Ijumaa, 22 Julai 2016

BBC Dira TV: Sam Allardyce amethibitishwa kuwa meneja wa timu ya taifa ya England. Allardyce, 61, amesaini mkataba wa awali wa miaka miwili baada ya makubaliano kufikiwa na klabu yake ya Sunderland alioisaidia msimu uliopita isishuke daraja. Anachukua nafasi ya Roy Hodgson, ambaye alijiuzulu baada ya England kutolewa kwenye michuano ya Euro 2016 na Iceland. Mchezo wa kwanza wa Allardyce utakuwa wa kirafiki Septemba mosi dhidi ya timu ambayo haijatajwa bado. Je nini maoni yako kuhusu uteuzi huu? Je mameneja wazawa wana ushawishi zaidi katika timu za taifa kuliko mameneja wa kigeni? @mompondazy

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni