pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumanne, 27 Septemba 2016
KUEREKEA OKTOBA 1 JOSEPH OMOG AKOMALIA SUALA LA UFUNGAJI SIMBA, AONYESHA NAMNA YA KUMALIZA KAZI MAPEMA
Kocha Joseph Omog amekomalia suala la upotezaji wa nafasi ambalo limekuwa kubwa katika kikosi chake cha Simba.
Simba imeweka kambi mjini Morogoro, ikifanya maandalizi dhidi ya mechi ya watani wake Yanga, Oktoba Mosi.
Katika mazoezi yake, Omog amekuwa akiwasisitiza wachezaji wake kufunga ikiwezekana kwa asilimia 90 katika nafasi wanazozipata.
Kwani kila wanapofika kwenye eneo la lango, amekuwa akisimamisha mpira na kuwasiistiza namna ya kuzitumia nafasi.
Simba imekuwa ikipoteza mechi zake nyingi za kufunga kila inapokuwa inashambulia katika mechi mbalimbali za ligi inazocheza.
BEJAIA WATAMBA WANA NAFASI KUBWA YA KUBEBA UBINGWA WA KOMBE LA SHIRIKISHO
MO Bejaia ina matumaini makubwa ya kubeba Kombe la Shirikisho itakapokutana na TP Mazembe katika fainali.
Timu zote mbili zimetokea katika kundi walilokuwemo Yanga ya Tanzania ambayo ilishindwa kuvuka kwenda nusu fainali.
Mohamed Sabah, mmoja wa wataalamu wa masuala ya ufundi, amesema Bejaia wako vizuri zaidi.
“Bejaia kwa sasa wana kikosi bora zaidi. Kikubwa tunahitaji ni kufunga bao la mapema na kushinda mechi ya kwanza,” alsiema Sabah alipozungumza na mtandao wa Kingfut.
Sabah amesema, anaamini Mazembe ni timu bora. Lakini nafasi ipo kwa Bejaia ambayo hata kufika kwake fainali, kumewashangaza wengi.
Bejaia itaanzia nyumba Oktoba 28 na mechi ya pili itakuwa ni Novemba 4 mjini Lubumbashi, DR Congo.
Hata hivyo, Sabah anasisitiza kama Bejaia itashinda mechi ya kwanza. Ina uhakika wa kufanya vema.
KUEREKEA OKTOBA 1 KIUNGO DHOOFU CHAWAPA HOMA MASHABIKI YANGA DHIDI YA WATANI WAO SIMBA
Mashabiki takribani 58 waliotuma maoni yao kuhusiana na kikosi cha Yanga kwenye blog hii, wamesisitiza kwamba kikosi chao lazima kijiimarishe katika kiungo.
Mashabiki hao wanaonekana kuingiwa hofu kutokana na kikosi hicho kupoteza mechi dhidi ya Stand na kiungo kikionekana kimepwaya huku wakiwa wanakutana na Simba, inayoonekana kuwa na kiungo bora zaidi.
Simba inaonekana kuwa na wachezaji wengi vijana zaidi na kiungo bora zaidi. Hali iliyoonyesha kuwapa hofu kubwa mashabiki hao.
"Hii ni hatari sana, lazima kocha Pluijm aifanyie kazi. Unajua hawa jamaa (Simba), wako vizuri sana katika kiungo," alisema Abdul Rashid wa Buguruni jijini Dar es Salaam.
Paul Matiku James wa Geita, naye alisema" "Stand walitupa shida kwenye kiungo. Kilikufa kabisa, sasa tunakutana na Simba. Nina hofu sana."
Wengine walielezea kuhusiana na timu yao kutoonekana ina makali mbele kama ilivyozoeleka.
Hata hivyo, Kocha Hans van der Pluijm, tayari alishaueleza kwamba watahakikisha wanafanya mabadiliko kwa walichoona ni tatizo.
Tayari Yanga ipo mjini Pemba ikijiandaa na mechi dhidi ya Simba itakayopigwa Jumamosi ya Oktoba Mosi.
TETESI ZA MASTAA MAJUU WEST Ham imeanza kumfukuzia kimya kimya kiungo wa Chelsea, Cesc Fabregas ambaye inadaiwa kuwa hayupo katika mipango ya muda mrefu ya Kocha Antonio Conte na anaruhusiwa kuondoka klabuni hapo katika dirisha la Januari. Fabregas alitolewa katika pambano la juzi dhidi ya klabu yake ya zamani Arsenal licha ya kufunga mabao mawili katika pambano la Leicester City wikiendi iliyopita na hatima yake imekuwa shakani Stamford Bridge tangu dirisha kubwa lililopita.
CHELSEA KIMENUKA KUWA kocha wa Chelsea ujipange, kazi sana asikwambie mtu. Shida ni bilionea mmiliki wa timu hiyo, Roman Abramovich. Walipochapwa 2-1 na Liverpool, usiku huo wa mechi bilionea huyo aliliweka kitimoto benchi la ufundi kwa nini wamechapwa mechi hiyo. Wakati Kocha Antonio Conte akijipanga kuhusu jambo hilo, kikosi chake kimekumbana na kichapo kingine, tena safari hii dhidi ya mahasimu wao wa kutoka jiji moja la London.
Jumatatu, 26 Septemba 2016
Wakala: wa Pogba afunguka Raiola, asema Ibrahimovic angenivunja miguu kama Pogba asingetua United!
Wakala Mino Raiola amesema kuwa Zlatan Ibrahimovic kwa utani alitishia kumvunja miguu yake kama angeruhusu Paul Pogba kutua klabu nyingine tofauti na Manchester United.
Raiola ambaye anawawakilisha wachezaji wote hao wawili, pamoja na Henrikh Mkhitaryan, alizidalalia dili zote hizo tatu za mastaa hao kutua United msimu huu-ikiwa dili la Pogba la Paundi 89 Milioni kuwa ndio kubwa zaidi.
“Zlatan alinambia, ‘Ukimpeleka Pogba klabu nyingine, ntakuvunja miguu yako’,” alisema Raiola
Wachezaji hao wawili wamempa kocha Jose Mourinho nafasi nyingi ndani ya uwanja, lakini ikiwa Zlatan tayari ameshatulia haraka kwenye timu na tayari ameshafunga magoli manne kwa Mashetani Wekundu hao, Pogba amehangaika kutulia tangu arudi kwenye klabu yake hiyo ya utotoni.
Hata hivyo, Mfaransa huyo alikuwa katika kiwango bora chenye thamani ya gharama yake, pale alipofunga kwenye ushindi wa 4-1 dhidi ya mabingwa watetezi Leicester City, Jumamosi hii.
Kuelekea mechi hiyo, Raiola, aliweka wazi hisia zake zifahamike kwamba Mourinho hamchezeshi Pogba katika eneo analolipendelea zaidi, ambayo ni sehemu ya kiungo mshambuliaji wa kushoto.
“Pogba bado anatakiwa atafute eneo lake kwenye tmu,” aliongeza Raiola. “Sehemu ninayopendelea acheze ni kiungo mshambuliaji wa kushoto.
“Kwa nguvu, stamina na ubunifu alionao… Pogba hatakuwa wa mchezo katika sehemu hiyo. Lakini ni Mourinho anayeamua.”
Huku Rooney akisugua benchi katika mechi dhidi ya Leicester, na Pogba akicheza katika sehemu ya kiungo mshambuliaji, bado tunabaki kusubiri kama kiwango bora kilichooneshwa Jumamosi kitamfanya Mourinho aendelee na mfumo uleule mpaka msimu unaisha au la.
Kumbe Azam fc kimenuka Ukweli huu apa ‘Kujiondoa katika timu kwa watoto wa mmiliki Azam FC ni tatizo…?’
Na Baraka Mbolembole
ACHANA na vipigo viwili mfululizo ambavyo timu ya Azam FC imekumbana navyo katika ligi kuu Tanzania Bara msimu huu, ndani ya timu hiyo mambo si shwari kama ilivyokuwa misimu iliyopita kufuatia kuwapo kwa mgogoro kati ya mmiliki wa timu hiyo iliyoanzishwa mwaka 2007 na baadhi ya watoto wake.
Kilichotokea ni kwamba, baada ya mmiliki ‘kuwakaribisha’ baadhi ya watu wenye asili ya Asia ndani ya timu hiyo na kuwapa mamlaka makubwa, watu hao wakaanza kupeleka maneno kwa mmiliki wa timu na kumwambia kuwa vijana wake wanatumia vibaya pesa jambo ambalo liliwakera watoto hao baadhi na kuamua kujiweka kando.
Kitendo cha kujiweka kando kwa vijana hao ambao wamekuwa na msaada mkubwa kwa timu hiyo tangu kuanzishwa kinadaiwa kuanza kutoa athari ndani ya timu kwa kuwa baadhi ya mahitaji ambayo yalikuwa yakipatikana klabuni hayapo tena na tayari ukata umeanza kupigiwa kelele ndani ya timu hiyo.
Azam FC hadi wanatwaa taji lao la kwanza la VPL msimu wa 2013/14 ilijiwekea utaratibu wa kutoa posho kwa kila mfanyakizi pale Azam Complex, Chamanzi.
Kwa mfano, timu ikishinda wafanyakazi wote walikuwa wakipatiwa posho ya juu na ikitokea matokeo ya sare ama kupoteza mechi posho inapungua kutokana na matokeo yatakavyokuwa ndio maana wakati ule kulikuwa na muunganiko na umoja wa hali ya juu sana kuanzia kwa wafanyakazi hadi kwa wachezaji na benchi lao la ufundi.
Utaratibu huo ulisaidia kwa kiasi kikubwa watu wa nje ya uwanja kuisapoti timu na vijana hao wa mmiliki wa timu ndiyo walikuwa chachu ya kila kitu. Sasa hakuna nafasi ya wahudumu wa uwanja kwa mfano kupata posho inayotokana na matokeo ya timu ndani ya uwanja.
Upande wangu naamini kwamba mtoto wa mfalme anapaswa kuishi katika mazingira yanayokidhi hadhi ya mtoto wa kifalme.
Kilichowaondoa vijana hao wa mmiliki wa Azam FC katika timu ‘kususa’ ni maneno ambayo yalipelekwa kwa mzee wao kwamba wamekuwa wakitumia kiasi kikubwa cha pesa katika maisha yao ya kawaida.
Wakatengenezewa ‘majungu’ na wageni hao na ili kuepusha lawama vijana hao wakaamua kujiweka kando na kuachana na mambo ya timu. Hilo limewaumiza na linaendelea kuwaumiza wengi pale Azam Complex kwa maana hivi sasa wengi wanategemea mishahara tu na si vinginevyo.
Nakumbuka mwanzoni mwa mwaka 2014 niliandika jinsi wachezaji wa timu hiyo walivyokuwa wakipigia majungu kwa mmiliki wa timu na nikasema ili Azam FC ifanikiwe kupata ubingwa bosi wa timu hakupaswa kuzungumza na baadhi ya wachezaji waliokuwa wakimpigia simu na kuzungumzia mambo ya timu kwa siri.
Baadhi ya wachezaji wa Azam wakati ule walikuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na mmiliki wa timu kiasi cha kufikia kutengenezea majungu na kuwachongea makocha kama Boris Bunjak. ‘Kujiondoa katika timu kwa watoto wa mmiliki Azam FC ni tatizo…?’
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)