Jumamosi, 26 Novemba 2016

COUTINHO AUMIA ENKA, KOCHA WAKE ATAKA RIPOTI YA DAKTARI ISUBIRIWE Liverpool inaweza kumkosa kiungo wake nyota Philippe Coutinho kwa mechi kadhaa baada ya kuumia kifundo cha mguu, leo. Coutinho aria wa Brazil ameumia wakati wa mechi dhidi ya Sunderland wakati alipogongana na beki Didier N‘Dong, wakati wakiwania mpira. Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema watalazimika kusubiri majibu ya madaktari kujua maumivu yake yakoje na nini kitafuatia. Coutinho ambaye amekuwa tegemeo katika safu ya ushambulizi ya Liverpool, alitolewa nje katika dakika ya 34 baada ya kuumia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni