Jumatano, 27 Julai 2016

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE 27.07.2016 Manchester City wana matumaini ya kumsajili winga wa Schalke Leroy Sane, 20, pamoja na mshambuliaji wa Palmeiras Gabriel Jesus kwa zaidi ya pauni milioni 60 (Daily Telegraph), wakala Mino Raiola amefuta vipimo vya afya vya Paul Pogga, 23, kwa ajili ya kujiunga na Manchester United vilivyokuwa vifanyike mjini Miami (AS), Lyon wamewaambia Arsenal na West Ham kuwa watahitaji kulipa pauni milioni 40 pamoja na marupurupu ili kumsajili Alexandre Lacazette, 25 (Daily Mirror), dau la pauni milioni 33.5 la Liverpool la kumtaka kiungo Joao Mario, 23 limekataliwa na Sporting Lisbon (Sun), Borussia Dortmund wametupilia mbali tetesi kuwa mshambuliaji wake Pierre-Emerick Aubameyang, 27, atajiunga na Manchester City (Bild), Chelsea na Everton watapambana kupata saini ya kiungo wa Sporting Lisbon William Carvalho, 24 (Daily Mirror), Chelsea wameionya Juventus kuwa hawana mpango wa kumuuza kiungo mkabaji Nemanja Matic, 27 (Daily Telegraph), kiungo Blaise Matuidi, 29, anayesakwa na Manchester United ameambiwa anaruhusiwa kuondoka PSG (L'Equipe), Arsenal na Tottenham zinamsaka mshambuliaji wa Toulouse Wissam Ben Yedder, 25, aliyefunga mabao 17 msimu uliopita nchini Ufaransa (Canal+) mshambuliaji Marco Arnautovic, 27, hataki kuondoka Stoke City na kwenda Everton, na atasaini mkataba mpya (Daily Mail), meneja wa Man City Pep Guardiola amekubali mkataba wa kumsajili mshambuliaji wa Atletico Nacional, Marlos Moreno, 19, kwa pauni milioni 8 (Guardian), dau la Napoli kumtaka mshambuliaji wa Ajax Arkadiusz Milik, 22, limekubaliwa, ili kuziba pengo la Gonzalo Higuain, 28 (Gazzetta dello Sport), meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane amemuambia winga Jese anaweza kuondoka (Marca), Arsenal na Liverpool wanataka kumsajili Jese, 23 (Sun), Everton wameweza kufikia kigezo cha uhamisho cha pauni milioni 7.1 na wana matumaini ya kumsajili Idrissa Gueye, 26, wa Aston Villa (Birmingham Mail), mabingwa wa Uturuki, Besitkas wanataka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli, 25, kwa mkopo (Gazzetta dello Sport), Leicester wameongeza dau lao la kumtaka mshambuliaji kutoka Poland Bartosz Kapustka, 19, kwa kutoa pauni milioni 5.2 kwa klabu yake ya Cracovia (The Times). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni