pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumatatu, 6 Februari 2017
BREAKING NEWS: MTOTO WA MATUMLA APIGWA, AZIMIA NA KUKIMBIZWA HOSPITALI Mohammed Matumla amepigwa na kuumizwa vibaya hali iliyosababishwa akimbizwe hospitali ya Temeke kwa kutumia gari dogo la mizigo au pick up. Matumla ambaye ni mtoto wa bondia nyota wa zamani, Rashid Matumla amepigwa katika raundi ya saba na bondia Mfaume Mfaume. Pambano lao lilikuwa la utangulizi lililokuwa likisubiriwa kwa hamu zaidi leo. Matumla alianza kupoteza mwelekeo katika raundi ya tano lakini akajitutumua hadi raundi ya saba ambayo aliambulia kipigo kikali kutoka kwa Mfaume. Baada ya kusukumiwa ngumi mfululizo, alianguka lakini akaonekana ni kama mtu aliyechanganyikiwa, akitaka kukimbia. wakamuhi na kumzuia na baadaye kumlaza chini. Daktari aliyekuwa mtazamaji, ndiye alilazimika kumtibu kwa ajili ya huduma ya kwanza kwa kuwa hakukuwa na huduma ya kwanza wala gari la wagonjwa ukumbini hapo. Wakati anaondolewa ukumbini hapo, hali yake haikuwa nzuri na alikimbizwa katika hospitali ya Temeke.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni