Jumapili, 27 Novemba 2016

OMOG AWAONYESHA SIMBA HATAKI LAWAMA, AKATAA KUTAJA JINA LA MCHEZAJI ANAYEMTAKA Kocha Joseph Omog ameonyesha hataki kuingia kwenye wingu la lawama baada ya kutotamka jina la mchezaji yoyote anayemtaka. Pamoja na kuandika kwamba anataka beki wa kati, kipa na mshambuliaji, Omog amewaachia kamati ya usajili ya klabu hiyo wafanye yao. “Kweli kocha ahajataja jina la mchezaji hata mmoja, hasa kutokea nje. Badala yake uongozi wa kamati ya usajili ndiyo utafanya kazi hiyo,” alisema. Tayari kamati ya Utendaji ya Simba ilikaa na kamati ya usajili na kujadili masuala mbalimbali ambayo yanahusiana na usajili. Simba ilimaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara ikiwa inaongoza kwa pointi mbili tu baada ya kupoteza mechi mbili za mwisho dhidi ya African Lyon na Prisons ya Mbeya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni