Jumatatu, 28 Novemba 2016

PICHA 5: Lwandamina alivyoongoza mazoezi Yanga kwa mara ya kwanza Kocha George Lwandamina rasmi leo ameanza kazi ya kukinoa kikosi chake cha Yanga kwa mara ya kwanza. Lwandamina raia wa Zambia ameanza kazi kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi Kilwa Road jijini Dar es Salaam. Awali, uongozi wa Yanga ulimficha kocha huyo hadi SALEHJEMBE alipomfichua na kufanya naye mahojiano ya kwanza. Ameanza kazi ikiwa ni mara ya kwanza baada ya likizo ambayo walipewa na aliyekuwa kocha mkuu, Hans van der Pluijm.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni