Jumanne, 29 Novemba 2016

Alichouliza mchezaji wa Chapecoense baada ya kunusurika kwenye ajali ya ndege Habari zilizo-trend sana leo kwenye upande wa soka ni kuanuka kwa ndege iliyokuwa imebeba wachezaji wa Chapecoense. Sasa katika watu walionusurika katika ajali hiyo mbaya iliyotokea kwenye mji wa Medellin ni pamoja na beki wa pembeni Alan Ruschel. Mchezaji huyo mwenye miaka 27 kwa sasa yupo Chapecoense kwa mkopo akitokea Internacional. Kwa mujibu wa ripoti, Ruschel alifika hospital akiwa macho huku akizungumza. Inatajwa kwamba alikuwa amevunjika sehemu kadhaa za mwili wake lakini alikuwa na majeraha kichwani pia. Kwa mujibu wa waandishi wa Colombia, ameripoti kwamba, baada ya Ruschel kufikishwa hospital alikuwa na kitu kimoja tu akilini mwake ‘familia yake.’ Mchezaji huyo aliomba mtu amtunzie pete yake ya ndoa huku maswali yake yote hayakuwa juu ya afya yake bali ni kuhusu familia yake. Mkewake aliposikia mumewe amenusurika kifo Mke wa mchezaji huyo anayejulikana kwa jina la Alissen Rushel ali-post ujumbe kwenye mitandao ya kijamii baada ya kupata taarifa kuwa mumewake amenusurika kutoka kwenye ajali hiyo ya ndege. Picha za kutoka snapchat Kabla ya ndege haijaruka, Alan Ruschel alikuwa busy kwenye mitandao ya kijamii. Alipost picha kadhaa kwenye ukurasa wake wa kijamii akionekana yupo ndani ya ndege. Alikua amekaa pamoja na golikipa wa Chapecoense Danilo ambaye anatajwa kuwa ni mchezaji wa pili kunusurika kutoka kwenye ajali hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni