pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Ijumaa, 25 Novemba 2016
AZAM FC YAWAAMBIA KAGERA SUGAR WASAHAU KABISA KUHUSU AME ALI Uongozi wa Azam FC umekata mzizi wa fitina kwa Kagera Sugar ambayo imeonekana kutaka saini ya fowadi wao, Ame Ally ‘Zungu’ ambaye yupo kwa mkopo Simba kuwa kusema suala hilo haliwezekani kwa sasa. Juzikati, Kocha wa Kagera, Mecky Maxime, alijipambanua jinsi anavyotamani kumpata fowadi huyo ambaye licha ya kupelekwa Simba kwa mkopo, bado ameshindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Mcameroon, Joseph Omog. Maxime alisema anashangazwa na Zungu kukosa nafasi kwani ni mmoja wa washambuliaji anaokubali uwezo wao ambapo walikuwa wote Mtibwa Sugar kabla ya kutwaliwa na Azam. Ofisa Mtendaji wa Azam, Saady Kawemba amesema kuwa dili hilo kwa sasa haliwezekani kwani hata Simba yenyewe imeonekana kuvutiwa naye na ataendelea kuwepo Msimbazi mpaka mwisho wa msimu. “Kagera hawajaja rasmi na itakuwa ngumu maana bado hatuwezi kumtoa aliko kwa sasa ili tu aende Kagera,” alisema Kawemba.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni