Jumapili, 27 Novemba 2016

KIMYAKIMYA, LWANDAMINA, PLUIJM WAKUTANA NA KUFANYA KIKAO FARAGHA Mkurugenzi wa Ufundi wa Yanga, Hans van der Pluijm na kocha mkuu mpya wa kikosi cha Yanga, George Lwandamina, wamekaa kikao kujadili mambo kadhaa. Lwandamina na Pluijm wamekutaka kwa lengo la kuweka mikakati kabla ya kuanza kazi. Habari za uhakika kutoka Yanga zimeeleza, wawili hao wamekutana na kuweka mikakati ikiwa ni pamoja na Lwandamina kuuliza maswali aliyotaka kujua kutoka kwa Pluijm. "Lwandamina alitaka kujua mambo kadhaa na Pluijm aliahidi kumpa ushirikiano na kweli imekuwa hivyo," kilieleza chanzo. Kazi ya hao wawili inaanza kesho wakati Lwandamina atakapokiongoza kikosi chake mazoezi na kuwaona wachezaji wake kwa mara ya kwanza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni