Ijumaa, 25 Novemba 2016

KAMA UNAKIPIGA MAJIMAJI HALAFU UNATAKA KUSEPA ZAKO, MANENO YAKO HAYA HAPA Pamoja na kuboronga katika raundi ya kwanza, uongozi wa Majimaji umewaweka wazi wachezaji wao kuwa wala wasiwe na presha kuwa mwenye kupata fursa kwingine kipindi hiki cha uhamisho wa dirisha dogo, yupo huru kuondoka. Katibu wa timu hiyo iliyoshinda mechi tano tu kati ya 15 na kumaliza kwenye nafasi ya 13, John Mbano amesema kuwa karibu wachezaji wote wanamaliza mikataba yao mwisho wa msimu, hivyo yeyote aliyepata ofa nzuri, ni jambo la kufuata taratibu za usajili kwani nao wako mawindoni kusaka mabeki na washambuliaji kama kocha Kally Ongala alivyopendekeza katika ripoti yake. “Bahati mbaya sana karibu timu nzima mikataba yao inafika mwisho baada ya msimu huu, hivyo kama kutakuwa na aliyepata ofa nzuri hatuwezi kuweka kipingamizi. Ni suala la klabu husika kufuata taratibu zote za kiusajili lakini hakuna mchezaji tunayeweza kumng’ang’ania,” alisema Mbano. SOURCE: CHAMPIONI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni