Jumatatu, 28 Novemba 2016

YANGA MAPEMAAA, YAMUANDALIA MKATABA TAMBWE, AKITUA TU, KAZI KWISHA anga imeonyesha haitaki kusubiri mambo yaende yasivyo baada ya kuona mkataba wa mshambuliaji wake nyota Amissi Tambwe unakwenda ukingoni, kwani tayari imeanza kumuandalia mkataba mpya ili imalizane naye, mapemaa. Mrundi huyo aliyetua Jangwani Desemba 15, 2014 akitokea Simba, amebakiza miezi sita kabla ya kumaliza mkataba wake na Yanga. Kwa mujibu wa kanuni za Fifa, anaruhusiwa kuanza mazungumzo na timu nyingine. Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alisema ni vigumu kumuachia mshambuliaji huyo aondoke kwenye timu hiyo na badala yake watamuongezea mkataba mwingine wakati wowote. Sanga alihoji itawezekana vipi kumuachia mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao! Hivyo hizo timu zinazopiga hesabu za kumsajili nyota huyo, zifute ndoto hizo. Aliongeza kuwa, uongozi huo umepanga kukaa naye meza moja kwa ajili ya kuujadili mkataba mpya katika kuhakikisha anabaki kuendelea kuichezea Yanga kwa misimu mingine miwili. "Ujue tutaonekana watu wa ajabu kumuachia Tambwe aondoke kwenye timu yetu, utamuachaje mshambuliaji anayeifungia timu mabao? Haitoshi ana rekodi nzuri ya kuwa mfungaji bora mara mbili kwenye misimu tofauti kwenye ligi kuu. "Hivyo, Wanayanga wala wasiogopeshwe na vitisho kutoka kwa wapinzani wao, Tambwe atabaki kuichezea Yanga kwenye misimu mingine ijayo ya ligi kuu, ninaamini kila mtu anajua uwezo wake wa kufunga mabao. “Tumepanga kukutana hivi karibuni kwa ajili ya kuujadili mkataba mpya na kikubwa ni dau la usajili na malipo ya mshahara ambao tumepanga kumboreshea ili tumshawishi abaki Yanga,” alisema Sanga.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni