Jumanne, 1 Novemba 2016

YANGA WASEMA WAKO TAYARI KWA AJILI YA MBEYA CITY ILIYO NYUMBANI KWAO

Yanga wanaamini wako tayari kwa ajili ya mechi ya kesho dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya. Yanga ni wageni lakini Kocha Hans ven der Pluijm amesema wamejiandaa vema wakati leo itakuwa ni siku moja kabla ya pambano. “Kila mmoja anajua itakuwa ni mechi ngumu, tunataka kushinda na tupo tayari. Tunajua Mbeya City ni timu ngumu, wako kwao, lakini tunataka kushinda,” alisema. Yanga waliwasili Mbeya jana na kupokelewa na mashabiki wao kwa wingi ambao walionyesha kuwa wanahitaji furaha kwa wao kushinda, kesho. Baada ya mechi hiyo, Yanga wataendelea kubaki mjini Mbeya kuisubiri Prisons katika mechi itakayopigwa kwenye uwanja huohuo, Jumamosi. Kabla ya mechi ya kesho, Yanga imeonekana ni moto wa kuotea mbali baada ya kushinda mechi tatu kwa jumla ya mabao 13. Ilianza kwa kuitwanga Kagera Sugar kwa mabao 6-2, ikarejea Dar es Salaam na kuivurumisha JKT Ruvu kwa mabao 3-0 kabla ya kuiranda Mbao FC kwa 3-0.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni