pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumatatu, 13 Februari 2017
OMOG AKUBALI, SASA SIMBA NI MWENDO KWENDA MBELE KUSAKA MABAO Unaweza kusema, Simba sasa wamenogewa baada ya ushindi mfululizo wa mabao matatu, hivyo wameapa kuendelea kucheza soka la ushambulizi. Simba imefanikiwa kuitwanga Majimaji ya Songea kwa mabao 3-0 kabla ya kufanya hivyo kwa Prisons ya Mbeya. Kocha Joseph Omog amesema, wataendelea kushambulia lakini tahadhari ni jambo muhimu zaidi. "Kweli, sasa tunaweza kushambulia zaidi. Lakini lazima tuwe makini katika ulinzi. Tutaendelea kushambulia kwa lengo kupata mabao zaidi," alisema Omog. Kabla ya mechi hizo mbili, mashabiki wa Simba walikuwa wakilalamika kwamba mfumo wa Omog umekuwa wa kujilinda sana
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni