Jumatano, 23 Novemba 2016

Hatutacheza dhidi ya Yanga kama waamuzi hawatatoka nje ya nchi- Manara Uongozi wa klabu ya Simba umesema, haukotayari timu yao kucheza dhidi ya Yanga kama mchezo wao utachezeshwa na waamuzi wa ndani (Tanzania). Afisa habari wa Simba Haji Manara amesema, Simba ipo tayari kukatwa mapato ya mchezo huo kwa ajili ya kugharamia waamuzi kutoka nje kuja kuchezesha mchezo wa Simba vs Yanga. “Hatutacheza mechi yoyote dhidi ya Yanga kama itachezeshwa na mwamuzi wa hapa nyumbani, sio kama hatuwatambui au hatuwaheshimu lakini tumechoka,” Manara ametoa kauli hiyo wakati akilalamikia timu yao kuonewa na waamuzi kila inapocheza dhidi ya watani wao wa jadi. “Mwaka jana mnakumbuka yule referee Deonensia Nkya nilieleza matatizo aliyoyafanya sasa tumeshachoka, waendelee kuchezesha tunawaheshimu sana tunajua kazi yao ni nzuri wanaifanya katika mazingira magumu lakini derby hii ya Yanga na Simba sasa inabidi kuchezeshwa na marefa kutoka nje.” “Simba ipo tayari kutoa sehemu ya mapato yake kwenye mchezo huo kuleta marefa, tunataka fair game.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni