pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumatatu, 28 Novemba 2016
ZAHA AICHAGUA IVORY COAST Winga wa Crystal Palace Wilfred Zaha amechagua kuichezea timu ya Taifa ya Ivory Coast na kuachana timu ya Taifa ya England. Mchezaji huyo ,24, aliwahi kucheza katika kikosi cha chini ya miaka 21 cha England na baadaye kuitwa katika kikosi cha wakubwa ambapo alicheza kwenye mechi dhidi ya Sweden Novemba 2012, na Scotland, August 2013. Hata hivyo mechi hizo zote hazikuwa za ushindani ,hivyo imekuwa si pingamizi kwa Zaha ambaye ni mzaliwa wa Abidjan,kuweza kujiunga na timu ya taifa ya Ivory Coast. Taarifa ya winga huyo kuwachagua tembo hao imethibitishwa na shirikisho la soka la Ivory Coast jana jumapili na hivyo kuweka matarajio ya kumuona akiwa na kikosi hicho kwenye michuano ya AFCON 2017, Gabon. Zaha amezaliwa mjini Abidjan, Ivory Coast , akiwa na umri wa miaka minne alihama pamoja na familia yake kwenda mjini London na alipofikisha umri wa miaka 12 alijiunga na Academy ya Crystal Palace.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni