Jumamosi, 26 Novemba 2016

Shinji Kagawa anaelezea future yake ndani ya Borussia Dortmund.Shinji Kagawa amepoteza nafasi yakee kwenye kikosi cha kwanza na kumfanya aanze mara tatu yu kwenye mechi za Bundesliga ndani ya uwanja wa Signal Iduna Park. Kwenye mechi ya UEFA ambapo BVB wameshinda 8-4, Kagawa alitoa assisit na kufunga mara mbili kuchangia ushindi huo. Mchezaji huyu mwenyr miaka 27 anahushishwa sana na kurudi kwenye ligi ya nchini kwao Japan hasa kujiunga na club ya Yokohama F Marinos. Mchezaji huyu wa zamani wa Man United na Cerezo Osaka amekubali kwamba ana wakati mgumu ndani ya Ujerumani kwa miezi michache iliyopita lakini bado anaimani na mazoezi anayofanya yatamrudisha kwenye kikosi cha kwanza. Alivyoulizwa kuhusu kuachana na club hiyo ili apate nafasi ya kucheza Kagawa alijibu,“Nataka kuonyesha kwamba naweza kucheza mechi hapa nitaonyesha kila kitu nilichokua nacho. Nilihitaji kufunga haya magoli na kutoa assist ili niendelee kujiamini. Hii mechi imekua muhimu sana kwangu. Najua nahitaki kufanya mazoezi sana ili niendelee kuwa bora zaidi” Tuendelee kumfatilia Shinji Kagawa kupitia king’amuzi cha Startimes ambapo tutamuona live kwenye ligi ya Bundesliga akionyesha huo uwezo alioahidi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni