pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumanne, 29 Novemba 2016
AZAM FC YAPATA MWENYEKITI MPYA, NI ALIYEKUWA MAKAMU MWENYEKITI Makamu Mwenyekiti wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Nassor Idrissa, amepanda cheo na kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo. Idrissa anachukua nafasi ya aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo Alhaji Said Mohamed Abeid, aliyefariki dunia mwanzoni mwa mwezi huu. Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, na kuituma kwenda kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwafahamisha mabadiliko hayo, imeeleza kuwa Shani Christoms Mligo, ndiye atakuwa Makamu Mwenyekiti mpya wa timu hiyo akichukua nafasi ya Idrissa. Mabadiliko hayo ya kiuongozi yamefanywa na Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC, ambapo uteuzi huo umeanza rasmi leo Novemba 29 mwaka huu.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni