Jumanne, 29 Novemba 2016

Kiungo wa Zesco atua Yanga Kiungo wa Zesco United Justine Zulu tayari ametua nchini akitokea Zambia kwa ajili ya mazungumzo na uongozi wa klabu ya Yanga. Kwa namna yoyote, hayo ni mapendekezo ya kocha George Lwandamina ambaye tayari ameanza majukumu ya kuifundisha Yanga ambapo jana Jumatatu Novemba 28 alisimamia mazoezi ya klabu hiyo kwa mara ya kwanza akiwa kocha mkuu mpya aliyechukua nafasi ya Hans van Pluijm. Kwa muda mrefu Yanga imekuwa na wachezaji wachache wa eneo la kiungo wa katikati (Thaban Kamusoko, Haruna Niyonzima, Juma Makapu na Mbuyu Twite) ukilinganisha na washindani wao wa ndani Simba na Azam FC ambao wanawachezaji wengi katika idara hiyo. Justine Zulu anamiaka 27 amezaliwa 11 August 1989 Lusaka, Zulu amewahi kuvitumikaia vilabu vya National Assembly, Hapoel Be’er Sheva, Hapoel Bnei Lod, Hapoel Rishon LeZion, Enosis Neon Paralimni, Lamontville Golden Arrows, Kabwe Warriors na ZESCO United. Mwaka 2012 alisaini miaka mitatu kuitumikia klabu ya Lamontville Golden Arrows ya Afrika Kusini. October 2013 alirejea kwenye ligi ya Zambia na kujiunga na Kabwe Warriors, ukiwa ni mkataba wa muda mfupi. Baadae alijiunga na Zesco United kuelekea msimu wa 2014 ambapo ameendelea kuhudumu hadi sasa. Mwaka 2011 alicheza mechi yake ya kwanza akiwa na timu ya taifa ya Zambia. Zulu alikuwa sehemu ya wachezaji walioitwa kwenye kikosi cha taifa kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2012 lakini hakufanikiwa kutajwa kwenye kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 waliotwaa taji hilo mwaka 2012. Wasifu wa Justine Zulu Date of birth11 August 1989 (age 27) Place of birthLusaka, Zambia Height1.82 m (5 ft 11 1⁄2 in) Playing positionMidfielder Club information Current teamZESCO United Senior career* YearsTeamApps(Gls) 2005–2007National Assembly 2007–2009Hapoel Be’er Sheva23(1) 2009–2010 Hapoel Bnei Lod 31 (1) 2010–2012 Hapoel Rishon LeZion 50 (3) 2012 Enosis Neon Paralimni 11 (0) 2012–2013 Lamontville Golden Arrows 4 (0) 2013 Kabwe Warriors 2014– ZESCO United

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni