Ijumaa, 22 Julai 2016

Liverpool wamekubali kulipa pauni milioni 25 katika mkataba wa kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi na Newcastle, Georginio Wijnaldum. Kiungo huyo, 25, ambaye alikuwa na miaka minne iliyosalia kwenye mkataba wake na Newcastle, atafanya vipimo vya afya Liverpool siku ya Ijumaa. Wijnaldum alijiunga na Newcastle kwa pauni milioni 14.5 akitokea PSV mwaka 2015, na kucheza mechi zote 38 za Newcastle msimu uliopita na kupachika mabao 11. Anakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa na Liverpool mpaka sasa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni