pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumapili, 31 Julai 2016
HAMILTON TENAAAA Dereva wa timu ya Mercedes Muingdreza Lewis Hamilton leo amefanikiwa kushinda Germany Grand Prix na nafasi ya pili ikikamatwa na Daniel Ricciardo wa Red Bull na namba 3 akishika Max Verstappen na yeye kutoka Red Bull. Hamilton huu ni ushindi wake wa 4 mfululizo na kuendelea kushika usikani katika msimamo wa Frmula 1 msimu huu akiwa na pointi 217 huku namba 2 ikikamatwa na Mjerumani Nico Rosberg ambaye leo amekuwa wa 4 na hivyo kuwa na pointi 198.
Jumamosi, 30 Julai 2016
TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAMOSI 30.07.2016 Arsenal wataongeza dau na kufikia pauni milioni 35 kumtaka mshambuliaji wa Lyon Alexandre Lacazette, 25, baada ya dau la awali la pauni milioni 29.3 kukataliwa na klabu hiyo ya Ufaransa (Daily Telegraph), Arsenal pia wanataka kumsajili beki wa Torino, Bruno Peres, 26, huku klabu hiyo ikitaka pauni milioni 16.9 (Gazzetta World), Arsenal vilevile wanazungumza na Valencia kutaka kumsajili beki mjerumani Shkodran Mustafi, 24, ambaye ana kipengele cha uhamisho chenye thamani ya pauni milioni 42.1 kwenye mkataba wake (Sky Sports), dau la Chelsea la pauni milioni 57, kumtaka mshambuliaji wa Everton, Romelu Lukaku, 23, limekatakiwa, huku klabu hiyo ikitaka pauni milioni 75 (Daily Mirror), kiungo wa Tottenham Christian Eriksen, 24, amekataa kusaini mkataba mpya, kwa sababu anataka mshahara wake wa pauni 30,000 kwa wiki kuongezwa (Evening Standard), Swansea wamepanda dau la kumtaka mshambuliaji wa Sevilla, Fernando Llorente, 31, baada ya Bafetimbi Gomis kwenda Marseille kwa mkopo hadi mwisho wa msimu, na hivyo hawana mshambuliaji rasmi kwa sasa (Daily Mail), Leicester City wako tayari kumpa mkataba wa pauni 100,000 kwa wiki kiungo Riyad Mahrez, 25 ambaye inaaminika anasakwa na Arsenal (Daily Express), Manchester United wanakaribia kumsajili beki wa kulia kutoka Brazil anayechezea Monaco, Fabinho, 22 (Globoesporte), Aston Villa wanaonekana watamuuza Idrissa Gana, 26, huku Everton wakiwa tayari kukamilisha usajili wa pauni milioni 7.1 kumchukua mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal (Daily Mirror), beki wa Manchester United Cameron Borthwick-Jackson, 19, huenda akaondoka Old Trafford na kwenda kucheza kwingineko kwa mkopo (Manchester Evening News), Everton hawajapanda dau lolote kumtaka beki wa Sunderland Lamine Kone, 27, licha ya taarifa kuzagaa kuwa dau la pauni milioni 14 limetolewa (Sunderland Echo), Everton wanataka kumsajili beki wa Swansea Ashley Williams, 31, ambaye huenda akagharimu pauni milioni 10 (Daily Mirror), Manchester City wanasita kutoa pauni milioni 50 kumsajili beki wa kati wa Everton John Stones, 22, wakitaka kutoa takriban pauni milioni 40 (Guardian), mshambuliaji wa West Brom Saido Berahino, 22, yuko tayari kubakia katika klabu hiyo hadi mkataba wake utakapomalizika msimu ujao na aondoke kama mchezaji huru (ESPN), Galatasaray wanataka kumsajili beki wa Manchester City Jason Denayer, 21, na pia kiungo wa Liverpool Lucas Leiva, 29 (Daily Mirror), Manchester City watathibitisha kuwa Sergio Aguero, 28, atasaini mkataba mpya kabla ya kuanza kwa msimu (Daily Mail). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.
Ijumaa, 29 Julai 2016
TETESI ZA SOKA ULAYA IJUMAA 29.07.2016 Kiungo wa Manchester United na Ujerumani Bastian Schweinsteiger, 31, huenda akawa mchezaji wa kwanza kuondolewa katika kikosi cha Jose Mourinho Old Trafford (Daily Express), Mourinho anapanga kuondoa wachezaji tisa huku akijiandaa kumkaribisha kiungo Paul Pogba, 23 (sun), iwapo United watashindwa kumsajili Pogba, watamfuatilia Blaise Matuidi, 29, kutoka PSG (Manchester Evening News), mshambuliaji kutoka Colombia Marlos Moreno, 19, anajiandaa kujiunga na Manchester City baada ya wakala wake kuthibitisha uhamisho wa pauni milioni 8 kutoka Atletico Nacional (Daily Mail), Real Madrid wanapanga kumchukua kiungo wa PSG Marco Verratti, 23, baada ya kushindwa kumsajili Paul Pogba (AS), meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anafikiria kumfanya James Milner, 30, kama beki wa kushoto baada ya kukata tamaa ya kumsajili Ben Chilwell, 19, kutoka Leicester (Daily Telegraph), Arsenal wamesema hawako tayari kutumia zaidi ya pauni milioni 33.7 kumsajili Alexandre Lacazette, 25 kutoka Lyon (Squawka), beki wa West Ham Reece Oxford, 17, mwenye thamani ya pauni milioni 18, anataka kuhakikishiwa kuanza katika kikosi cha kwanza kufuatia kusakwa na Manchester United (Evening Standard), West Ham wanakaribia kumsajili mshambuliaji wa Swansea Andre Ayew, 26, kwa pauni milioni 16 (Sun), Arsenal wanazungumza na beki wa Ujerumani Shkodran Mustafi, 24, anayechezea Valencia (Sky Sports), Peter Crouch, 35, amehusishwa na kuhamia Swansea (South Wales Evening Post), Newcastle United hawajapata dau lolote la kumtaka Ayoze Perez, 23, kutoka Barcelona, licha ya taarifa kusema dau la pauni milioni 15 limetolewa (Chronicle). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa
Alhamisi, 28 Julai 2016
TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI 28.07.2016 Kiungo wa Ufaransa Paul Pogba, 23, anakaribia kukamilisha uhamisho wake kwenda Manchester United kwa usajili unaovunja rekodi ya dunia wa pauni milioni 112, huku chanzo ndani ya Juventus kikisema mkataba tayari umekamilika (Sun), Manchester United imempa Pogba pauni milioni 100 na wana matumaini ya kukamilisha usajili wake katika saa 48 zijazo (Guardian), Real Madrid pia wamehusishwa na kumsajili Pogba, huku kocha Zinedine Zidane akisema "kila mtu" anataka kumsajili kiungo huyo kabla ya dirisha la usajili kufungwa (Sky Sports), hata hivyo Real Madrid wanasema hawawezi kumgombea Pogba na wapo tayari kumsajili kiungo Moussa Sissoko, 26, ambaye Newcastle inataka pauni milioni 30 (Daily Telegraph), beki wa Everton, John Stones, 22, anajiandaa kujiunga na Manchester City kwa pauni milioni 50 na mkataba huo unaweza kukamilika wiki hii (Daily Mail), iwapo City watashindwa kumsajili Stones, Pep Guardiola wanataka kumchukua Leonardo Bonucci, 29, kutoka Juventus (Daily Mirror), Everton wameanza kujitayarisha kuziba nafasi ya Stones kwa kutaka kumsajili Lamine Kone, 27, wa Sunderland kwa pauni milioni 14 (Sun), Arsenal wamezungumza na wakala wa beki Mjerumani Shkodran Mustafi, 24, anayechezea Valencia (Twitter ya Emanuele Giulianelli), beki wa kati wa Manchester City Eliaquim Mangala, 25, huenda akaziba nafasi ya Mustafi akiondoka Valencia na iwapo City watamchukua Stones (Sun), Chelsea wametoa dau la pauni milioni 38 kumtaka beki Kalidou Koulibaly, 25, kutoka Napoli (Sky Italy), Stoke bado wanamtaka mshambuliaji wa West Brom, Saido Berahino, 22 (Talksport), Liverpool huenda wakazidiwa kete na Wolves katika kumsajili kiungo wa Benfica Anderson Talisca, 22 kwa pauni milioni 20 (A Bola), Southampton wanataka kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Cristian Tello, 24, kwa pauni milioni 10 na pia kiungo wa Malaga, Recio, 24, kwa pauni milioni 5 (Sun), Barcelona wanamtaka mshambuliaji wa Newcastle Ayoze Perez, 23, kuwa kama mshambuliaji wa akiba kuwasaidia Messi, Neymar na Suarez (IBTimes), mshambuliaji wa Leicester Leonardo Ulloa, 30, amemuambia meneja wake Claudio Ranieri kuwa anataka kuondoka na kujiunga na Swansea kwa pauni milioni 10 (Sun), Swansea pia wanataka kumsajili Fernando Llorente, 30, kwa mkopo kutoka Sevilla (IUSport), kiungo wa Leicester Andy King, 27, atasaini mkataba mpya kusalia King Power hadi 2020 (ESPN), meneja mpya wa Sunderland amekataa kumsajili beki wa Aston Villa, Micah Richards, 28, kwa pauni milioni 5 (Northern Echo). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.
Jumatano, 27 Julai 2016
TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE 27.07.2016 Manchester City wana matumaini ya kumsajili winga wa Schalke Leroy Sane, 20, pamoja na mshambuliaji wa Palmeiras Gabriel Jesus kwa zaidi ya pauni milioni 60 (Daily Telegraph), wakala Mino Raiola amefuta vipimo vya afya vya Paul Pogga, 23, kwa ajili ya kujiunga na Manchester United vilivyokuwa vifanyike mjini Miami (AS), Lyon wamewaambia Arsenal na West Ham kuwa watahitaji kulipa pauni milioni 40 pamoja na marupurupu ili kumsajili Alexandre Lacazette, 25 (Daily Mirror), dau la pauni milioni 33.5 la Liverpool la kumtaka kiungo Joao Mario, 23 limekataliwa na Sporting Lisbon (Sun), Borussia Dortmund wametupilia mbali tetesi kuwa mshambuliaji wake Pierre-Emerick Aubameyang, 27, atajiunga na Manchester City (Bild), Chelsea na Everton watapambana kupata saini ya kiungo wa Sporting Lisbon William Carvalho, 24 (Daily Mirror), Chelsea wameionya Juventus kuwa hawana mpango wa kumuuza kiungo mkabaji Nemanja Matic, 27 (Daily Telegraph), kiungo Blaise Matuidi, 29, anayesakwa na Manchester United ameambiwa anaruhusiwa kuondoka PSG (L'Equipe), Arsenal na Tottenham zinamsaka mshambuliaji wa Toulouse Wissam Ben Yedder, 25, aliyefunga mabao 17 msimu uliopita nchini Ufaransa (Canal+) mshambuliaji Marco Arnautovic, 27, hataki kuondoka Stoke City na kwenda Everton, na atasaini mkataba mpya (Daily Mail), meneja wa Man City Pep Guardiola amekubali mkataba wa kumsajili mshambuliaji wa Atletico Nacional, Marlos Moreno, 19, kwa pauni milioni 8 (Guardian), dau la Napoli kumtaka mshambuliaji wa Ajax Arkadiusz Milik, 22, limekubaliwa, ili kuziba pengo la Gonzalo Higuain, 28 (Gazzetta dello Sport), meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane amemuambia winga Jese anaweza kuondoka (Marca), Arsenal na Liverpool wanataka kumsajili Jese, 23 (Sun), Everton wameweza kufikia kigezo cha uhamisho cha pauni milioni 7.1 na wana matumaini ya kumsajili Idrissa Gueye, 26, wa Aston Villa (Birmingham Mail), mabingwa wa Uturuki, Besitkas wanataka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli, 25, kwa mkopo (Gazzetta dello Sport), Leicester wameongeza dau lao la kumtaka mshambuliaji kutoka Poland Bartosz Kapustka, 19, kwa kutoa pauni milioni 5.2 kwa klabu yake ya Cracovia (The Times). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.
Jumanne, 26 Julai 2016
Jumatatu, 25 Julai 2016
TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATATU 25.07.2016 Manchester United wamewasilisha dau jingine la pauni milioni 92 kumtaka kiungo Paul Pogba, 23, lakini Juventus wanataka euro milioni 10 zaidi (The Guardian), mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, 27, bado anasakwa na klabu yake ya zamani Atletico Madrid huku Chelsea wakimtaka Alvaro Morata, 23, wa Real Madrid kuziba nafasi yake (Daily Mirror), Juventus wanajiandaa kumchukua kiungo wa Chelsea Nemanja Matic, 27, kuziba nafasi ya Paul Pogba ambaye huenda akajiunga na Manchester United (Daily Mail), Liverpool watapanda dau la mwisho la takriban pauni milioni 8 kumtaka beki Ben Chilwell, 19, kutoka Leicester (The Sun), Stoke wanajiandaa kutoa dau la kuvunja rekodi ya klabu hiyo kumtaka mshambuliaji wa West Brom, Saido Berahino, 22, baada ya pauni milioni 20 kukataliwa (Stoke Sentinel), Raphael Varane, 23, amesema hajiandai kuungana na meneja wake wa zamani Jose Mourinho, Manchester United, na kusisitiza kuwa atasalia Real Madrid msimu huu (Marca), Georgio Wijnaldum, 25, amesema meneja Jurgen Klopp alimshawishi kwenda Liverpool badala ya Tottenham au Everton (Liverpool Echo), meneja wa Bournemouth Eddie Howe anataka kununua beki mpya wa kati msimu huu (The Guardian), meneja mpya wa Sunderland David Moyes atawasiliana na Manchester United kuona kama ataweza kumchukua Adnaj Januzaj, 21, kwa mkopo (Daily Mail), Stoke City wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa Liverpool Joe Allen, 26, baada ya Swansea kushindwa kupanda dau (The Sun), Hull City watazungumza na meneja wa zamani wa Wigan, Roberto Martinez, 42, kuziba nafasi ya Steve Bruce (Daily Express). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.
Jumapili, 24 Julai 2016
Jumamosi, 23 Julai 2016
David Moyes ameteuliwa na Sunderland kuwa meneja wa klabu hiyo kwa mkataba wa miaka minne. Meneja huyo wa zamani wa Everton na Manchester United, 53, anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Sam Allardyce ambaye amepewa kazi ya kuwa meneja wa timu ya taifa ya England. “Nimechukua kazi katika klabu kubwa Uingereza, na kwa kuungwa mkono kwa kiasi kikubwa, nina hamu ya kufanya kazi tena katika Ligi Kuu ya England,” amesema Moyes. Meneja huyo amekuwa bila kazi tangu alipofukuzwa na Real Sociedad mwezi Novemba mwaka jana. Allardyce alithibitishwa kuwa meenja wa England siku ya Ijumaa @mompondazy
TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAMOSI 23.07.2016 Meneja mpya wa Chelsea Antonio Conte amemuambia mmiliki wa timu Roman Abramovic kuwa anahitaji kusajili wachezaji wengine watano ili Chelsea irejee katika ubora wake (Daily Mirror), Manchester United wanafikiria kutoa dau la pauni milioni 54 kumtaka mshambuliaji wa Real Madrid James Rodriguez, 25 (El Confidencial), Manchester City watarejea tena Everton na kutoa dau la zaidi ya pauni milioni 50 kumtaka beki John Stones, 22 (Daily Mirror), meneja wa Tottenham, Mauricio Pochettino amewaacha Nabil Bentale, 21, Clinton N’Jie, 22, Federico Fazio, 29, na Alex Pritchard, 23, katika kikosi kilichokwenda Australia, na huenda wakauzwa (The Sun), kiungo wa Liverpool, Lucas Leiva, 29, anasakwa na Galatasaray ya Uturuki (Daily Mail), meneja wa Manchester City Pep Guardiola amekatishwa tamaa ya kumsajili kiungo wa Real Madrid, Toni Kroos, 24, kwa sababu ya mshahara wa pauni 240,000 kwa wiki wa mchezaji huyo (The Sun), Ryan Giggs na Roy Keane wanatajwa kuziba nafasi ya Steve Bruce aliyeondoka Hull City (Daily Express), meneja wa Leicester Claudio Ranieri amesema beki wa kushoto Ben Chilwell, 19, atasaini mkataba mpya, kufuatia tetesi kuwa Liverpool wamepanda dau la pauni milioni 7 (Leicester Mercury), mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli, 25, anahitaji ”nafasi nzuri” ili kurejea katika ubora wake, amesema wakala wake Mino Raiola (Liverpool Echo), Everton wanajiandaa kutoa pauni milioni 25 kumtaka kiungo wa Swansea Gylfi Sigurdsson, 26 (Daily Express), West Brom wametoa dau la pauni milioni 7 kumtaka beki wa Brighton Lewis Dunk, 24 (Daily Mirror), mshambuliaji wa Arsenal amemshawishi meneja Arsene Wenger kumsajili kiungo wa Barcelona Arda Turan, 29 (The Sun), Arsenal pia huenda wakakasirisha mashabiki wao tena baada ya kusema wasitarajie usajili wowote wa bei ghali msimu huu (The Times). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa@mompondazy
Ijumaa, 22 Julai 2016
BBC Dira TV: Sam Allardyce amethibitishwa kuwa meneja wa timu ya taifa ya England. Allardyce, 61, amesaini mkataba wa awali wa miaka miwili baada ya makubaliano kufikiwa na klabu yake ya Sunderland alioisaidia msimu uliopita isishuke daraja. Anachukua nafasi ya Roy Hodgson, ambaye alijiuzulu baada ya England kutolewa kwenye michuano ya Euro 2016 na Iceland. Mchezo wa kwanza wa Allardyce utakuwa wa kirafiki Septemba mosi dhidi ya timu ambayo haijatajwa bado. Je nini maoni yako kuhusu uteuzi huu? Je mameneja wazawa wana ushawishi zaidi katika timu za taifa kuliko mameneja wa kigeni? @mompondazy
TETESI ZA SOKA ULAYA IJUMAA 22.07.2016 Chelsea wanafikiria kutoa dau la takriban pauni milioni 50 kumsajili tena Romelu Lukaku, 23, kutoka Everton. Everton wanasema Lukaku ana thamani ya pauni milioni 65 (Liverpool Echo), Manchester City wapo katika nafasi nzuri ya kumsajili mshambuliaji wa Palmeiras, Gabriel Jesus, 19, ambaye pia anasakwa na Barcelona, Real Madrid na Manchester United (Manchester Evening News), Tottenham watampa mkataba mpya wa miaka mitano kiungo Eric Dier, 22, na kumpa mshahara wa pauni 70,000 kwa wiki (Telegraph), iwapo kiungo wa Juventus atakwenda Manchester United, wakala wake huenda akalipwa pauni milioni 20 (Daily Mail), wakala mwenyewe Raiola anakanusha kuwa mkataba wa Pogba tayari umekamilika (The Sun), Chelsea wameambiwa walipe pauni milioni 67 kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid, Alvaro Morata, 23 (Daily Mirror), matumaini ya West Ham ya kumpata Mario Gomez, 31, yameongezeka baada ya mshambuliaji huyo kusema anaondoka Besitkas (daily Express), Chelsea watatoa pauni milioni 41.61 kumsajili Edinson Cavani (le 10Sport.com). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.
THE SPORTS CAMPUS FRIDAY, 22 july 2016
User Rating: / 0 PoorBest England and Manchester United legend David Beckham believes that the arrival of big-name coaches in the English Premier League, especially Jose Mourinho and Pep Guardiola in Manchester, will make the forthcoming season more exciting, unpredictable and something which the football fans will surely enjoy watching. The former Real Madrid star added that after the battles between Alex Ferguson, Arsene Wenger and Kevin Keegan, the new arrival of United coach Mourinho, Man City’s Guardiola, Chelsea’s Antonio Conte will add a new flavour to the league. “What I love about this group of managers is the character of them. You have obviously had this over the years with Sir Alex Ferguson and Arsene Wenger and their battles together and Kevin Keegan and things like that,” Beckham was quoted as saying by Sky Sports on Friday. "But when you talk about Pep, Jurgen Klopp at Liverpool, Antonio Conte - who I love, I love his mannerisms, the way he is on the sidelines and he shows so much passion - obviously with Jose in the mix and being at a club like Manchester United, which for me is the biggest club in the world, it is going to be such an exciting season off the pitch, let alone on the pitch," he added. "So it is going to be one that people are going to enjoy watching.” The 41-year-old also praised Klopp for bringing change in the Liverpool side. “It makes it unpredictable, but with Klopp going in at Liverpool, you could see the change. And when he first went in, I started to think, 'This could be worrying as a Man United fan to see Liverpool coming back to being up there again with the big teams'," he said. “But Jose going to United and Conte going to Chelsea and Pep - who I love, I have been a big fan of his for so many years, both on the pitch and off the pitch, he does so much for a team - it (season) will be unpredictable. "But I do think it will be one of those teams who will be champions at the end of the year.” Beckham also lauded United’s decision to bring in Portuguese tactician Mourinho, commenting it as a great move. “I fully expect it to work. With Jose leaving Chelsea and now coming back into the Premier League with United, for me it is a great move. I had huge respect for (previous United coach) Louis Van Gaal, but it did not work out the way people expected it to. But I think at the end of the day, now it is a new start for United. “We have had a couple over the last three or four years, which is not the Manchester United style, who are used to a manager like Alex Ferguson being in there for so many years.” The former England skipper also heaped praise on reigning EPL champions Leicester City, saying that the Claudio Ranieri-managed side deserved to be champions. “Full credit to Ranieri and the players, they stuck together and it has really showed how the unity of a team can take you so far. But obviously they have a lot of talent as well, so it is not just about the togetherness of a team like Leicester, they actually play well together, have a lot of talented players in their team, so they deserved it," the six-time EPL winner said. “But of course, Leicester City champions, considering where they were the season before, it was a shock, but they deserved it,” Beckham signed off. Tags: arsenal chelsea liverpool manchester united @mompondazy.blog.sport. com