Jumatano, 23 Novemba 2016

Tetesi za Drogba kurejea Stamford Bridge Baada ya legend wa Liverpool Steven Gerrard, ikafata zamu ya mkongwe wa Chelsea Frank Lampard. Siku ya Jumatano asubuhi Novemba 23 Didier Drogba ameungana na makamanda hao wa Premier League kutangaza kustaafu kucheza ligi ya MLS ya nchini Marekani. Mshambuliaji huyo raia wa Ivory Coast amemaliza muda wake katika klabu ya Montreal Impact baada ya kuichapa Toronto FC kwenye mchezo wa MLS. Drogba aliwaambia waandishi wa habari kwamba, hatokuwepo ndani ya ligi hiyo msimu ujao. Inaonekana tayari klabu inatambua uamuzi wa Drogba kwasababu mapema tu ilachia video inayoonesha matukio muhimu ya akiwa katika klabu hiyo (Montreal Impact). Akizungumza kuhusu mchezo wa wiki ijayo amesema ni mchezo muhimu ingawa anaweza asiwepo kwenye kikosi. Kila mmoja anajua ulikuwa ni mchezo wangu wa mwisho hapa na hivyo ndivyo ilivyo tuangalie mambo mengine yajayo. Drogba anahusishwa kurejea kwenye klabu ya Chelsea ambapo huenda akapewa majukumu kwenye benchi la ufundi ingawa kwa sasa bado ni tetesi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni