Jumapili, 27 Novemba 2016

BILA YA LWANDAMINA, ZESCO YABEBA UBINGWA WA KOMBE LA BARCLAYS ZAMBIA Pamoja na kuondokewa na kocha wake mkuu, George Lwandamina, Zesco wamefanikiwa kubeba Kombe la Barclays la Zambia. Linakuwa ni kombe lao la tano baada ya ushindi wa Barclays baada ya kuichapa Zanaco kwa bao 1-0. Ushindi huo kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Zambia ulipatikana baada ya bao la Idriss Mbombo katika dakika ya 71. Mara ya mwisho Zesco ilitwaa kombe hilo mwaka 2014 chino ya Lwandamina ambaye kesho rasmi anaanza kazi ya kuinoa Yanga. Baada ya bao hilo, Mbombo amekuwa mshambuliaji aliyefunga katika michuano tote ya Zambia akiwa na Charity Shield, bao moja,Champions League (5), Super League (9) na Barclays Cup (1).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni