pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumapili, 27 Novemba 2016
Tukio lililofanya Mourinho aondolewe kwenye benchi la ufundi dhidi ya West Ham Kwa mara ya pili msimu huu kocha wa Manchester United Jose Mourinho aliondolewa kwenye benchi la ufundi wakati wa mchezo wa Premier League dhidi ya West Ham. Utovu wa nidhamu kwa waamuzi baada ya Paul Pogba kujirusha, Mourinho alijikuta akishindwa kuzuia hisia zake akiwa eneo lake la kujidai na kuibutua chupa iliyokuwa mbeke yake kwa hasira. Akipewa maelekezo na fourth official, mwamuzi Jon Moss alimwamuru Jose Mourinho kuondoka kwenye eneo la ufundi na aende jukwaani. Rui Faria akaachwa kwenye benchi kumalizia dakika 60+ zilizosalia katika mchezo uliomalizika kwa sare ya 1-1 dhidi ya West Ham.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni