Jumanne, 29 Novemba 2016

Balaa la El Clasico limeshaanza mitandaoni Tayari kumekuwa na shauku kubwa kuelekea mchezo wa La Liga kati ya Barcelona dhidi ya Madrid ‘El Clasico’ utakaopigwa mwishoni mwa juma hili. Jumamosi ijayo macho yote yatakuwa Camp Nou wakati FC Barcelona wakiwakabili wapinzani wao Real Madrid kwa mara ya kwanza msimu huu. Miamba hiyo ya soka la Canalan wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa nyuma ya Madrid kwa pointi sita kufatia sare ya 1-1 waliyoipata ugenini dhidi ya Real Sociedad wakati wa mchezo wa La Liga weekend iliyopita. Real Madrid bado hawajapoteza mchezo wakiwa na pointi 31 kitu kitakachowafanya Barcelona kuwa na shauku ya kuivuruga rekodi hiyo. Kuna athari za majeruhi kwenye vikosi vya timu zote, Andres Iniesta anatarajiwa kurejea kikosi kwa upande wa Barcelona wakati Gareth Bale yeye hayupo kabisa kwenye kikosi cha Real Madrid. Pambano hilo la la miamba ya soka ya Hispania limeanza kutoa fursa kwa wadau kuanza kuweka mijadala mezani na mtu wa kwanza kutumia fursa hiyo ni model Iryna Ivanova wa Russia. Amekuwa akitumia picha kadhaa kuteka mashabiki kwenye mitandao ya kijamii. Mlimbwende huyo alitupia picha mbili kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa kuwauliza mashabiki wake wanamhusudu mchezaji gani kati ya Leo Messi na Cristiano Ronaldo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni