Ijumaa, 10 Machi 2017

AZAM FC WAWAOMBA SIMBA WAKAWASHANGILIE YANGA UWANJA WA TAIFA Uongozi wa Azam FC umewaambia wapenzi na mashabiki wa Simba na timu nyingine, waungane kwa pamoja kuishabikia Yanga, kesho Jumamosi itakapocheza dhidi ya Zanaco ya Zambia. Kauli hiyo imetolewa na Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd huku akisisitiza kwamba kufanya hivyo ni uzalendo ambao unatakiwa kuanzia sasa na kuendelea. Yanga itacheza dhidi ya Zanaco katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ambapo mshindi atacheza hatua ya makundi ya michuano hiyo. Upande mwingine, Azam FC yenyewe itacheza dhidi ya Mbabane Swallows ya Swaziland kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar, ukiwa ni mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, keshokutwa Jumapili. “Kwa sasa lazima tukubali tu kwamba Yanga na Azam ndiyo wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa, hivyo litakuwa jambo la busara kwa mashabiki wote kuweka itikadi zetu pembeni na kuuungana pamoja kuhakikisha timu hizi zinafika mbali. “Nawaomba tu mashabiki wote, wa Azam, Simba na timu nyingine Jumamosi tukaishangilie Yanga pale Taifa, kisha Jumapili, tuungane tena kwenda Azam Complex kuishangilia Azam,” alisema Idd.

MAOFISA WA TFF WASHINDA SAKATA LA RUSHWA MAHAKAMA YA KISUTU Maofisa wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wameshinda kesi yao ya tuhuma za rushwa. Juma Matandika ambaye ni Msaidizi wa Rais wa TFF Jamal Malinzi, na Martin Chacha aliyekuwa mkurugenzi wao mashindano wa TFF. walikua wananashtumiwa kuomba rushwa ya milioni 25 kwa viongozi wa timu ya Geita Gold Sports ameachiwa huru Leo Sauti ziliolewa kuwa ni zao, zilisikika zikieleza mipango ya kuisaidia Geita Gold Sports na ilitakiwa fedha kwa ajili pia ya kuwapa viongozi wengine. Ingawa wadau wengi wanaojua sauti zao waliamini ni wao kabisa, lakini Mahakama ya Mkazi Kisutu imetupilia mbali ushahidi wa sauti uliowasilishwa mahakamani hapo.

Jumanne, 14 Februari 2017

ARSENAL ILIVYOIFUATA BAYERN NA KUMBUKUMBU YA KIPIGO CHA MABAO 5-1 Arsenal leo ina kibarua cha Ligi ya Mabingwa Ulaya itakapowavaa Bayern Munich ambao mara ya mwisho waliwatwanga kwa mabao 5-1. Tayari Arsenal wameondoka London na kutua salama jijini Munich, Ujerumani tayari kwa mchezo huo. Je, wauweza mzigo huo wa Kijerumani?

KAMA ULIFIKIRI SIMBA WAMEITANGULIZA YANGA, WANACHOWAZA NI KINGINE KABISAAAA... Wakati homa ya pambano la watani wa jadi, Simba na Yanga ikizidi kupanda taratibu, Kocha Msaidizi wa Simba, Mganda, Jackson Mayanja, ametamka kuwa hawana hofu hata kidogo na wapinzani wao hao huku wakiwaza mchezo wao unaofuata dhidi ya African Lyon. Vinara hao wa ligi watawavaa wapinzani wao wakuu Yanga kwenye mechi ya ligi itakayopigwa Februari 25, mwaka huu ambapo pambano hilo linatarajiwa kuwa na ushindani kutokana na tofauti ya pointi baina ya timu hizo. Mayanja amesema hawawezi kuwafikiria Yanga kutokana na mchezo wao kuwa mbali na kilichopo kwenye fikra zao ni kuangalia namna ya kulipa kisasi kwa Lyon kwenye mechi ya Kombe la FA (Shirikisho), Alhamisi ijayo. “Yanga hatuna wasiwasi nao kwa sababu mechi yao ipo mbali lakini hata ikija tutacheza kwa uwezo wetu kuhakikisha tunapata matokeo mbele yao na tunaamini tunaweza kufanya hivyo. “Lakini sasa tunaangalia namna ya kuwafunga Lyon kwenye mechi yetu inayofuata,” alisema Mayanja.

HIKI NDICHO ALICHOVUNJIKA JESUS WA MANCHESTER CITY Mshambuliaji Gabriel Jesus wa Manchester City amevunjika mfupa wa tano wa mguu maarufu kama metatarsal. Jesus ambaye alionekana ni mkombozi wa Man City katika ushambulizi alivunjika katika dakika ya 14 ya mchezo dhidi ya Bournemouth ambao City walishinda kwa mabao 2-0. Lakini tayari amepatiwa matibabu na na inaonekana maendeleo ni mazuri. TAKWIMU ZAKE PREMIER LEAGUE Mechi 4 Nafasi alizotengeneza 4 Mashuti yaliolenga 4 Mabao aliyofunga 3 Pasi za mabao 1

DI MARIA ATUPIA MBILI PSG IKIITULIZA BARCELONA KWA 'LAINI' YA 4G PSG imeonyesha inaweza baada ya kuitwanga Barcelona kwa mabao 4-0 katika mechi ya kwanza ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mbaingwa Ulaya. Barcelona ikiwa ugenini jijini Paris imeshindwa kuonyesha cheche licha ya kuongozwa na nyota wake Lionel Messi na Neymar na kujikuta ikipokea kipigo hicho cha kondoo mchovu. Angelo Di Maria ametumbukia nyavuni mara mbili huku Endson Cavani aliyetimiza miaka 30 jana akifunga moja na Julian Draxler akifunga moja. Mechi nyingine Benfica imeifunga Borussia Dortmund kwa bao 1-0.

YANGA WAPOKELEWA UWANJA WA NDEGE KWA MBWEMBWE ILE MBAYA Mashabiki wa Yanga wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kuipokea timu yao ambayo imewasili leo ikitokea Comoro ambako iliitwanga Ngaya kwa mabao 5-1 katika mechi ya kwanza ya Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika.

Jumapili, 12 Februari 2017

LIVE KUTOKA COMORO: NGAYA 1 VS 5 YANGA (FULL TIME) MPIRA UMEKISHAAAA Dk 89, Yanga wanaendelea kushambulia kwa kasi, Chirwa anaingia lakini Mohamed Zahir anamzuia hapa Dk 88, Makapu anafanya kazi ya ziada kuukoa mpira kutoka kwa Said aliyekuwa ameingia vizuri Dk 87, Zulu tena, anajaribu shuti la mbali na mpira unaokolewa na mabeki wa Ngaya Dk 84 Yanga wanaingia vizuri, pasi ya Kamusoko, Chirwa anajaribu inawababatiza mabeki wanaokoa Dk 80, Ngaya wanaingia tena kwenye lango la Yanga lakini Dida anadaka na mwamuzi anasema ni faulo. Juma Abdul anaonekana kuumizwa, anatibiwa hapa SUB Dk 78 anaingia Said Juma Makapu kuchukua nafasi ya Simon MSuva. Hii inaonekana Lwandamina ameamua kuimarisha kiungo zaidi baada ya kuona Ngaya wanacheza katikati Chirwa anaingia vizuri tena Dk 76, Ngaya wanaonekana kuamka na kucheza vizuri katikati lakini bado mashambulizi yao si makali GOOOOOOOO Dk 73, Kakumusoko anaachia mkwaju mkali kwelikweli unajaa wavuni ilikuwa ni baada ya kupokea pasi ya Niyonzima Dk 70, Yanga wanaendelea kushambulia kwa kasi na Ngaya wanalazimika kuwa makini lasivyo watakutana na mvua ya mabao GOOOOOOO Dk 66 Said Khalfan anaachia Mkwaju mkali na kuandika bao kwa Ngaya GOOOOOOO Dk 65, Tambwe anaunganisha krosi safi ya Juma Abdul na kuandika bao la nne (Mashabiki wa Ngaya wanaanza kuondoka uwanjani) GOOOOOOOOO Dk 59, Kamusoko anamchambua kipa na kutoa pasi safi kwa Chirwa ambaye anaandika bao saaafi kabisa Dk 57 kona safi ya Said, mpira unamkuta Juma Abdul, inakuwa kona tena, inachongwa mara ya tatu Cannavaro anaondosha hapa Dk 56, Alfa anaingia na kupiga mpira krosi hapa lakini Dida anapangua na kuwa kona, inachongwa tena na kuwa kona tena SUB Dk 56 Nyanga wafanya mabadiliko tena, Ali anatoka na nafasi yake inachukuliwa Derita Alfa Dk 55, kuna wachezaji wanaingia kumbeba mchezaji aliyeumia wa Ngaya. KADI Dk 50, Saidi wa Ngaya analambwa kadi ya njano kwa kumfanyia madhambi Kamusoko aliyekuwa ameishamtoka SUB Dk 48 Ngaya wanafanya mabadiliko Said Haligan anaingia kuchukua nafasi ya Azeraden Dk 47, Msuva anaingia vizuri tena hapa, anaachia mkwaju mkali hapa lakini Ngaya wako makini Dk 45 Mpira umeanza, Yanga wanaanza kwa kasi na Msuva anaingia na kuachia mkwaju lakini Goal kick MAPUMZIKO Dk 45+2 nafasi nyingine kwa Yanga, kipa akiwa nje ya lango lakini Tambwe anashindwa kulenga na kuwa goal kick GOOOOOOOOO Dk 45+1, Msuva anaachia mkwaju mkali kutoka pembeni na kuandika bao la pili kwa Yanga Dk 45, Msuva anaingia vizuri anagongeana na Niyonzima anaachia mkwaju mkali lakini kipa Said Komandoo anaruka na kudaka kama nyani hapa Dk 44, Tambwe anakwenda vizuri hapa anawekawa chini hapa. Faulo inachongwa na Chirwa lakini Said Komandoo anaudaka kwa mbwembwe hapa GOOOOOOOOOOOOOO Dk 43, Haji Mwinyi anapiga mpira wa mrefu, Chirwa anauwahi na kupiga pasi safi kwa Zulu ambaye anaachia mkwaju saafi na kuandika bao moja kwa Yanga Dk 42, hatari kabisa katika lango la Yanga, Dida anaruka kuupiga ngumi mpira, lakini hakuupiga kwa nguvu, ukatua kwa Al Manana, naye akaachia shuti ambalo licha ya kutokuwepo kwa kipa lakini hakulenga lango Dk 40, krosi nyingine nzuri ya Mwingi, Tambwe anaruka hapa lakini kila Said Komando anaruka na kuudaka vizuri kabisa Dk 36, Yanga wanaonekana kuwa wepesi na wanapeleka krosi nyingi zaidi lakini mara nyingi kunakuwa hakuna watu wa kuzitumia. Lakini inaonekana hata mabeki wa pembeni wakati wanataka kufunga wao, jambo ambalo linawakosesha nafasi za kufungaDK 35, Yanga wanapata kona nyingine, inachongwa na Niyonzima lakini wanaokoa Ngaya na kuwa wa kurushwa Dk 31, Tambwe katika nafasi nzuri baada ya kupokea pasi nzuri ya Chirwa, yeye na kipa wa Ngaya aitwaye Komando. Lakini Tambwe anapaishaa juuuu Dk 30 hatari kwenye lango la Yanga, Fadhul wa Ngaya anaingia vizuri na kuachia mkwaju mkali lakini Dida yuko imara Dk 29, Niyonzima anachonga kona safi, inaondoshwa. Mpira unamkuta Juma Abdul na kuurudisha kwa Niyonzima na anaachia shuti kali lakini hakulenga Dk 28, Yanga wanapata kona ya kwanza baada ya krosi safi ya Zulu kuokolewa Dk 24, Dida anaonyesha umahiri kwa kuuwahi mpira baada ya Cannavaro kuteleza na kuanguka Dk 18, mpira wa Haji Mwinyi unakwenda juujuu na kugonga mwamba na kutoka nje. Goal kick Dk 16, krosi nzuri ya Juma Abdul ilitua langoni mwa Yanga lakini mwamuzi amesema ni madhambi Hata hivyo, Yanga wamekuwa wakijibu mashambulizi hayo kwa mipira ya krosi Mechi imeanza kwa kasi na Ngaya wamekuwa wakishambulia sana KIKOSI CHA YANGA 1. Deogratius Munishi 2. Juma Abdul 3. Mwinyi Haji 4. Nadir Haroub 5. Kelvin Yondani 6. Justin Zullu 7. Saimoni Msuva 8. Thabani Kamusoko 9. Amisi Tambwe 10. Obrey Chirwa 11. Haruna Niyonzima Akiba - Ali Mustafa - Hassani Kessy - Oscar Joshua - Emanuel Martin - Juma Mahadhi - Juma Saidi - Deusi Kaseke

Jumamosi, 11 Februari 2017

LIVE KUTOKA UWANJA WA TAIFA: SIMBA 3 VS 0 PRISONS (KIPINDI CHA PILI) SUB Dk 74 Pastory Athanas anaingia kuchukua nafasi ya Ibrahim Ajib Dk 73, Prisons wanaingia vizuri na Meshack anauchonga vizuri mpira lakini unatoka nje kidogo mwa lango la Simba Dk 73, pasi nzuri ya Mavugo, Kazimoto anaachia shuti kali hapa, lakini kipa anadaka Dk 72, Ndemla anaachia shuti kali hapa lakini goal kick SUB Dk 70 Shiza Kichuya anaingia kuchukua nafasi ya Liuzio GOOOOOOO Dk 68, Mavugo anaifungia Simba bao la tatu kwa Kichwa akiunganisha krosi ya outer ya Ajibu Dk 65 Chona wa Prisons naye yuko chini paleSUB Dk 62, Kazimoto anaingia kuchukua nafasi ya Mwanjale Dk 62 Mwanjale anatolewa nje kwenda kutibiwa Dk 61, Mwanjale yuko chini baada ya kuumia, inaonekana hataendelea kwani mara ya pili ndani ya dakika 5 anaanguka na kutibiwa Dk 58, Agyei tena anaikoa Simba baada ya krosi dongo ya Kimenya Dk 57, Krosi ya Bukungu ndani ya eneo la hatari lakini haikumfikia yoyote, Prisons wanaokoa SUB Dk 56 upande wa Prisons Meshack Selemani anaingia kuchukua nafasi ya Benjamin Asukile Dk 55, Mavugo anawatoka mabeki wa Simba, wanaokoa na kuwa kona, inachongwa lakini goal kick Dk 54, Prisons wanaingia ndani ya eneo la hatari la Simba, Agyei anafanya kazi ya ziada tena Dk 51, krosi nzuri ya Kimenya ndani ya lango la Simba, Agyei anatokea na kudaka kama nyani Dk 49, Hamisi wa Prisons anageuka vizuri na kuachia mkwaju lakini unakuwa goal kick Dk 47, Mwanjale anafanya kazi ya ziada kuokoa mbele ya Asukile aliyekuwa anakwenda kumuona Agyei, yuko chini anatibiwa sasa Dk 45, kipindi cha pili kimeanza na kila upande unaonekana kuwa makini

Alhamisi, 9 Februari 2017

Jumatano, 8 Februari 2017

Antonio Conte : “Naweza kuua mtu” Mzuka wa kocha Antonio Conte anapokuwa uwanjani umekuwa kivutio sana kwa mashabiki wa soka.Conte amekuwa mwenye furaha sana pale Chelsea inapopata ushindi haswa dhidi ya timu ngumu.Conte amekuwa akifanya mambo yanayowashangaza watu wengi kutokana na mizuka yake uwanjani mfano tukio alilofanya juzi alipoonekana kama anampiga kofi kocha wake msaidizi akimuelekeza kitu. Antonio Conte amekiri kwamba kocha wake msaidizi Angello Allesio amekuwa mhanga mkubwa wa mizuka yake.Allesio ndio mtu anayekaa pembeni na Conte na hii inamfanya kukumbana na dhahma zote za Muitaliano huyo anapopandisha mizuka.Hali hii huwashangaza watu wengi lakini Allesio anaonekana kumzoea Conte. Conte amekiri kwamba anaweza hata kuua mtu,Conte amesema akiona kitu hakiendi sawa huwa anachanganyikiwa sana “nikiona jambo halipo sawa,naweza kufanya lolote nadhani naweza hata kuua mtu” Conte aliiambia Sky Sports.Conte alisema katika mechi ya Arsenal alimuona Kante amekaa sehemu isiyo sahihi na alitaka kumuelekeza ila akamuona Allesio yuko pembeni ndipo alimpiga yeye akimuambia amuelekeze Kante. Conte anadai aliamini sana mbinu zake wakati anakuja Uingereza japo mechi za kwanza la ligi hiyo walishinda lakini hakuona kama walishinda kwa kutumia mbinu zake.Conte anasema anashukuru kuona mbinu zake zikiitoa Chelsea chini na sasa kuwa kati ya timu za kuogopwa nchini Uingereza. Lakini Conte bado haamini kwamba Chelsea itakuwa bingwa,Conte anasema ligi ya Uingereza hakuna kitu kiitwacho “mechi rahisi” na amewataka vijana wake wapambane tu hadi mwisho.Conte ametolea mfano Liverpool walivyofungwa na Hull City huku akikiri kwamba angependa mechi kati ya Swansea na Man City ingeisha suluhu.

KAULI KUMI ZA MANJI BAADA YA KUSIKIA AMEITWA NA MAKONDA KUHUSIANA NA MADAWA YA KULEVYA MOJA: "Nimesikia wakisema natakiwa kufika kituo cha Polisi siku ya Ijumaa. Mimi nina nafasi mbili kwenye jamii, Mimi ni baba wa familia yangu lakini nafasi yangu ya pili mimi ni mwenyekiti wa Yanga na nyote mnajua ninavyoheshimiwa." MBILI: "Huwezi kunitangaza kupitia redio kwamba niende kwenye kutuo cha polisi saa tano. Makonda ni mdogo kwangu kiumri. Nafikiri anajua taratibu sahihi za kufanya, iko wapi barua ya kuwa nahitajiwa." TATU "Na katiba inasema kila mtu ana haki yake, pia akumbuke unaponichafua mimi kama Mwenyekiti wa Yanga unachafua Yanga nzima." NNE: "Kama unataka mimi nikusaidie kutaja wauzaji, lakini vipi unaniweka hadharani kwa kuanza kunitangaza mimi ambaye ni ninayekusaidia wewe. Utanilinda vipi?" TANO: "Mimi nitaenda Kituo cha Polisi kesho sisubiri hiyo Ijumaa."

MANJI AAMUA KWENDA SENTRO POLISI KESHO BADALA YA IJUMAA, ATAKA YEYE NA MAKONDA WAPIMWE Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kesho amepanga kwenda kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi cha jijini Dar es Salaam maarufu kama "Sentro" kesho badala ya keshokutwa . Manji ameyasema hayo hivi punde saa chache tangu Mkuu wa Mkoa wa Polisi wa Dar es Salaam , Paul Makonda kutangaza majina 65 ya wanaitakiwa kufika kwenye kituo cha hicho kikubwa cha Polisi ili kusaidia vita ya kupambana na madawa ya kulevya kama sehemu ya wanaotumihumiwa au la. Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Manji alisema kuwa hawezi kubadili ratiba zake keshokutwa na kwenda kupanga foleni ya watu 65 kwa ajili ya kitu hicho. Manji alisema, ana kazi nyingi za kufanya hiyo keshokutwa ijumaa, hivyo ataenda kesho asubuhi na mapema sana ili kutekeleza suala hilo aliloitiwa. Pamoja na kukubali kwenda tena mapema, Manji amesema amepanga kuchukua hatua za kisheria kwa kwenda mahamakani kwa ajili ya kumfungulia mashtaka Makonda. "Mimi nitaenda kituo cha Polisi kesho asubuhi na mapema na sisubiri hiyo Ijumaa anayotaka yeye Makonda naomba nieleweke. "Baada ya kutoa huo ushirikiano Polisi, basi nitaenda mahakamani kumfungilia mashtaka Makonda kwa kunidhalilisha kwa kutumia vibaya jina langu, kwani kitendo cha kutumia jina la mtu vibaya ni makosa na katiba ya nchi inaniruhusu kumshtaki Makonda," alisema Manji. "Kama kweli mtu unamuita kukusaidia kwa ajili ya madawa ya kulevya, vipi unamtangaza mbele ya hadhara. Akishakutajia utaweza vipi kumlinda muda wote, ingekuwa vizuri kumuita kimyakimya, halafu akutajie na wewe ufanyie kazi hasa kama uliona anajua," alisema. "Kweli nitakwenda Alhamisi, niko tayari kupimwa na kusachiwa. Lakini ningependa na Makonda apimwe pia na kusachiwa. "Sikatai kuwepo na vita ya madawa, lakini hauwezi ukafanya kila kitu bila ya kujali haki za watu, heshima zao, majina yao. Hii si sawa na siwezi kukubali."

Jumatatu, 6 Februari 2017

BREAKING NEWS: MTOTO WA MATUMLA APIGWA, AZIMIA NA KUKIMBIZWA HOSPITALI Mohammed Matumla amepigwa na kuumizwa vibaya hali iliyosababishwa akimbizwe hospitali ya Temeke kwa kutumia gari dogo la mizigo au pick up. Matumla ambaye ni mtoto wa bondia nyota wa zamani, Rashid Matumla amepigwa katika raundi ya saba na bondia Mfaume Mfaume. Pambano lao lilikuwa la utangulizi lililokuwa likisubiriwa kwa hamu zaidi leo. Matumla alianza kupoteza mwelekeo katika raundi ya tano lakini akajitutumua hadi raundi ya saba ambayo aliambulia kipigo kikali kutoka kwa Mfaume. Baada ya kusukumiwa ngumi mfululizo, alianguka lakini akaonekana ni kama mtu aliyechanganyikiwa, akitaka kukimbia. wakamuhi na kumzuia na baadaye kumlaza chini. Daktari aliyekuwa mtazamaji, ndiye alilazimika kumtibu kwa ajili ya huduma ya kwanza kwa kuwa hakukuwa na huduma ya kwanza wala gari la wagonjwa ukumbini hapo. Wakati anaondolewa ukumbini hapo, hali yake haikuwa nzuri na alikimbizwa katika hospitali ya Temeke.

SIMBA IMETENGA DAKIKA HIZI 270 KWA AJILI YA YANGA.... Baada ya juzi Jumamosi timu ya Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Majimaji, benchi la ufundi la timu hiyo limeitengea Yanga dakika 270 za kifo. Kocha msaidizi wa timu hiyo, Mganda, Jackson Mayanja amesema kuwa endapo Yanga itafanikiwa kuzipenya dakika hizo vizuri bila ya kipigo chochote, basi inaweza kutwaa ubingwa ligi kuu. Dakika hizo 270 za maangamizi ambazo Simba imeitengea Yanga ni zile zitakazoikutanisha na Simba, Azam pamoja na Mtibwa Sugar. Mayanja alisema kuwa mechi hizo ni ngumu kwa Yanga na ana uhakika itapoteza mechi moja kati ya hizo, jambo ambalo litawarudisha katika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kuu. “Nawashukuru sana wachezaji wangu kwa jinsi walivyopambana dhidi ya Majimaji na tukafanikiwa kupata matokeo mazuri ambayo yamerudisha matumaini yetu ya kuhakikisha tunapambana vilivyo kuwania ubingwa wa ligi kuu. “Siku tulipofungwa na Azam hakika hali haikuwa nzuri lakini sasa tupo vizuri na tutapambana kuhakikisha tunaishusha Yanga katika nafasi hiyo na ni matumaini yetu kuwa hilo litatimia ndani ya siku chache zijazo kwa sababu inakabiliwa na mechi ngumu kuliko sisi. “Hajacheza na sisi lakini pia haijacheza na Azam pamoja na Mtibwa Sugar, kwa jinsi hali ilivyo naamini kabisa Yanga lazima itasimamishwa katika mechi hizo kama siyo sisi basi Azam au Mtibwa Sugar watafanya hizo,” alisema Mayanja.

RAIS WA VILLA YA UGANDA, AMUOMBA OKWI BAO MOJA KILA MECHI Mshambuliaji wa zamani wa Simba na Sonderjsyke ya Denmark, Emmanuel Okwi ameombwa ajitahidi angalau kupata wastani wa bao moja kila mechi. Rais wa SC Villa, Ben Immanuel Misagga amemuomba Okwi kukaza kamba na ikiwezekana kufunga mabao. “Unarudi nyumbani, lakini tunachotaka kikubwa ni mabao. Kama utaweza angalau kila mechi bao moja,” alisema Misagga wakati akimtambulisha Okwi. Okwi aliamua kuvunja mkataba na Sonderjsyke kwa madai ya kupata nafasi ya kutosha ya kucheza. Alijiunga na klabu hiyo akitokea Simba aliyopata nayo mafanikio makubwa

Jumamosi, 4 Februari 2017

SERENGETI BOYS YAPANGWA KUNDI B GABON Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Tanzania, Serengeti Boys imepangwa Kundi B pamoja na Angola, Mali na Niger katika fainali za vijana chini ya umri wa miaka (AFCON U-17) mwaka huu Gabon. Katika makundi yaliyotolewa leo na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), wenyeji Gabon watakuwa Kundi A pamoja na Guinea, Cameroon na Ghana na michuano hiyo itaanza Aprili 2 mwaka huu. Tanzania imerejeshwa kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika kwa vijana wa umri huo baada ya kushinda rufaa yake dhidi ya Kongo Brazzaville iliyotumia mchezaji aliyezidi umri. Mwanzoni mwa mwezi uliopita, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) liliwapa siku 10 Shirikisho la Soka Kongo (FECOFOOT) kumuwasilisha mchezaji Langa Lesse Bercy mjini Libreville, Gabon afanyiwe vipimo vya MRI ili kuthibitisha umri wake kama anaruhusiwa kucheza mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17, lakini wameshindwa kufanya hivyo. Na hiyo ilikuwa mara ya tatu, FECOFOOT wanashindwa kumpeleka Langa Lesse Bercy akafanyiwe vipimo baada ya kushindwa kufany hivyo awali mara mbili mjini Cairo, Misri kwa vipimo. Fainali za U-17 Afrika ilikuwa zifanyike nchini Madagascar kuanzia Aprili mwaka huu, lakini mwezi uliopita CAF iliivua uenyeji na kutoa muda hadi Januari 30 mwaka huu nchi nyingine kujitokeza kuomba uenyeji kabla ya juzi kuiteua Gabon kuandaa fainali hizo.

HATIMAYE LIPULI YAREJEA LIGI KUU TANZANIA BARA Lipuli imeitwanga Polisi kwa mabao 3-1 na kufanikiwa kurejea Ligi Kuu Bara. Ushindi wa Liipuli unaifanya kuwa timu ya kwanza kurejea Ligi Kuu Bara.

WENGER AKIWA JUKWAANI AKISHUHUDIA ARSENAL IKIADHIBIWA BILA HURUMA NA WENYEJI WAKE CHELSEA Walinzi wa Uwanja wa Stamford Bridge walilazimika kuwazuia mashabiki kuendelea na zoezi na kupiga picha na Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ambaye alikuwa jukwaani. Wenger alikuwa jukwaani akitumikia adhabu ya mechi tatu kutokuwa katika benchi wakati Chelsea ikiitwanga Arsenal 3-1

TASWIRA NAMNA ARSENAL ILIVYOCHEZEA KICHAPO CHA MABAO 3-1 PALE DARAJANI CHELSEA: Courtois; Azpilicueta, David Luiz, Cahill; Moses (Zouma 87), Kante, Matic, Alonso; Pedro (Willian 84), Diego Costa, Hazard (Fabregas 84). SUBS NOT USED: Begovic, Terry, Batshuayi, Chalobah. GOALS: Alonso 13, Hazard 53, Fabregas 86 BOOKINGS: Matic ARSENAL: Cech; Bellerin (Gabriel 14), Mustafi, Koscielny, Monreal; Coquelin (Giroud 65), Oxlade-Chamberlain; Walcott (Welbeck 70), Ozil, Iwobi; Sanchez. SUBS NOT USED: Ospina, Gibbs, Reine-Adelaide, Maitland-Niles. GOALS: Giroud 90 BOOKINGS: Mustafi REFEREE: Martin Atkinson

LIVE KUTOKA MAJIMAJI SONGEA: MAJIMAJI 0-2 SIMBA GOOOOOOOOO Dk 64 Ndemla anaachia mkwaju mkali na kuiandikia Simba bao la pili. Ulikuwa ni mpira safi wa kona, Majimaji wakajichanganya naye hakufanya ajizi Dk 63, Simba wanagongeana vizuri, Mavugo anampa Kotei anaachia shuti kali, linaokolewa na kuwa kona SUB DK 60, James Kotei anaingia kuchukua nafasi ya Ajibu, mfungaji wa bao pekee hadi sasa Dk 58, Mavugo anamchambua beki hapa, anaachia mkwaju lakini hakulenga langoDk 57 sasa, Majimaji ndiyo wanaoshambulia sana, Simba wanapaswa kuwa makini kwa kuwa inaweza kuwa hatari kwao Dk 56, Kaheza, yeye na kipa anapiga lakini mpira wake unamgonga kipa na kwenda nje. Kona, inachongwa lakini haina faisa DK 52, mpira mzuri wa Mavugo unaokolewa na kuwa kona, inachongwa na kuzaa kona nyingine SUB Dk 52, Simba wanamtoa Juma Liuzio na nafasi yake inachukuliwa na Pastory Athanas Dk 50, Sabato anajaribu kumtoka Mwanjale lakini anautoa na kuwa kona, inachongwa, Agyei anapangua na mabeki wanaondosha Dk 49, Kibuta anageuka na kuachia mkwaju mkali kwa mara nyingine, lakini hakulenga lango. Goal kick Dk 47 Simba wanagongeana vizuri kabisa hapa na Ajibu anaachia mkwaju mkali kabisa lakini sentimeta chache, goal kick Dk 45, mechi imeanza kwa kasi na Simba wanakuwa wa kwanza kufika kwenye lango la Majimaji MAPUMZIKO Dk 45+1 shuti la mpira wa adhabu wa Kaheza, Agyei anatema na mabeki wake wanaokoa. Inakuwa kona lakini haina manufaa kwa Majimaji DK 45+1, krosi nzuri kabisa, Kibuta yeye na kipa wa Simba, anafumba macho na kuukosa mpira DAKIKA 1 YA NYONGEZA Dk 45, Majimaji wanaingia tena kwenye lango la Simba lakini Mwanjale anaokoa mbali kabisa DK 44, nafasi nzuri kwa Majimaji, Sabato anaupata vizuri anapiga kichwa lakini anashindwa kulenga DK 42 sasa, Majimaji wanaonekana kufunguka na kucheza vizuri lakini hawako makini sana wanapoingia kwenye lango la Simba Dk 40, Kipangile wa Majimaji anaingia kwenye lango la Simba, lakini anashindwa kutulia Dk 39, Selemani Kibuta mbele ya Muzamiru anaachia mkwaju mkali kabisa hapa, unatoka pembeni kidogo ya lango la Simba Dk 35, Mavugo anapokea pasi nzuri ya Ajibu na kupiga shuti kali, linatoka sentimeta chache kabisa Dk 31, Sabato anaingia vizuri tena na kuachia shuti lakini hakulenga Dk 28 Majimaji wanapoteza nafasu nzuri hapa na Agyei anadaka vizuri kabisa Dk 22, Sabato anapoteza nafasi nzuri baada ya kuunganisha kichwa karibu na lango la Majimaji lakini hakulenga GOOOOOOO Dk 19, krosi safi ya Shiza Kichuya, Ajibu anaunganisha vizuri kwa kichwa na kuandika bao la kwanza kwa Simba Dk 15 sasa, Simba wanaonekana na kugongeana vizuri lakini bado hakuna kashkash kubwa wanayofikisha langoni Dk 12, Kona ya pili wanapata Majimaji hapa baada ya Bukungu kuutoa mpira nje, inachongwa lakini Agyei anadaka Dk 11 Simba wanagongeana vizuri na Liuzio anaupachika mpira wavuni. Mwamuzi anasema kabla, tayari alikuwa ameotea DK 9, krosi inapigwa langoni mwa Simba, kipa Agyei anakwenda markiti lakini Zimbwe au Tshabalala anajitokeza na kuokoa vizuri kabisa Dk 8, kona ya kwanza ya mchezo wanapata Majimaji baada ya Mwanjale kuutoa mpira kwa kichwa Dk 7, Peter anageuka na kuachia mkwaju hapa lakini Agyei anadaka kwa ulaini Dk 7 sasa, bado mpira unachezwa zaidi katikati ya uwanja na hakuna mashambulizi makubwa ndani ya Dk 2 Simba wanaingia kwenye lango la Majimaji, Mazamiru anapiga shuti linawababatiza mabeki hapa na wanaokoa Dk ya 1, Majimaji wanaanza kwa kasi, krosi nzuri inapigwa hapa lakini mwamuzi anasema offside KIKOSI CHA SIMBA: 1. Daniel Agyei 2. Janvier Bukungu 3. Mohamed Zimbwe 4. Novatus Lufunga 5. Method Mwanjale (C) 6. Muzamiru Yassin 7. Shiza Kichuya 8. Said Ndemla 9. Laudit Mavugo 10. Juma Liuzio 11. Ibrahim Ajibu SUB Peter Manyika Mwinyi Mazimoto James Kotei Haji Ugando Athanas Kitandu 04 Feb 2017

Ijumaa, 3 Februari 2017

EXCLUSIVE: CAF YATANGAZA SERENGETI BOYS IMEFUZU MICHUANO YA KOMBE LA MATAIFA AFRIKA Shirikisho la Soka Afrika (Caf) limetangaza Serengeri Boys kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa vijana chini ya miaka 17. Caf imeitangaza Tanzania kupitia Serengeti Boys na kuing’oa Congo iliyofuzu lakini ikawa na tuhuma ya kumchezesha mchezaji kijeba Langa Bercy ambaye imeelezwa anacheza Ligi Kuu ya Congo. Ilitakiwa Congo kumpeleka mchezaji huyo kwa ajili ya vipimo vya DNA ili kubaini umri wake kitaalamu. Msemaji wa TFF, Alfred Lucas Mapunda amethibitisha hilo: "Ni kweli tumepata taarifa hizo za Caf kwamba Congo wametolewa nje. Tanzania sasa imefuzu." Lakini mwisho ilionekana suala hilo lilishindikana na mwisho usiku huu, Caf imetangaza rasmi kuwa Serengeti Boys au Tanzania ndiyo iliyofuzu michuano hiyo ya vijana Afrika. Katika mechi ya mwisho, Serengeti Boys ilifungwa bao 1-0 ikiwa ni baada ya kushinda 3-2 nyumbani Dar es Salaam na mfungaji wa bao la Congo nyumbani kwao akiwa ni kijeba huyo aliyekuwa amekomaa sura ile mbaya lakini akachezea timu ya watoto

LIVE KUTOKA UWANJA WA TAIFA: YANGA 0-0 STAND UNITED DK 14, kila upande unafanya mashambulizi lakini ulinzi unaonekana kuwa mkali zaidi kwa kila upande Dk 10, Shambulizi jingine wanafanya Yanga kwa mpira wa faulo wa Mwinyi lakini Stand wanaokoa Dk 7, Selembe anaingia vizuri kabisa baada ya kugongeana na Chidiebere lakini Disa anatoka na kudaka Dk 5, Yanga inapata kona ya pili baada ya Niyonzima kupiga mpira ukaokolewa na kutoka. Kona yenye haina matunda Dk 4, Ngoma anaingia vizuri, lakini Stand wanawahi na kutoa inakuwa kona Dk ya 1 mpira umeanza kwa kasi na Yanga ndiyo wanaoshambulia mfululizo KIKOSI CHA YANGA 1. Deougratius Munishi ‘Dida’ 2. Juma Abdul 3. Mwinyi Haji 4. Nadir Haroub 5. Kelvin Yondani 6. Justice Zulu 7. Simon Msuva 8. Thabani Kamusoko 9. Donald Ngoma 10. Obey Chirwa 11. Haruna Niyonzima Akiba Ben Kakolanya Ramadhani Kessy Vicent Andrew Deus Kaseke Martin Emmanuel Said Juma Makapu

Alhamisi, 2 Februari 2017

WENGER AWEKA HADHARANI NIA YA KUMSAJILI KINDA ANAYEMFANANISHA NA THIERRY HENRY Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ameweka hadharani nia yake ya kumsajili mchezaji kinda wa Monaco, Kylian Mbappe. Wenger amesema Mbappe mwenye umri wa miaka 18, anamfananisha na gwiji wa Arsenal, Thierry Henry. Ameweka wazi nia yake hiyo kijana huyo aliyefunga mabao sita katika mechi 19, atakuwa hatari zaidi kila anapopata uzoefu. Inaonekana Arsenal na Monaco wameanza mazungumzo ya awali kwa ajili ya usajili wa kinda huyo.

LIUZIO ASEMA SIMBA WAMEJUA KINACHOWAANGUSHA, KAZI INAANZIA KWA MAJIMAJI Straika wa Simba, Juma Liuzio, amesema wamejua tatizo lililopo katika kikosi chao na sasa wanajipanga kufanya kweli katika mchezo wao dhidi ya Majimaji. Liuzio amesema tatizo kubwa katika kikosi chao ni umaliziaji, akidai wanatengeneza nafasi nyingi lakini umaliziaji ndiyo mbovu, sasa wameufanyia kazi na wataanza kuonyesha mabadiliko hayo katika mechi ya Majimaji. “Sidhani kama Simba ni timu mbovu kama watu wanavyofikiri, nikwambie kitu, sisi washambuliaji tungekuwa makini mechi na Azam, basi matokeo yasingemalizika yale ya kufungwa bao 1-0. “Kiukweli, viungo wetu walitutengenezea nafasi nyingi za kufunga lakini umakini wetu mbaya ndiyo ukasababisha sisi tupoteze mchezo huo. “Tumeliona hilo tatizo letu, niwaahidi mashabiki wa Simba kuwa, tatizo hilo tumelimaliza na mechi dhidi ya Majimaji tutathibitisha hilo,” alisema Liuzio.

CHAMA CHA WAAMUZI CHAMPA KAZI HAJI MARA ATAFUTE MWAMUZI WA YANGA VS SIMBA Kama unakumbuka, Msemaji wa Simba, Haji Manara amekuwa akisisitiza mechi dhidi ya watani wao, Yanga ichezeshwe na mwamuzi kutoka nje. Sasa Chama cha Waamuzi Tanzania (Frat) kimempa Manara kazi ya kutafuta atakayeweza kuchezesha mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga kwa kufuata weledi ya sheria 17 za soka. Kwa kuwa watani hao wanatarajia kukutana Februari 25, mwaka huu, maana yake Manara ananafasi kubwa ya kumpata mwamuzi huyo. Simba na Yanga, zinatarajia kukutana katika Ligi Kuu Bara ambapo awali ilipangwa wacheze Februari 18 lakini mchezo huo umesogezwa mbele kutokana na majukumu ya kimataifa ya Yanga. Mwenyekiti wa Frat, Mwalimu Nassor, amesema bado hawajapanga ratiba ya mwamuzi wa mechi ya watani. “Wakati mwingine hatupendi malalamiko, maana kila timu inayofungwa au kuzidiwa ndiyo hulalamika. Basi yeye atafute huyo mwamuzi ili tupunguze lawama," alisema Mwalimu. SOURCE: CHAMPIONI

CAMEROON YAITWANGA GHANA NA KUIFUATA MISRI FAINALI YA AFCON Cameroon imeifuata Misri kwenye fainali ya Kombe la Mataifa Afrika maarufu kama Afcon. Kikosi cha Cameroon ambacho kilikuwa hakipewi nafasi kubwa, kimeitwanga Ghana kwa mabao 2-0 katika mechi ya pili ya nusu fainali. Cameroon imeifuata Misri kwenye fainali ya Kombe la Mataifa Afrika maarufu kama Afcon. Kikosi cha Cameroon ambacho kilikuwa hakipewi nafasi kubwa, kimeitwanga Ghana kwa mabao 2-0 katika mechi ya pili ya nusu fainali. Ilikuwa mechi ngumu tokea mwanzo na mapumziko ilikuwa ni sare ya bila kufungana. Ngadeu Ngadjui aliiifungia Ghana bao katika dakika ya 72 baada ya uzembe wa mabeki wa Ghana lakini wakati inaonekana kama Ghana watasawazisha, Cameroon wakamaliza kazi kupitia kwa Christian Bassogog..

MESSI MTU MWINGINE, AFUNGA BONGE LA BAO BARCELONA IKIITWANGA ATLETICO 2-1 COPA DEL REAY FC Barcelona imeishinda Atletico MAdrid kwa mabao 2-1 katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Mfalme nyumbani kwake Vincente Cardelon, Madrid. Gumzo zaidi ni bao la pili la Barcelona lililofungwa na Lionel Messi akiwa katikati ya msitu wa mabeki wa Atletico. Messi ameonyesha ni “mtu wa sayari nyingine” kutokana na namna alivyokokota mpira huo katikati ya mabeki kabla ya kuachia fataki kali la mguu wa kushoto. Bao jingine la Barcelona lilifungwa na Luiz Suarez ambaye aliwachambua mabeki wawili akitokea katikati ya uwanja kabla ya kufunga. Bao la wenyeji lilifungwa na Mfaransa Antoine Griezmann ambaye alimzidi ujanja Javier Mascherano na kupiga kichwa safi kabisa. Atletico Madrid (4-4-2): Moya; Vrsaljko (Torres 46), Godin, Savic, Filipe; Juanfran, Gabi, Koke, Saul (Gaitan 59); Carrasco (Gameiro 70), Griezmann. Subs not used: Moreira, Lucas, Keidi, Correa, Goal: Griezmann Booked: Savic, Juanfran, Saul, Gabi, Griezmann Barcelona (4-3-3): Cillessen; Sergi Roberto, Pique, Umtiti, Alba; Rakitic (Denis 58), Mascherano, Gomes (Rafinha 72), Mesis, Suarez, Neymar. Subs not used: Masip, Arda, Alcacer, Vidal, Mathieu Goals: Suarez, Messi Booked: Mascherano, Messi, Neymar

PICHAAAAAAZ: MAN CITY ILIVYOITWANGA WEST HAM NYUNDO NNE BILA MAJIBU WEST HAM (4-2-3-1): Randolph 5; Byram 5, Reid 6, Fonte 5, Cresswell 4; Noble 5, Obiang 4 (Snodgrass 64 min, 5); Fegouli 4 (Fernandes 64, 5), Antonio 6, Lanzini 5; Carroll 5 (Fletcher 79) Subs not used: Adrian, Collins, Calleri, Quina Booked: Obiang, Lanzini, Carroll Manager: Slaven Bilic 5 MANCHESTER CITY (4-3-3): Caballero 6; Sagna 6, Stones 6, Otamendi 6, Kolarov 6; De Bruyne 8 (Fernandinho 68, 5), Toure 6, Silva 8.5 (Delph 80); Sterling 8 (Aguero 73, 5), Jesus 7.5, Sane 8 Subs not used: Bravo, Kompany, Zabaleta, Jesus Navas Goals: De Bruyne 17, Silva 21, Jesus 39, Toure 67 pen Booked: Jesus, De Bruyne, Sterling Manager: Pep Guardiola 7 Referee: Kevin Friend 6 Attendance: 56,980

MAN UNITED WALIVYOPATA SARE YA TISA PREMIER MSIMU HUU, HULL CITY WAKIKOMAA 0-0 OLD TRAFFORD Licha ya kuwa nyumbani Old Trafford, Manchester United imejikuta ikipata safe ya 0-0 dhidi ya Hull City. Pamoja na juhudi kubwa za washambuliaji wake wakiongozwa na Zlatan Ibrahimovic, Wayne Rooney na bwamdogo Rashford, bado Man United ilishindwa kubadili mambo hadi mwisho wa dakika 90.

CROUCH AFUNGA BAO LA 100 STOKE CITY IKIPATA SARE YA 1-1 VS EVERTON STOKE CITY (4-2-3-1): Grant 7: Bardsley 6.5, Shawcross 6, Martins Indi 7, Pieters 6.5: Whelan 7, Adam 7: Afellay 7, Allen 6 (Berahino 67mins 6), Arnautovic 6 (Ngoy 88): Crouch 8 Unused subs: Given (GK), Muniesa, Berahino, Bony, Imbula, Edwards Goal – Crouch (7) Booked - Bardsley Manager – Mark Hughes EVERTON (3-5-2): Robles 6: Holgate 6 (McCarthy 46mins 7), Williams 7, Funes Mori 6: Coleman 7, Davies 7, Barkley 6, Schneiderlin 7, Baines 7.5: Mirallas 7 (Lookman 69mins 7), Lukaku 6 Unused subs: Stekelenburg (GK), Jagielka, Lennon, Barry, Valencia Manager – Ronald Koeman Goal - Shawcross (o.g 39) Attendance – 27,612 Referee – Craig Pawson 8 Man-of-the-Match – Peter Crouch

KIPA WA MIAKA 44 ALIVYOIPELEKA MISRI FAINALI YA AFCON Misri imeong’oa Burkina Faso na kiting fainali ya Kombe la Afcon nchini Gabon. Kikosi cha Misri ambacho kilikuwa hakipewi nafasi kimetinga fainali baada ya kushinda kwa penalti 4-3. Mechi hiyo ilichezwa kwa dakika 120 na bado matokeo yalikuwa ni safe ya 1-1. Baada ya hapo uliingia wakati wa mikwaju ya penalti na kips mkongwe zaidi barani Afrika Essam El-Hadary mwenye umri wa miaka 44 akaonyesha umuhimu wake kwa kupangua mikwaju miwili. El Hadary alianza kupangua penalti ya Kouakou Koffi, halafu ya Bertrand Traore aliyewahi kukipiga Chelsea na kupitisha safari ya Misri kwenda fainali. Burkina Faso (4-3-3): Koffi; Yago, Dayo, Kone, Coulibaly; A R Traore (Diawara 80), Kabore; B Traore, Toure, Nakoulma; Bance (A Traore 102) Unused subs: Sawadogo, Paro, Malo, Sare, Pitroipa, Guira, Koanda, Bayala, Sanou Goal: Bance 77 Egypt (4-2-3-1): El-Hadary; Elmohamady (Gaber 106), Hegazy, Gabr, Fathy; Hamed, I. Salah; M. Salah, Said, Hassan (Ramadan 85); Kahraba (Warda 74) Unused subs: Gaber, Koka, Dewidar, Hafez, Ekramy, Elneny, Mohsen, Samir Goal: M. Salah 66 Stadium: Stade de l'Amitie, Libreville

Jumatano, 1 Februari 2017

KALI ASEMA MAJIMAJI WANAWASUBIRI SIMBA WAKAACHE POINTI SONGEA Muda ukiwa unahesabika kuelekea mchezo wao dhidi ya Simba, Kocha Mkuu wa Majimaji, Muingereza, Kally Ongala amesema haoni sababu ya kushindwa kuifunga Simba kwa kuwa wapo katika hatari ya kushuka daraja. Simba ambayo inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 45 nyuma ya vinara wa ligi hiyo Yanga wanaoongoza kwa pointi 46, Jumapili hii inatarajia kucheza na Majimaji mkoani Songea kwenye Uwanja wa Majimaji ambapo kwa sasa wapinzani wao hao wanakamata nafasi ya 14 wakiwa na pointi 20. Akizungumza Ongalla alisema kutokana na kutopata muda mrefu wa kufanya maandalizi yao hawana sababu yoyote ya kushindwa kuifunga Simba kwa kuwa wapo kwenye wakati mgumu. "Kiukweli tunashukuru tunaendelea na maandalizi kwa kuwa muda umekuwa wa kutosha hivyo tutahakikisha tunaifunga Simba kwa sababu hatupo katika nafasi nzuri hivyo ushindi kwetu ni kitu muhimu. “Unajua Simba ni timu nzuri kwa sababu hata ukiangalia wapo katika nafasi nzuri kwenye msimamo tofauti na sisi, sasa hilo hatutaki kulipa nafasi kwa kuwa tunachokiangalia ni suala la matokeo hivyo wao wajue kuwa lazima huku watuachie pointi tatu," alisema Ongalla.

BAO LA DAVID LUIZ WA CHELSEA WAKATI KIPA WA LIVERPOOL AKIPANGA KIKOSI Hivi ndivyo David Luiz alivyomtungua kipa Simon Mignolet wa Liverpool wakati akipanga ukuta.

PAYET AANZA KUKIPIGA UFARANSA MARSEILLE IKIIGARAGAZA LYON KWA 2-1 Kiungo mpya wa Marseille, Dimitri Payet ameingia katika mechi ambayo imeisha kwa kikosi chake kuisha kwa sare ya mabao 2-1. Marseille imeitwanga Lyon kwa mabao 2-1 katika mechi ya michuano ya Coupe de France kwenye Uwanja wa Velodrome, usiku wa kuamkia leo. Payet amejiunga na West Ham kwa dau la pauni million 25.

ARSENAL ILIVYOOSHWA NA WATFORD KWA KUCHAPWA MABAO 2-1 Arsenal: Cech 6.5; Gabriel 5, Mustafi 5, Koscielny 5, Monreal 5; Ramsey 4 (Oxlade-Chamberlain 20 min, 6), Coquelin 6 (Perez 67, 6), Iwobi 6.5, Ozil 6, Sanchez 6.5; Giroud 4 (Walcott 46, 7) Substitutes not used: Ospina, Gibbs, Bellerin, Maitland-Nile Manager: Arsene Wenger 6 Scorers: Iwobi 58 Booked: Gabriel, Monreal, Sanchez Watford: Gomes 7.5; Cathcart 6.5, Prodl 7, Kaboul 7.5, Britos 6; Behrami 6.5 (Doucoure 63, 5); Janmaat 6, Capoue 8, Cleverley 6, Niang 6 (Success 69, 5); Deeney 6 (Okaka 85). Substitutes not used: Arlauskis, Mariappa, Mason, Watson. Manager: Walter Mazzarri 6.5 Scorers: Kaboul 10, Deeney 13 Booked: Prodl, Okaka, Cleverley Referee: Andre Marriner Attendance: 60,035

Jumanne, 31 Januari 2017

BAADA YEYE NA KLOPP "KUSHINDWANA", SAKHO SASA ANUKIA CRYSTAL PALACE Klabu ya Crystal Palace imeonyesha nia ya kumpata beki Mamadou Sakho. Liverpool intake kulipwa pauni milioni 20 ili kumuachia beki huyo raia wa Ufaransa. Sakho na Kocha Jurgen Kloop aria wa Ujerumani wanaonekana kutoelewana kabisa. Wakati dirisha la usajili linakwenda ukingoni , inaonekana juhudi zinafanyika.

BAADA YA SIMBA KUITOLEA NJE, MAMELODI SASA KUIVAA AZAM ALHAMISI Baada ya kikosi cha Simba kutoa nje kucheza na Mamelodi, ssa timu hiyo itashuka dimbani Alhamisi, kuivaa Azam FC. Taarifa zinasema, Mamelodi wataendelea na maandalizi kwa ajili ya mechi dhidi ya Azam FC hiyo Alhamisi, mechi inayotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Awali, Mabingwa hao wa Afrika walitakiwa kucheza kesho dhidi ya Simba, lakini klabu hiyo imeona ina majukumu ya maandalizi dhidi ya Majimaji mjini Songea, wikiendi hii. Lakini pia kumekuwa na taarifa kwamba waandaaji wa mechi hiyo hawakuwa na maandalizi mazuri kati yao na uongozi wa Simba kuhusiana na mechi hiyo. Hata hivyo, mmoja wa waandaaji amesema, Simba walikuwa na taarifa za kutosha lakini wamegeuka huenda inatokana na wao kupoteza mechi dhidi ya Azam FC Jumamosi na Yanga ikaishinda Mwadui FC na kukwea kileleni.

Jumatatu, 30 Januari 2017

SIMU INAWEZA KUMTIA PAUL POGBA MATATANI, USHAHIDI HUU HAPA…Kiungo wa bei kubwa wa Manchester United, Paul Pogba anaweza kuingia matatani baada ya kuonekana akiendesha gari huku akitumia simu kitu ambacho ni kinyume na sheria za uendeshaji gari nchini England.

MAMELODI SUNDOWNS FC WATUA DAR KUZIFUATA SIMBA, AZAM Msafara wa kikosi cha Mamelodi Sundowns FC ya Afrika Kusini umewasili leo Jumatatu mchana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuweka kambi kwa muda kisha kucheza mechi mbili za kirafiki. Mamelodi wamewasili Dar es Salaam wakiwa na jumlaya watu 42 huku ikielezwa kuwa wengine 10 wanatarajiwa kuingia kesho Jumanne. Ikiwa Dar es Salaam, Mamelod inatarajiwa kucheza mechi za kirafiki dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa kisha dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa Azam Complex wiki hii kabla ya kuondoka Jumamosi ijayo.

DIMITRI PAYET JEURI SANA, AKAMILISHA DILI LA UHAMISHO, AWATOLEA KAULI WEST HAM Dimitri Payet ametangazwa rasmi kuwa mchezaji wa Marseille ya Ufaransa akitokea West Ham United ya England kwa ada ya pauni 25m lakini kuna neno ametoa kuhusu timu yake ya zamani. Payet ambaye alitolewa lugha nyingi kali na mashabiki wa West Ham walimuona kama msaliti kwa kugoma kucheza akitaka auzwe amesaini mkataba wa miaka minne na nusu na klabu yake hiyo ya nyumbani na kuamua kuzungumzia kilichotokea. Akizungumzia kuhusu tabia yake iliyojitokea mpaka dili hilo linakamilika, Payet amesema: "Sina haja ya kuthibitisha au kufafanua kuhusu tabia yangu. Slaven Bilic (kocha wa West Ham) tulizungumza na tunajua kilichotokea. “Sina cha ziada kuzungumzia kuhusu suala hilo, naona bora nitahifadhi hayo, nitayazungumza siku nyingine lakini siyo sasa, kwa ufupi nilihitaji sana kurejea Ufaransa hasa Marseille."

HAWA WACHEZAJI WOTE WAMEZALIWA LEO NA MIAKA YAO WALIYOTIMIZA Wachezaji waliozaliwa leo na umri waliotimiza (kwenye mabano) Fili Djuricic (25) Dimitar Berbatov (36) Arda Turan (30) Lucas Biglia (31) Peter Crouch (36) Juninho (42) HERI YA KUZALIWA KWAO