Jumanne, 29 Novemba 2016

Maneno ya Pogba Pengine tunakabiliwa na laana Paul Pogba amewatania wachezaji wenzake wa Manchester United kwa kuwaambia hivi karibuni wataanza kuamini kuwa wana mkosi endapo wataendelea kupata matokeo ya sare katika uwanja wao wa nyumbani. United wametoka sare katiki Uwanja wa Old Trafford dhidi ya Stoke City, Burnley, Arsenal na West Ham, matokeo ambayo ni mabaya zaidi kuwahi kupata timu hiyo katika Premier League. Pogba alitoa pasi ya goli la kusawazisha kwa Zlatan Ibrahimovic kwenye mchezo uliomalizika kwa sare ya 1-1 dhidi ya Wesh Ham Jumapili ya wikiendi iliyopita. “Siku si nyingi tutaanza kuamini tuna laana,” Pogba alisema. “Haijalishi timu ipi inakuja hapa, tunawatalawa, ilikuwa kwa Arsenal na hata dhidi ya West Ham juzi. “Ipo siku bahati yetu itakuja tu iwe leo ama siku yoyote ile na hapo ndipo tunapaswa kuitumia kwa uhakika. “Bado nina imani kubwa na timu kwasababu tunatengeneza nafasi nyingi sana. Bahati itakuja tu, Nina imani kubwa sana na timu yangu. Kikubwa tunachopaswa kufanya ni kuwa na makini na makosa madogo-madogo “Tuliruhusu mabao rahisi dhidi ya West Ham na Arsenal pia. Ni makosa madogo madogo tu. Bado nina imani kubwa kila kitu kitakuwa sawa tu. Tunapoteza pointi kirahisi mno, lakini tutatoboa tu. United watakuwa na kibarua kingine dhidi ya West Ham tena kwenye mchezo wa robo fainali ya Kombe la Ligi kesho

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni