pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Alhamisi, 9 Februari 2017
Tanzania yaporomoka, Cameroon yapaa viwango FIFA Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA), limetangaza viwango vipya vya ubora wa soka duniani kwa mwezi Februari, 2017 huku Tanzania ikiporomoka kwa mara nyingine. Tanzania imetupwa kwenye nafasi ya 158 ikiwa na alama 152 ikiporomoka kwa nafasi mbili kutoka mwezi uliopita ambapo ilikuwa katika nafasi ya 156. Barani Afrika Kufuatia mafanikio makubwa ya kubeba taji la Kombe la Mataifa ya Afrika Jumapili iliyopita, Camerron imepanda kwa nafasi 29 katika viwango vilivyotolewa. Cameroon inakamata nafasi ya 33 duniani ikiwa mbele ya Austria na nyuma ya Iran. Misri waliofungwa na Cameroon pamoja na wenyeji Gabon wamepanda pia. Misri wamesogea hadi nafasi ya 23 huku Gabon waliotolewa katika hatua ya makundi wakipanda kwa nafasi 21 na kushika nafasi ya 87 Kuna mabadiliko ya timu moja tu katika orodha ya kumi bora baada ya Ufaransa kuipiku Colombia na kutua namba 6 ilhali vinara Argentina wakiendeleza uongozi wao wakifuatiwa kwa ukaribu na Brazil na Ujerumani katika nafasi ya pili na ya tatu. Ukanda wa Afrika Mashariki Uganda imeendelea kuongoza licha ya kuporomoka kwa nafasi mbili na kutua nadasi ya 73 duniani, wanfuatiwa na Kenya katika nafasi ya 87. Rwanda iko katika nafasi ya 100 ikiwa imeteremka kwa nafasi saba ikifuatiwa na Burundi katika nafasi ya 138 mbele ya Tanzania.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni