pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Ijumaa, 29 Julai 2016
TETESI ZA SOKA ULAYA IJUMAA 29.07.2016 Kiungo wa Manchester United na Ujerumani Bastian Schweinsteiger, 31, huenda akawa mchezaji wa kwanza kuondolewa katika kikosi cha Jose Mourinho Old Trafford (Daily Express), Mourinho anapanga kuondoa wachezaji tisa huku akijiandaa kumkaribisha kiungo Paul Pogba, 23 (sun), iwapo United watashindwa kumsajili Pogba, watamfuatilia Blaise Matuidi, 29, kutoka PSG (Manchester Evening News), mshambuliaji kutoka Colombia Marlos Moreno, 19, anajiandaa kujiunga na Manchester City baada ya wakala wake kuthibitisha uhamisho wa pauni milioni 8 kutoka Atletico Nacional (Daily Mail), Real Madrid wanapanga kumchukua kiungo wa PSG Marco Verratti, 23, baada ya kushindwa kumsajili Paul Pogba (AS), meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anafikiria kumfanya James Milner, 30, kama beki wa kushoto baada ya kukata tamaa ya kumsajili Ben Chilwell, 19, kutoka Leicester (Daily Telegraph), Arsenal wamesema hawako tayari kutumia zaidi ya pauni milioni 33.7 kumsajili Alexandre Lacazette, 25 kutoka Lyon (Squawka), beki wa West Ham Reece Oxford, 17, mwenye thamani ya pauni milioni 18, anataka kuhakikishiwa kuanza katika kikosi cha kwanza kufuatia kusakwa na Manchester United (Evening Standard), West Ham wanakaribia kumsajili mshambuliaji wa Swansea Andre Ayew, 26, kwa pauni milioni 16 (Sun), Arsenal wanazungumza na beki wa Ujerumani Shkodran Mustafi, 24, anayechezea Valencia (Sky Sports), Peter Crouch, 35, amehusishwa na kuhamia Swansea (South Wales Evening Post), Newcastle United hawajapata dau lolote la kumtaka Ayoze Perez, 23, kutoka Barcelona, licha ya taarifa kusema dau la pauni milioni 15 limetolewa (Chronicle). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni