Jumatatu, 25 Julai 2016

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATATU 25.07.2016 Manchester United wamewasilisha dau jingine la pauni milioni 92 kumtaka kiungo Paul Pogba, 23, lakini Juventus wanataka euro milioni 10 zaidi (The Guardian), mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, 27, bado anasakwa na klabu yake ya zamani Atletico Madrid huku Chelsea wakimtaka Alvaro Morata, 23, wa Real Madrid kuziba nafasi yake (Daily Mirror), Juventus wanajiandaa kumchukua kiungo wa Chelsea Nemanja Matic, 27, kuziba nafasi ya Paul Pogba ambaye huenda akajiunga na Manchester United (Daily Mail), Liverpool watapanda dau la mwisho la takriban pauni milioni 8 kumtaka beki Ben Chilwell, 19, kutoka Leicester (The Sun), Stoke wanajiandaa kutoa dau la kuvunja rekodi ya klabu hiyo kumtaka mshambuliaji wa West Brom, Saido Berahino, 22, baada ya pauni milioni 20 kukataliwa (Stoke Sentinel), Raphael Varane, 23, amesema hajiandai kuungana na meneja wake wa zamani Jose Mourinho, Manchester United, na kusisitiza kuwa atasalia Real Madrid msimu huu (Marca), Georgio Wijnaldum, 25, amesema meneja Jurgen Klopp alimshawishi kwenda Liverpool badala ya Tottenham au Everton (Liverpool Echo), meneja wa Bournemouth Eddie Howe anataka kununua beki mpya wa kati msimu huu (The Guardian), meneja mpya wa Sunderland David Moyes atawasiliana na Manchester United kuona kama ataweza kumchukua Adnaj Januzaj, 21, kwa mkopo (Daily Mail), Stoke City wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa Liverpool Joe Allen, 26, baada ya Swansea kushindwa kupanda dau (The Sun), Hull City watazungumza na meneja wa zamani wa Wigan, Roberto Martinez, 42, kuziba nafasi ya Steve Bruce (Daily Express). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni