA YANGA VS NGAYA YA COMORO HUYU HAPA Mwamuzi wa mchezo wa hatua ya awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Ngaya Club DE Mbe ya Comoro, amewekwa hadharani na Shirikisho la Soka Afrika (Caf). Mchezo huo unaotarajiwa kupigwa Februari 12, mwaka huu kwenye Uwanja wa Stade de Moroni uliopo katika Mji wa Moroni nchini Comoro, utachezeshwa na mwamuzi wa kati raia wa Shelisheli, James Fedrick Emile. Caf ikiwa tayari imemtaja mwamuzi huyo wa kati, lakini bado haijawaorodhesha wasaidizi wake ambao ni washika vibendera wawili, mwamuzi wa mezani na msimamizi wa mchezo huo. Baada ya mchezo huo, timu hizo zitarudiana Februari 17, mwaka huu jijini Dar na mshindi wa jumla atacheza hatua ya pili dhidi ya Zanaco ya Zambia au APR ya Rwanda. Yanga ambao ni wawakilishi wa Tanzania Bara kwenye michuano hiyo, kwa sasa inaendelea na maandalizi makali kuhakikisha inafanya vizuri huku ikiwa tayari imeanza harakati za chini chini za kuwachunguza wapinzani wao hao.
MASHABIKI WAMVAA MGOSI MAZOEZINI WAKITAKA MAELEZO KUHUSU KIWANGO CHA TIMU Meneja wa Simba Mussa Hassan Mgosi alilazimika kufanya kazi ya ziada kuwajibu na kutuliza mzuka wa mashabiki wa Simba. Mashabiki hao walimfuata Mgosi akiwa ametulia pembeni ya uwanja akifuatilia mazoezi ya Simba kwenye Uwanja wa Boko Veterani, jana jioni. Mashabiki wa Simba walikuwa na kero kadhaa lakini suala la wafungaji ndio lilikuwa likiwakera zaidi. Wengine waliamini wachezaji hawajalipwa mishahara yao kwa miezi kadhaa, jambo linalochangia wasicheze kwa kujituma. Baada ya mashabiki kadhaa kuweka hewani malalamiko yao, Mgosi alimjibu mmoja baada ya mwingine kwa ufafanuzi mzuri na mwisho kukata kiu Yao. Baadhi ya aliyowaeleza ni wao viongozi kuendelea kuwakumbusha wachezaji wao mara kwa mara kwamba Simba wanataka nini. Lakini akawasisitiza mashabiki kuendelea kuwaunga mkono bila ya kujali wako katika wakati upi.
KAHEMELE AACHIA NGAZI SIMBA Katibu Mkuu wa Simba, Patrick Kahemele ameachia ngazi. Taarifa kutoka kwa rafiki wa karibu wa Kahemele zinaeleza aliandika barua na kamati ya utendaji ya Simba, imepitisha hilo. Upande mwingine wa taarifa, umeeleza Kahemele anarejea na kujiunga na Azam TV ambako alikuwa akifanya kazi kabla. “Kweli anaondoka, leo kamati ya utendaji ya Simba imekubaliana naye,” kilieleza chanzo. Juhudi za kuwapata viongozi wa Simba walizungumzie hilo, zinaendelea.
Jumanne, 24 Januari 2017
KISA SIMBA, TFF YATANGAZA KUUFUNGIA UWANJA WA JAMHURI, MOROGORO Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema kuwa mechi namba 151 kati ya Mtibwa Sugar vs Simba kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, baada ya mchezo kumalizika mashabiki waliingia uwanjani kwa wingi na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wachezaji, waamuzi na waandishi wa habari. Pia kamera ya Azam Tv upande wa goli la Kusini iliangushwa na washabiki hao. Vilevile sehemu ya kuchezea (pitch) ya Uwanja wa Jamhuri iko katika hali mbaya ambapo inahitaji marekebisho makubwa ili iweze kuendelea kutumika kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom. TFF imebaini kuwa kitendo cha washabiki kuingia uwanjani baada ya filimbi ya mwisho, licha ya kuwa ni kinyume cha kanuni lakini pia kilichangiwa na askari polisi kutokuwa makini katika majukumu yao ya kusimamia usalama uwanjani na badala yake kuelekeza umakini katika kutazama mechi. Hivyo, Uwanja umesimamishwa kutumika kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom ili kutoa fursa kwa wamiliki kufanya marekebisho makubwa kwenye eneo la kuchezea.
MKUDE ALIA MTANDAO KUTAKA KUMCHANGANYA YEYE, WANASIMBA Nahodha wa Simba, Jonas Mkude amelalamika kulishwa maneno akisema kuna mtandao unaomsakama akionyesha hofu huenda kuna watu wanataka kuvivuruga Simba. Katika taarifa yake iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Simba, Mkude amesema suala la kusema yeye analalamikia mshahara halina ukweli wowote. "Jana usiku nilitumiwa taarifa ya upotoshwaji iliosambazwa na mtandao unaojiita Goal, eti wachezaji Simba wanadai mishahara ya miezi miwili," alisema. "Taarifa hiyo imesema mshahara ni chanzo cha timu kutofanya vizuri. Napenda kuwaarifu wanachama na washabiki wetu kuwa, taarifa hizo zinalenga kutuondoa katika nia yetu ya kuipa ubingwa Simba. "Kwa maana ya weledi wa uandishi, hilo si sahihi na si jambo jema," alisisitiza. "Naomba tushikamane na kuamini tunafanya vema, timu inayoongoza ligi na iliyofuzu kwenye raundi nyingine utasemaje inafanya vibaya," alihoji. Simba ndiyo kinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 45 wakifuatiwa kwa karibu na Yanga wenye pointi 43.
MANARA ASEMA TFF IKIENDA BILA KUBADILI TENA RATIBA, ATAMPOSA NA KUMUOA WEMA SEPETU, AAHIDI KUTEMBEA NA NGUO YA NDANI HADI TFF Na Haji S Manara Kuna kurogwa na kujiroga, kuna kufa na kujiua pia kulia na kuliliwa. Sisi Watanzania hakika tupo katika fungu la pili, fungu la kukosa , fungu mzigo, tunajiroga, tunajiua na tunaliliwa. Hakika hatujui twataka nini, hatujui malengo yetu, lakini kubwa hatujui hata tutokapo wala tuendako, na leo naandika kitu kidogo tu kinachotushindwa kwenye soka letu, RATIBA!! Wakati wenzetu wanazungumzia changamoto nzito na kubwa ktk maendeleo yao ya mchezo murua zaid duniani wa soka, Watanzania tunahangaika namna ya kupanga ratiba ya mechi zetu za ligi yetu na Kombe la Shirikisho, ratiba inayobadilishwa Kama nguo, tena mvaaji mwenyewe ni mbunifu wa mavazi au mwanamitindo, ambae huvaa nguo tano kwa siku. Siku za nyuma niliwahi kuwaambia Clouds FM kuwa, iwapo ratiba ya Ligi Kuu nchini isipopanguliwa ntatembea bila shati toka Mtaa Msimbazi hadi zilipo ofisi za TFF pale Karume Stadium. Nilidhani Kwa kusena vile walau TFF na bodi ya Ligi wataona haya na kuhakikisha ratiba ya Ligi kuu haitabadilishwa tena, kumbe ndio kwanza wakubwa wameweka gundi masikioni, toka wakati ule ratiba ishafumuliwa Mara tatu, na leo hii imebadilishwa tena, Kwa kisinguzio kile kile, eti ratiba za Caf na za ligi zimeingiliana. Ninajiuliza iwapo ratiba ya Ligi yetu ni muhali kuipanga,vipi kuhusu programu nyingine za maendeleo? Itakuwaje kuhusu timu yetu ya taifa juu ya ndoto zetu za mchana wa jua kali? vipi kuhusiana na zile programu hewa za soka la vijana, watoto na wanawake? Hakika kwetu hayo ni sawa na bahari ya Mediterranean au bahari kuu ya hadithi za Alfu Leila uleila, hatuwezi ratiba tutaweza kwenda Afcon 2019? Hatuwezi kupanga ratiba tutaweza kuwa na mipango madhubuti ya kuendeleza mchezo huu ambao yatajwa watu bilioni tatu duniani kote wanaushabikia? Kama tumerogwa aliyeturoga Kafa, hatuponi hadi kiyama , tutakapokutana nae mchawi wetu. Nimalizie Kwa kuwapa mtihani mwingine TFF na bodi ya Ligi, iwapo Kama ratiba yao ya Ligi kuu na Kombe la shirikisho haitabadilishwa kuanzia sasa hadi mwisho wa msimu, ntamposa mlimbwende Wema Sepetu, na akikubali ntamuoa, akikataa ntatembea na boxer toka nyumbani kwangu hadi TFF.
Mwamuzi aliyetoa penati na msaidizi wake aliyepiga wachezaji vichwa wafungiwa TFF imetoa maamuzi ya mechi ya Ligi Daraja la kwanza kati ya wenyeji Lipuli na Mshikamano. Kocha wa Mshikamano, Hamisi Kinonda amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 300,000 baada ya kuondolewa kwenye benchi kwa kupinga muda wa nyongeza wa dakika tano, na kumtolea lugha ya matusi Mwamuzi wa Akiba. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 40(11) ya Ligi Daraja la Kwanza. Wachezaji wa Mshikamano FC, John Mbise jezi namba 9, Abdallah Makuburi (5), Ally Mangosongo (12) na kipa Steven Peter (1) wanapelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kumshambulia Mwamuzi Bryson A. Msuya. Lakini pia Mwamuzi Bryson A. Msuya amefungiwa mwaka mmoja kwa kutozingatia sheria ipasavyo wakati akitoa penalti dhidi ya timu ya Mshikamano FC, na ripoti yake kufanana na ile ya Kamishna. Mwamuzi Msaidizi Namba Moja, Makongo Katuma amefutwa katika orodha ya waamuzi wanaotambuliwa na TFF kwa kuwapiga vichwa wachezaji wawili wa Mshikamano FC wakati Mwamuzi wa Kati alipokuwa akishambuliwa na wachezaji wa timu hiyo wakati wakipinga adhabu ya penalti dhidi yao. Adhabu hizo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 38(1) na 38(1c) na (1e) za Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Waamuzi. Mwamuzi Katuma pia alipata alama za chini ambazo zisingemruhusu kuendelea kuchezesha Ligi Daraja la Kwanza. Naye Mwamuzi wa Akiba, Hashim Mgimba ameondolewa kwenye ratiba kwa kuonyesha muda wa nyongeza (added time) tofauti na ule alioelekezwa na Mwamuzi. Adhabu dhidi ya Mgimba imezingatia Kanuni ya 38(1d) ya Ligi Daraja la Kwanza. Kamishna wa mechi hiyo Fidelis Ndenga wa Njombe ameondolewa kwenye ratiba ya makamishna kwa taarifa yake kufanana na ile ya Mwamuzi. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 39(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Makamishna. Pia Kamati imetoa mwito kwa vyombo vya usalama (askari polisi) kutumia nguvu za wastani katika kutuliza ghasia viwanjani, hasa pale wanapotaka kushughulikia eneo linalohusu wachezaji. Uwanja wa Kichangani umeondolewa kutumika kwa mechi za Ligi, hivyo klabu za Iringa sasa timu zao zitatumia Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora mjini humo kwa mechi zao la Ligi. Uwanja huo ulikuwa kwenye matengenezo ambayo tayari yamekamilika
Atawakuta kina Yondani, Morris, Dida wale wale kwa nini Okwi asirudi ? Okwi akianguka chini baada ya kukwatulia na Nadir Haroub ( Hisani) Nimesoma waraka wa Suleiman Dide kuhusu kurudi ama kutokurudi kwa Emmanuel Okwi. Yeye amesema kwamba haungi mkono Mganda huyo kurudishwa tena kwa wekundu hao wa Msimbazi akiweka mezani sababu mbili kuu 1.Anadai kuwa hajui muendelezo wa kiwango cha Okwi kule Denmark alikokuwa 2.Okwi ni moja ya wachezaji wasumbufu sana Nakubaliana na Sule kwa hoja zote mbili lakini kwa mawazo yangu ni kwamba kukalia benchi katika timu inayoshiriki Ligi Kuu nchini Denmark si sawa na kukaa benchi timu ya Ligi Kuu Tanzania Bara. Hapa namaanisha kuwa inawezekana kabisa kule alikutana na washambuliaji wazuri kuliko yeye na pia kule kunao mabeki imara kuliko Ligi ya Tanzania ambapo akija atawakuta walewale akina Agrey Morris, Kelvin Yondani, Shomari Kapombe, na makipa kama akina Dida, Barthez, na wengine ambao anajua namna ya kuwaonea hivyo kwangu mimi sioni shida akija kujiunga na timu yoyote ile Simba, Yanga au hata Azam FC. Hoja ya pili ya Sule ni kwamba Okwi ni msumbufu.Bado simbishii kabisa kwani hayo yapo wazi lakini kama akiingia mkataba na timu yoyote kati ya hizo, zina jukumu la kuidhibiti nidhamu yake. Tatizo lililopo kwa timu zetu ni kwamba wale wachezaji wanaoonekana kuwa na viwango wanadekezwa kama mayai ndiyo maana mara kadhaa wanafanya kama watakavyo lakini viongozi wakiwadhibiti naamini nidhamu yao itakuwa juu. Binafsi naamini Okwi akija Tanzania ataendelea kuwakimbiza sana tena sana Imeandikwa na Ezekiel Tendwa, mwandishi wa New Habari ambaye ametoa maoni yake. Unakubaliana au kupingana naye, au una cha kuongezea tuandikie kupitia barua mosesjohnmponda@gmail.com
Neymar amfikia Gaucho Mshambuliaji wa Barcelona, Neymar amemfikia kwa mabao gwiji wa klabu hio, Ronaldinho baada ya kufunga bao moja katika ushindi wa Barcelona wa mabao 4-0 dhidi ya Eibar. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil alifunga bao hilo baada ya kuuwahi mpira wa krosi ya kimo cha chini kutoka kwa Aleix Vidal. Hilo lilikuwa ni bao lake la kwanza tangu Oktoba mwaka jana na kumfanya kufikisha jumla ya mabao 94 akiwa na uzi wa Barcelona. Mabao hayo 94 ni sawa na idadi ya mabao ya gwiji mwingine wa Brazil, Ronaldinho aliyetoa burudani katika uwanja wa Nou Camp. kwa kufunga mabao 94 katika mechi 207. Neymar ameifikia rekodi hio ya mabao 94 katika mechi 164 huku umri wake ukimpa nafasi kubwa ya kufunga zaidi.
Jumatatu, 23 Januari 2017
MOHAMED DEWJI AIBUKA MSHINDI TUZO YA KIONGOZI BORA WA AFRIKA Bilionea kijana zaidi barani Afrika, Mtanzania Mohammed Dewji ameshinda tuzo ya Kiongozi Bora Afrika katika hafla iliyofanyika jijini Zurich nchini Uswiss. Dewji maarufu kama Mo ameshinda tuzohiyo inayojulikana kwa jina la African Leadership Person of The Year ambayo hutolewa kwa wafanyabiashara au viongozi wanaofanya vizuri. Mo ameshinda tuzo hiyo ambayo ni heshima kubwa kwake kwa kuwa watu kadhaa maarufu walikuwa wakipewa nafasi ya kuitwaa. Mfanyabiashara huyo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MeTL Ltd, hivi karibuni aliweka dau la Sh bilioni 20 kutaka kununua hisa asilimia 51 katika klabu ya Simba. Kabla amekuwa mdhamini na mfadhiri wa klabu hiyo akiwa msaada mkubwa wakati ikifika hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Afrika kwa kuing’oa Zamalek.
MROMANIA WA AZAM FC KUANZA KUONYESHA MAKALI YAKE VS SIMBA Kocha mpya wa Azam FC, Mromania, Aristica Cioaba, kwa mara ya kwanza Jumamosi ijayo anatarajiwa kukaa katika benchi kuiongoza timu hiyo itakapopambana na Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Uwanja wa Uhuru, Dar. Mromania huyo ambaye amepewa mkataba wa miezi sita na Azam akichukua nafasi ya Mhispania, Zeben Hernandez aliyetimuliwa mwishoni mwa mwaka jana, bado hajaanza kazi rasmi ya kuinoa timu hiyo kutokana na kukosa kibali cha kufanyia kazi hapa nchini. Meneja wa timu hiyo, Philip Alando, amesema: “Kila kitu tumekamilisha kwa maana ya kulipia gharama za kupata kibali, kilichobaki kwa sasa ni kusubiri tu uhamiaji kuona ni lini watatupatia hicho kibali. “Kwanza tumeomba kibali cha kazi, tutakapokipata, ndipo tutafanya mchakato wa kuomba kibali cha makazi, matarajio yetu ni kuona kabla hatujapambana na Simba tumekamilisha kila kitu ili kocha wetu huyu aanze rasmi kazi.” Ikumbukwe kuwa, kwa sasa kikosi cha Azam kinanolewa na kocha wa muda, Idd Nassor Cheche baada ya Zeben na benchi lake la ufundi lililokuwa likiundwa na Wahispania watano kufutwa kazi kutokana na matokeo mabaya waliyokuwa wakiyapata
AZAM FC YAIPIGA COSMO 3-1, YATINGA 16 BORA FA CUP MABAO matatu yaliyofungwa na nahodha John Bocco, Shaaban Idd na Joseph Mahundi, yametosha kabisa kuivusha Azam FC kwenye hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) ikiichapa Cosmo Politan 3-1 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Azam FC iliuanza mchezo huo kwa kasi katika dakika 15 za kwanza za mchezo huo, lakini ilishindwa kuipenya safu ya ulinzi ya Cosmo kufuatia eneo la ushambuliaji na kiungo kutoelewana vizuri. Dakika ya 16 Bocco alikaribia kuipatia bao la uongozi Azam FC, lakini kichwa cha chini alichopiga kilitoka sentimita chache ya lango la Cosmo Politan, dakika 15 baadaye Yahaya Mohammed, naye alikosa nafasi ya wazi akiwa ndani ya eneo la 18 baada ya mpira aliopiga kupaa juu ya lango. Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, timu zote zilienda mapumziko zikiwa hazijafungana, Azam FC ilikianza kipindi cha pili kwa kufanya mabadiliko ya wachezaji wawili ikiwatoa kiungo Frank Domayo na Yahaya na kuwaingiza Joseph Mahundi na Shaaban Idd. Mabadiliko hayo yaliongeza kasi kwa upande wa Azam FC kutokana na kuongeza presha langoni mwa Cosmo, ambapo dakika ya 49 Shaaban alimiliki vema mpira ndani ya eneo la 18 mbele ya mbele ya mabeki lakini shuti alilopiga lilimlenga kipa wa Cosmo. Dakika ya 69 Bocco aliwanyanyua vitini mashabiki wa Azam FC baada ya kutumia uzembe wa kipa wa Cosmo aliyeupiga mpira uliombabatiza kwenye kisigino na kujaa wavuni. Bocco hakushangilia bao hilo kama alivyoahidi kabla ya mchezo huo kutokana na timu hiyo kuwa ndiyo iliyomlea na kumtoa kabla ya kusajiliwa na Azam FC. Shaaban aliifungia bao la pili Azam FC dakika ya 76 akimalizia mpira uliotemwa na kipa wa Cosmo kufuatia shuti alilopigiwa na Bocco. Mahundi alipigilia msumari wa mwisho langoni mwa timu hiyo dakika ya 80 baada ya kupiga shuti kali lililojaa wavuni akiwa ndani eneo la 18. Hadi dakika 90 za mchezo huo zinamalizika, Azam FC iliondoka uwanjani na ushindi huo mnono na sasa inasubiria kupangiwa mpinzani wake atakayepambana naye katika hatua ya 16 bora. Mara baada ya mchezo huo, Azam FC inatarajia kushuka tena dimbani Jumamosi ijayo kupambana na Simba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodadom Tanzania Bara (VPL) utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Kikosi cha Azam FC leo: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Gadiel Michael, Yakubu Mohammed, Aggrey Morris, Stephan Kingue/Singano dk 73, Himid Mao, Salum Abubakar, Frank Domayo/Mahundi dk 45, John Bocco (C), Yahaya Mohammed/Shaaban dk 45
Ijumaa, 20 Januari 2017
AISHI MANULA AANDIKA REKODI YAKE, SASA DAKIKA 630 BILA YA KUFUNGWA HATA BAO MOJA Suluhu waliyoipata Azam, juzi Jumatano dhidi ya Mbeya City, imemfanya kipa wa Azam, Aishi Manula, kucheza mechi saba mfululizo ambazo ni sawa na dakika 630 bila ya kuruhusu wavu wake kutikiswa. Manula ambaye anasifika kwa uhodari wa kuokoa mikwaju ya penalti, amefanikiwa kufanya hivyo katika michezo miwili ya Ligi Kuu Bara na Kombe la Mapinduzi. Mara ya mwisho kwake kuruhusu bao ilikuwa ni Desemba 24, mwaka jana kwenye sare ya bao 1-1 dhidi ya Majimaji kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea. Baada ya hapo, akaiongoza Azam kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Prisons, kisha kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi matokeo yalikuwa hivi; Azam 1-0 Zimamoto, Azam 0-0 Jamhuri, Azam 4-0 Yanga, Azam 1-0 Taifa Jang'ombe na Azam 1-0 Simba. Manula anatakiwa kufanya hivyo kwenye mechi nne zijazo ili kuipiku rekodi ya Muivory Coast, Vincent Angban ambaye kabla ya kuvunjiwa mkataba na Simba, msimu huu alicheza mechi kumi za kimashindano bila ya kuruhusu bao.
KAMA NDIYO HIVI, UWANJA WA JAMHURI UONDOLEWE LIGI KUU KWA wanaofuatilia michezo na hasa soka kwa muda mrefu watakuwa wanakumbuka namna Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya ulivyokuwa kero katika mchezo wa soka nchini. Uwanja huo ulikuwa mbaya kwelikweli kwa maana ya kiwango hasa katika sehemu ya kuchezea. Vyombo vya habari vilipiga kelele sana kuhusiana na uwanja huo ambao baadhi ya sehemu zake zilikuwa na changarawe na kusababisha sehemu hiyo kuwa hatari kwa afya za wachezaji. Nakumbuka wakati fulani kuna mtu mmoja aliyejitambulisha kuwa ni Mnyakyusa wa Mbeya, alisema amechoshwa na kelele zangu kwa Uwanja wa Sokoine kwa kuwa aliona ninausakama wakati kuna viwanja vingi vibovu hapa nchini! Alitaka niachane na uwanja huo kwa kuwa naweza nikazungumzia wa mkoa ninaotoka. Sikuwahi kuacha kwa kuwa nilijua ninachokizungumzia. Hoja zangu zilikuwa ni kwamba uwanja unaingiza fedha na wahusika hawakujali wanaowaingizia fedha hizo wanakuwa katika hali gani. Wanaoingiza fedha ni wachezaji, kwa uwanja ulivyo wanakuwa katika hatari muda wote wa mchezo na lazima wanakuwa na hofu. Tukubaliane kuwa hofu hiyo inasababisha kupotea kwa burudani ambayo wengine wanaopeleka fedha hiyo ni wale wanaokwenda kuwaangalia wachezaji. Hawapati burudani kwa kuwa watoa burudani wanakuwa wamejawa hofu ya uhakika wa afya yao. Daktari wa Simba, Yassin Gembe alimzuia kiungo wa Simba, Mohammed Ibrahim kuivaa Mtibwa Sugar na akaeleza kwamba Uwanja wa Jamhuri si rafiki kwa afya za wachezaji. Mo Ibra ndiyo alikuwa anarejea baada ya kuwa majeruhi. Juzi wakati Simba ikipambana na Mtibwa Sugar, hakika ni aibu na kama wahusika wanaosimamia matunzo ya uwanja huo basi walitakiwa kuachia ngazi mara moja. Uwanja huo kama unakumbuka Championi liliwahi kuanika vyoo vichafu vya uwanja huo, mazingira hovyo kabisa, hali ambayo baadaye ilisababisha hali ya kutoelewana kati ya gazeti na wahusika wa uwanja huo ambao kwa akili yao ilivyo, waliona wanaandamwa. Cha kushangaza baada ya hapo wakafanya marekebisho. Kwa sasa, uwanja huo bila ya ubishi haufai kabisa kutumika katika michuano kama ya Ligi Kuu Bara na hakuna ubishi kwamba Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) inaonekana wazi kushindwa kuelewa umuhimu wa afya za wachezaji. Nawakumbusha, mpira hauchezwi jukwaani, kwanza ni uwanja wa kuchezea ndiyo majukwaa. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), nalo limeshindwa kusimamia na kuonyesha afya za wachezaji ni muhimu. Kwani kama lingekuwa makini, lingeagiza uwanja huo kufungwa na mechi zichezwe kwingine. Kama TFF au TPLB wangekuwa makini, wangekuwa wakali na kuagiza uwanja huo kufungiwa, basi wahusika wangekosa fedha na baada ya hapo kuuboresha. Kwa sasa hakuna wanachokosa, hakuna hasara wanayopata na wanaingiza mamilioni huku wakitoa huduma ya hovyo na duni kabisa. Unaweza kusema uwanja huo unazinyonya klabu zinazoutumia na kuchangia hasara kuu. Nani asiyejua matibabu ni gharama? Kama wachezaji wanaumia maana yake klabu zinalazimika kuingia gharama kuhakikisha wanapona. Unaweza kuumia kwenye uwanja mzuri lakini nafasi ya kuumia kwenye uwanja mgumu, mbovu na wenye mabonde kama majaruba mfano huo wa Jamhuri inakuwa kubwa maradufu. Kama kuna nguvu za kukuza mpira nchini, kupitia viwanja kama Jamhuri ni kujidanganya na hakika, unapaswa kufungiwa hadi hapo utakapofanyiwa marekebisho na kuwa katika ubora sahihi. Jamhuri ni uwanja wa hovyo kabisa ambao unachangia kuporomosha kiwango cha soka nchini na wahusika kama TFF, TPLB nao wamelala kwa kuwa wanajua mwisho wanakusanya kinachowahusu na kuziachia klabu maumivu makali ya gharama. Kwa mashabiki nao wanabaki na maumivu ya kutoona au kushuhudia kile walichokuwa wanakiratajia kama burudani kwa kuwa wanaohusika na uwanja wamepata chao. Hii ni dhuluma ya wazi, ni dharau bila ya woga na tabia mbaya ya kujali unachoingiza bila kujali uhakika na ubora wa huduma unayoitoa. Hakuna ubishi, ni dalili ya kufeli.
Billic amuonyesha Payet dawa ya jeuri ni kiburi Baada ya Dimitri Payet kuigomea timu yake ya Westham sasa amerudi mazoezini.Payet ambae alikataa kufanya mazoezi na kikosi chake ili kulazimisha uhamisho wake.Lakini kocha mkuu wa Westham Slaven Billic amemuonesha Payet kitendo ambacho kinaonekana kama kutojali uwepo wake klabuni hapo. Slaven Billic amempiga stop Payet kupasha na kikosi cha kwanza.Lakini mara nyingi mchezaji asipopasha na kikosi cha kwanza hupelekwa kupasha na kikosi cha hakiba.Lakini Billic hataki kumuona Payet hata kwenye kimosi cha hakiba na amempeleka akapashe katika kikosi cha watoto. Dimitri Payet amekuwa akihushishwa na kuchoshwa na Westham kiasi cha kulazimisha auzwe.Klabu ya Ufaransa ya Marseille imekuwa ikihusishwa na kutaka kumrudisha nyumbani katik ligi ya Ligue 1,lakini pia Chelsea na Manchester United nao hawako mbali baada ya mgomo huo wa Payet.Kocha wa Westham amempeleka Payet katika kikosi cha vijana chini ya miaka 23 hadi suala lake litakapoisha. Tayari mabosi wa Westham wamesema winga huyo hauzwi lakini kwa hali inavyoendelea Westham wanaonekana kuanza kuchoshwa na Payet.Ni mwezi wa pili tu mwaka jana ambapo Payet alisaini mkataba mpya wa £125,000 kwa wiki lakini anataka zaidi. Mwenyekiti mwenza wa Westham bwana David Gold alisema “Payet hauzwi,ni mwaka jana tu alisaini mkataba mrefu tunataka aliheshimu hilo,toka amekuja hapa mashapiki wamekuwa wakimpa ushirikiano mkubwa sasa inapaswa aheshimu swala hilo”. Westham United ni kati ya timu yenye mashabimi wakorofi Uingereza na wamekasirishwa sana na Payet.Kwenye mechi yao dhidi ya Crystal Palace walisikika wakiimba nyimbo za kumtusi Payet.Picha ya mshambuliaji huyo iliyoko nje ya uwanja wa Westhamwa London Stadium inalindwa na polisi kuogopa mashabiki wahuni wa timu hiyo kuichana. Hali inayomkumba Payet ni tofauti na ile ya Diego Costa wa Chelsea kwani yeye baada ya timu kutosafiri naye kuwakabili Leicester alianza mazoezi binafsi na sasa amerudi timu ya kwanza kupasha nao.
ULIMWENGU ATUA LIGI KUU YA SWEDEN MIAKA MIWILI , DAR ES SALAAM MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu anaondoka nchini leo kwenda kukamilisha usajili wake klabu ya AFC Eskilstuna ya Ligi Kuu ya Sweden. Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Ulimwengu amesema kwamba baada ya mazungumzo ya awali na klabu hiyo anakwenda kusaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo, ambayo awali ilikuwa inajulikana kama FC Cafe Opera na Vasby United. “Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa watu wangu wote wa karibu kama Jamal Kisongo ambao wamekuwa karibu na mimi kwa kipindi chote hiki na kunipa ushauri hadi kufikia maamuzi haya ya kujiunga na timu hii. Tumekataa ofa nyingi sana na kuikubali hii kwa sababu za msingi sana,”alisema. Thomas Ulimwengu anakwenda kukamilisha usajili wake klabu ya AFC Eskilstuna ya Ligi Kuu ya Sweden Ulimwengu alisema kwamba anashukuru Mungu ndoto zake za kucheza Ligi Kuu Ulaya zinatimia na ataitumia AFC Eskilstuna kama daraja la kupandia timu kubwa barani humo. “Kila kitu ni malengo tu, inategemea na mtu unataka kitu gani katika wakati gani, nakwenda AFC Eskilstuna kucheza mpira kama nilivyocheza TP Mazembe ili nionekane nisogee mbele zaidi,”alisema. Ulimwengu aliyezaliwa Juni 14, mwaka 1993 aliibukia katika taasisi ya soka Tanzania (TSA) mwaka 2008, kabla ya mwaka 2009 kwenda kuanza kukomazwa Ligi Kuu katika klabu ya Moro United alikokuwa akicheza kwa mkopo hadi mwaka 2010 alipokwenda akademi ya Athletic FC ya Sweden, alikocheza hadi 2011 TP Mazembe alipochukuliwa na timu ya vijana ya Mazembe. Alicheza U-20 ya Mazembe kwa msimu moja kabla ya kupandishwa rasmi timu ya wakubwa mwaka 2012 na moja kwa moja kuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza hadi anamaliza Mkataba wake Oktoba mwaka jana. Ulimwengu anajivunia kushinda mataji makubwa akiwa na Mazembe kama Ligi ya Mabingwa Afrika, Super Cup ya Afrika na pamoja na kucheza Klabu Bingwa ya Dunia.
YANGA NA ASHANTI JUMAMOSI, SIMBA NA POLISI JUMAPILI KOMBE LA TFF Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM YANGA SC wataanza kutetea Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwa kumenyana na Ashanti United, zote za Dar es Salaam wikiendi hii. Mchezo huo wa hatua ya 32 Bora umepangwa kufanyika Jumamosi Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam baada ya Ashanti kuitoa timu ngumu ya Daraja la Kwanza, Friends Rangers. Vigogo wengine, Simba SC watashuka Uwanja wa Uhuru Jumapili kumenyana na Polisi Dar es Salaam, wakati washindi wa pili wa mwaka jana, Azam FC watamenyana na Cosmopolitan Jumatatu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa jioni hii na TFF, mechi nyingine za Jumamosi ni kati ya Alliance na Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Maji Maji na Mighty Uwanja Maji Maji, Songea, wakati Jumapili mbali na Simba na Polisi Dar, Ruvu Shooting itamenyana na Kiluvya United Uwanja Mabatini, Toto Africans na Mwadui Uwanja wa CCM Kirumba na Mbeya Worriors na Prisons Uwanja Sokoine, Mbeya. Mbali na Azam na Cosmo, mechi nyingine za Jumatatu ni kati ya Stand United na Polisi Mara Uwanja Karume, Musoma, Ndanda FC na Mlale JKT Uwanja Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, wakati Jumanne Mtibwa Sugar watamenyana na Polisi Moro Uwanja wa Uwanja Jamhuri, Morogoro, Kurugenzi FC na JKT Ruvu Uwanja wa Mafinga, Mbeya City na Kabela City Uwanja Sokoine, Madini na Panone Uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Hatua ya 32 Bora itakamilishwa kwa mechi mbili Jumatano, Singida United wakiikaribisha Kagera Sugar Uwanja wa Namfua, Singida na African Lyon na Mshikamano Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Hata hivyo, mchezo wa Lyon na Mshikamano unaweza kusogezwa mbele ikibidi. RATIBA KAMILI 32 BORA ASFC Januari 21, 2017 Alliance Vs Mbao (CCM Kirumba, Mwanza) Maji Maji Vs Mighty (Maji Maji, Songea) Yanga Vs Ashanti United (Uhuru, Dar es Salaam) Januari 22, 2017 Ruvu Shooting Vs Kiluvya United (Mabatini, Mlandizi) Toto Africans Vs Mwadui (CCM Kirumba, Mwanza) Simba SC Vs Polisi Dar (Uhuru, Dar es Salaam) Mbeya Worriors Vs Prisons (Sokoine, Mbeya) Januari 23, 2017 Stand United Vs Polisi Mara (Karume, Musoma) Azam FC Vs Cosmopolitan (Azam Complex, Chamazi) Ndanda FC Vs Mlale JKT (Nangwanda Sijaona, Mtwara) Januari 24, 2016 Mtibwa Sugar Vs Polisi Moro (Jamhuri, Morogoro) Kurugenzi FC Vs JKT Ruvu (Mafinga, Iringa) Mbeya City Vs Kabela City (Sokoine, Mbeya) Madini Vs Panone (Sheikh Amri Abeid, Arusha) Januari 25, 2017 Singida United Vs Kagera Sugar (Namfua, Singida) African Lyon Vs Mshikamano (Uhuru, Dar es Salaam)
Alhamisi, 19 Januari 2017
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)