Jumatano, 23 Novemba 2016

CHOMBO KIPYA CHA CRISTIANO RONALDO Imeripotiwa kuwa nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amerejea tena katika game ya mapenzi, wiki iliyopita mchezaji huyo ameonekana huko Disneyland,Paris akiwa na mwanadada mrembo Mhispania Georgina Rodriguez anayedaiwa kuwa ndiye mpenzi wake mpya. Cristiano alionekana akiwa amevalia wigi,Hoodie, kofia ya Baseball na miwani ya jua ili asiweze kutambulika kwa uharaka lakini watu waliweza kumtambua na kumpiga picha akiwa na mrembo huyo Picha za Ronaldo na mwanadada huyo wakiwa huko katika mji mkuu wa France zilinaswa, na nyingine wakionekana wakibusu. Wawili hao imeripotiwa kuwa kwa mara ya kwanza walikutana kwenye tukio (event) la Dolce & Gabbana ambapo walikuwa wamekaa VIP. Inasemekana Georgina anafanya kazi kwenye Store ya Gucci mjini Madrid. Pia hivi karibuni Ronaldo alimualika mwanadada huyo kwenda Santiago Bernabeu kuangalia mechi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni