pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumamosi, 26 Novemba 2016
Leicester yadhihirisha soka kakika 90 Bao la dakika za majeruhi la Islam Slimani limeipa pointi moja Leicester ilipotoka nyuma mara mbili dhidi ya Middlesbrough. Alvaro Negredo alikata ukame wa mabao baada ya kufunga goli lake la kwanza la msimu alipoifungia Boro bao la kuongoza dakika ya 13 kufuatia ya kubadilishana pasi na Gaston Ramirez. Riyad Mahrez aliisawazisha bao dakika ya 34 kwa mkwaju wa penati baada ya Calum Chambers kudaiwa kuunawa mpira kwenye eneo la hatari. Dakika ya 71 Negredo akaweka tena kambani na likiwa ni bao la pili kwa Middlesbrough huku likiwa ni bao lake la pili msimu huu. Dakika za nyongeza (90+4) Slimani aliweka kambani kwa mkwaju wa penati baada ya Wes Morgan kufanyiwa madhambi na Marten de Roon na mwisho wa siku mchezo kumalizika kwa sare ya magoli 2-2.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni