Jumanne, 14 Februari 2017

KAMA ULIFIKIRI SIMBA WAMEITANGULIZA YANGA, WANACHOWAZA NI KINGINE KABISAAAA... Wakati homa ya pambano la watani wa jadi, Simba na Yanga ikizidi kupanda taratibu, Kocha Msaidizi wa Simba, Mganda, Jackson Mayanja, ametamka kuwa hawana hofu hata kidogo na wapinzani wao hao huku wakiwaza mchezo wao unaofuata dhidi ya African Lyon. Vinara hao wa ligi watawavaa wapinzani wao wakuu Yanga kwenye mechi ya ligi itakayopigwa Februari 25, mwaka huu ambapo pambano hilo linatarajiwa kuwa na ushindani kutokana na tofauti ya pointi baina ya timu hizo. Mayanja amesema hawawezi kuwafikiria Yanga kutokana na mchezo wao kuwa mbali na kilichopo kwenye fikra zao ni kuangalia namna ya kulipa kisasi kwa Lyon kwenye mechi ya Kombe la FA (Shirikisho), Alhamisi ijayo. “Yanga hatuna wasiwasi nao kwa sababu mechi yao ipo mbali lakini hata ikija tutacheza kwa uwezo wetu kuhakikisha tunapata matokeo mbele yao na tunaamini tunaweza kufanya hivyo. “Lakini sasa tunaangalia namna ya kuwafunga Lyon kwenye mechi yetu inayofuata,” alisema Mayanja.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni