pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Alhamisi, 19 Januari 2017
LIVEROOOL YASONGA MBELE KOMBE LA FA Lucas Leiva akishangilia baada ya kuifungia Liverpool dakika ya 18 bao pekee katika ushidi wa 1-0 ugenini dhidi ya wenyeji Plymouth kwenye mchezo wa Raundi ya Tatu Kombe La FA England usiku wa jana Uwanja wa Home Park, Plymouth. Divock Origi alikosa penalti dakika ya 87 iliyookolewa na kipa na sasa Liverpool itapambana na timu ya Daraja la Kwanza, Wolves Uwanja wa Anfield katika Raundi ya Nne ya FA
REAL MADRID SASA WAGEUKA VIBONDE, WAGONGWA TENA HISPANIA Cristiano Ronaldo wa Real Madrid akimruka Gustavo Cabral wa Celta Vigo katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Kombe la Mfalme usiku wa jana Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid. Celta Vigo ilishinda 2-1 ugenini, hicho kikiwa kipigo cha pili mfululizo kwa Real Madrid kufuatia wiki iliyopita pia kufungwa 2-1 na Sevilla katika La Liga baada ya kucheza mechi 40 bila kufungwa. Bao la Real lilifungwa na Marcelo dakika ya 69 wakati ya Celta Vigo yalifungwa na Iago Aspas dakika ya 64 na Jonny Castro dakika ya 70 P
Jumatano, 18 Januari 2017
MAMBO YA SAMATTA JANA GENK IKITOA SARE KOMBE LA UBELGIJI Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta Jumanne akipiga mpira kitaalamu wakati timu yake, KRC Genk ikimenyana na KV Oostende katika mchezo wa Kombe la Ubelgiji Uwanja wa Versluys Arena, Oostende. Timu hizo zilifungana bao 1-1.
Gurdiola awasifu wachezaji wake kwa kupigwa nne Ni heri kuambiwa ukweli unaouma ili ukujenge na uweze kubadilika ila uongo mtamu utakupotosha na kukupoteza.Sikia Pep Gurdiola alichowaambia wachezaji wake. Pep Gurdiola anaonekana sasa mambo ni magumu sana.Toka amekuja Uingereza amekuwa na matokeo magumu sana katika ligi hii tofauti na ilivyotarajiwa.Ameshaanza kutolewa mbio za ubingwa na hakuna mwenye uhakika kama atamaliza katika top four msimu huu.Wengi walichotarajia sio kinachomtokea. Pengine hii sijui ni kuwapa moyo au kudata,kwani Pep amewapongeza wachezaji wake.Gurdiola amewaambia wachezaji wake kwamba walicheza vizuri zidi ya Everton.Katika mchezo huo ambao Gurdiola anawasifu wachezaji wake,City walikula kipigo cha mbwa mwizi cha goli nne kwa sifuri ugenini zidi ya Everton. Hii iliwashtua wachezaji wa City na inaonekana labda anajaribu kuwajenga kisaikolojia.Timu imefungwa goli nne leo hii wanasifiwa kucheza vizuri.Haieleweki uzuri huo Gurdiola ameuchukulia kwa sura gani.City wana makosa mengi kiuchezaji haswa eneo lao la ulinzi kuanzia alipo Stones na golikipa wao Bravo wanafanya makosa kila siku.Haihitaji maarifa makubwa sana kuona kwamba City wana ulinzi mbovu sana kwa sasa.Claudio Bravo golikipa aliyepewa nafasi baada ya Gurdiola kumruhusu Joe Hart aondoke hadi sasa ameruhusu goli 14 katoka mechi 22. Wikiendi iliyopita tuliona magoli kwa namna ambayo huezi amini kuwa hawa ni Man City.Makinda wapya wa Everton Lookman na Tom Davies walionekana kutowaogopa kabisa City na walicheza kwa kujiamini mno.Timu pinzani zinazocheza na Man City zimekuwa haziwapi heshima Man City kwani sio Etihad sio ugenini timu pinzani za Man City zinajaribu kuwapa presha mabeki wa City wanaoonekana kukosa umakini. Pep Gurdiola anaonekana wazi anastahili zigo la lawama kwa kumuachia Hart aonfoke,lakini pia Stones aliyenunuliwa kwa £50m anaonekana kupwaya mno.Ni kipindi ambacho Gurdiola alipaswa awaambie ukweli wachezaji wake kuhusu uzembe wanaofanya.
EXCLUSIVE: OKWI AVUNJA MKATABA WAKE DENMARK, SONDERJYSKE YASEMA ISHU IMEANZIA KWENYE NAMBA Mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi ameamua kuondoka nchini Denmark. Okwi amevunja mkataba wake na klabu ya Sonderjyske Fodbold ambayo alijiunga nayo akitokea Simba. Mkuu wa masuala ya michezo ya klabu hiyo, Jorgen Haysen amesema Okwi mwenye umri wa miaka 24 ameamua kuvunja mkataba baada ya kuona hajapata namba ya uhakika katika kikosi hicho. “Okwi hakupata nafasi ya kucheza kama ambavyo alitarajiwa, lakini kiwango chake pia hakikukua kumshawishi kocha aanze kumpa nafasi kwa kiwango cha juu. “Mwisho akaamua kuondoka, tumekaa na kufikia makubaliano vizuri. Zaidi, ninamtakia kila la kheri aendako,” alisema. Okwi alitua katika kikosi hicho Julai 2015 akitokea Simba na kusaini mkataba wa miaka mitano na mkataba wake ungeisha 2020. Hata hivyo, mara kwa mara Okwi amekuwa akihusishwa kurejea Simba lakini amekuwa haeleweki. Mara kadhaa, amekuwa akikanusha na mara nyingine akieleza yuko tayari kuzungumza au yuko tayari kurejea Simba. Hata hivyo, viongozi wa Simba wamekuwa kwenye mgawanyiko mkubwa kuhusiana na ujio wake, wako wakitaka arejee na wengine wakipinga kabisa.
LIVE KUTOKA JAMHURI: MTIBWA SUGAR 0 VS 0 SIMBA (FLL TIME) MPIRA UMEKWISHAAA DAKIKA 4 ZA NYONGEZA Dk 89, Mtibwa wanafanya kazi ziada kuokoa mpira wa faulo Dk 86, Kipa Mohammed anafanya kazi ya ziada na kuugusa mpira uliokuwa unajaa wavuni, kona. Simba wanachonga lakini haina madhara SUB 85, Mtibwa Sugar wanamuingiza Hussein Javu kuchukua nafasi ya Jaffar Salum SUB Dk 83 Simba wanamtoa Kichuya, nafasi yake inachukuliwa na Jamal Simba Mnyate Dk 81, nafasi nzuri kwa Mtibwa, mabeki wa Simba wanagongana na mpira unamkuta Friday, lakini anapinga shuti matege....hakuna kitu Dk 79, Mandawa tena, anaachia mkwaju mkali lakini anapaisha juuu SUB Dk 77, Barnabas anaingia Kelvin Friday SUB Dk 75, Simba wanamtoa Kazimoto na nafasi yake inachukuliwa na Pastroy Athanas Dk 73, Ajibu anafanya kazi ya kugeuka na kuachia shuti hapa, Said Mohammed anaokoa na kuwa kona ambayo haina madhara Dk 72, Mandawa amegeuka anapiga shuti kali kabisa hapa lakini Agyei anadaka kwa ufundi mkubwa kabisa Dk 70, Banda anaachia mkwaju mkali kabisa hapa lakini unamgnga beki Mtibwa na kuwa kona Dk 68, Kichuya anawachambua mabeki wa Mtibwa lakini Shomari anatoa na kuwa kona, inachongwa na kuokolewa Dk 65 Baba Ubaya anagongana na Hamad Juma na wote wako chini wanatibiwa KADI Dk 64, Issa Rashid "Baba Ubaya" analambwa kadi yah njano kwa kumuangusha Kazimoto Dk 59, Kichuya anamtoka Baba Ubaya, krosi safi kabisa lakini Mbonde anaruka na kupiga kichwa safi kabisa Dk 57, Liuzio anamzidi mbio Henry lakini anashindwa kuudhibiti mpira kutokana na uwanja kuwa mbovi Dk 54, Simba wanamuingiza Ajibu kuchukua nafasi ya Mavugo Dk 50, mpira bado unakuwa ni wa kubutua zaidi lakini safu ya ulinzi ya Simba wanapaswa kuwa makini hasa pembeni DK 45,Mtibwa wanaanza kwa kasi, krosi matata ya barnabas nakuwa kona MAPUMZIKO Dk 44, MAvungo anajaribu kuingia tena lakini Henry Joseph anaondosha hatari Dk 41 Mavugo anageuka na kuachia fataki hapa, linatoka kidogo juu la lango la Mtibwa Dk 37, Luizio na Kotei wanafanya kazi nzuri hapa, wanagongeana vizuri lakini shuti la Mavugo linashindwa kulenga Dk 36, ladha ya mpira ni butuabutua zaidi kuliko pasi za uhakika Dk 31 Kotei anafanya anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira miguuni mwa Chanongo akiwa anakaribia kuachia fataki karibu na lango la Simba. Inakuwa kona, inachongwa na Issa Rashid lakini Simba wanaokoa Dk 28, Luizio anamtoka Ali Shomari, anapiga krosi safi kwa Mavugo akiwa yeye na kipa Mohammed lakini anashindwa kufunga Dk 20, hakika mpira hauna mvuto sana. Mtibwa Sugar wanapata kona, inachongwa vizuri na Mandawa anapiga kichwa safi kabisa, lakini Agyei anadaka vizuriDk 15 Kotei mita 28 anaachia shuti kali lakini Said Mohammed anadaka vizuri kabisa Dk 14, Mtibwa Sugar wanafanya shambulizi kali hapa, lakini Simba wanaokoa na kuwa kona. anaichonga Baba Ubaya lakini Simba wanaokoa vizuri Dk 11 sasa, mechi ina presha kubwa. Lakini zaidi mpira unachezwa katikati na uwanja unaendelea kuonekana tatizo katika umiliki wa mpira Dk 6, Simba wanapata kona, anaichonga hapa Kichuya lakini ni kona hovyoooo Dk 4 mpira safi wa krosi wa Hamad Juma lakini unakosa mtu, Mtibwa wanaokoa Dk 1, mpira umeanza lakini ikionekana kuanza kwa kubutua. Mtibwa wanapata faulo si mbali na lango la Simba KIKOSI MTIBWA: 1-Said Mohamed 2-Ally Shomary 3-Issa Rashid 4-Henry Joseph 5-Salim Mbonde 6-Shaban Nditi 7-Haruna Chanongo 8-Ally Makarani 9-Rashid Mandawa 10-Jaffary Salum 11-Vicent Barnabas SUB -Benedict Tinoko -Rogers Gabriel -Kassian Ponera -Dickson Daudi -Ibrahim Rajabu Jeba -Kelvin Friday -Hussen Javu KIKOSI SIMBA: 1. Daniel Agyei, 2. Hamad Juma, 3. Mohamed Zimbwe 4. Abdi Banda 5. Method Mwanjale, 6. Jonas Mkude 7. Shiza Kichuya 8. James Kotei 9. Laudit Mavugo 10 Juma Liuzio 11. Mwinyi Kazimoto Sub… Peter Manyika Novatus Lufunga Jamal Mnyate Pastory Athanas Mzamiru Yassin Ibrahim Ajibu
LIVE KUTOKA JAMHURI: MTIBWA SUGAR 0 VS 0 SIMBA Dk 28, Luizio anamtoka Ali Shomari, anapiga krosi safi kwa Mavugo akiwa yeye na kipa Mohammed lakini anashindwa kufunga Dk 20, hakika mpira hauna mvuto sana. Mtibwa Sugar wanapata kona, inachongwa vizuri na Mandawa anapiga kichwa safi kabisa, lakini Agyei anadaka vizuriDk 15 Kotei mita 28 anaachia shuti kali lakini Said Mohammed anadaka vizuri kabisa Dk 14, Mtibwa Sugar wanafanya shambulizi kali hapa, lakini Simba wanaokoa na kuwa kona. anaichonga Baba Ubaya lakini Simba wanaokoa vizuri Dk 11 sasa, mechi ina presha kubwa. Lakini zaidi mpira unachezwa katikati na uwanja unaendelea kuonekana tatizo katika umiliki wa mpira Dk 6, Simba wanapata kona, anaichonga hapa Kichuya lakini ni kona hovyoooo Dk 4 mpira safi wa krosi wa Hamad Juma lakini unakosa mtu, Mtibwa wanaokoa Dk 1, mpira umeanza lakini ikionekana kuanza kwa kubutua. Mtibwa wanapata faulo si mbali na lango la Simba KIKOSI MTIBWA: 1-Said Mohamed 2-Ally Shomary 3-Issa Rashid 4-Henry Joseph 5-Salim Mbonde 6-Shaban Nditi 7-Haruna Chanongo 8-Ally Makarani 9-Rashid Mandawa 10-Jaffary Salum 11-Vicent Barnabas SUB -Benedict Tinoko -Rogers Gabriel -Kassian Ponera -Dickson Daudi -Ibrahim Rajabu Jeba -Kelvin Friday -Hussen Javu KIKOSI SIMBA: 1. Daniel Agyei, 2. Hamad Juma, 3. Mohamed Zimbwe 4. Abdi Banda 5. Method Mwanjale, 6. Jonas Mkude 7. Shiza Kichuya 8. James Kotei 9. Laudit Mavugo 10 Juma Liuzio 11. Mwinyi Kazimoto Sub… Peter Manyika Novatus Lufunga Jamal Mnyate Pastory Athanas Mzamiru Yassin Ibrahim Ajibu
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)