Alhamisi, 5 Januari 2017

MICHAEL JOHNSON LEADERS Michael Johnson ni mmoja wa wanariadha mashughuli kuwahi kutokea duniani. Aliwahi kushinda medali 4 za dhahabu kwenye michuano ya Olympics na Medali 9 za dhahabu katika World Championships. Mmarekani huyo ni mwanariadha pekee wa kiume katika historia kuwahi kushinda mbio za mita 200 na mita 400 kwenye mchuano mmoja wa Olympics, aliweka rekodi hiyo mwaka 1996 huko Atlanta. MJ mwaka 1999 katika World Championship huko Sevilla,Spain aliweka rekodi ya dunia katika mbio za mita 400 akitumia muda wa sekunde 43.18, rekodi hiyo imedumu kwa miaka 17 ambapo imekuja kuvunjwa na Msouth Afrika Wayde van Niekerk kwenye michuano ya Olympics,Rio 2016 akitumia muda wa sekunde 43.03. Mwaka 2016 MJ alianzisha Progamu inayoitwa Michael Johnson Young Leaders ambayo inafanya kazi kupitia mfumo wa misaada ikiwa na malengo matatu. 1.Michezo 2.Uongozi 3.Jamii MJ ,49, ameamua kuanzisha Programu hii endelevu ili kusaidia vijana kutoka nchi mbalimbali ambao wanatokea katika background ya michezo na kupitia changamoto mbalimbali katika maisha yao. Vijana kutoka nchi mbalimbali watachaguliwa kupitia Local Sports Organizations na kupata fursa ya kwenda Dallas-USA kupewa mafunzo ya michezo na uongozi (Leadership). . Mtandao huu ni mkubwa, unafanya kazi kwa kushirikiana na Coaches Across Continents ambayo ni NGO ya kimataifa, Co Create consultancy na nyinginezo. . . Kupitia ukurusa huu tutaendelea kukupa habari na sasisho (Updates) mbalimbali kuhusu Programu hii. Cc @___tooma___

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni