Jumapili, 1 Januari 2017

VIGOGO HAWA NDIYO KIKWAZO CHA CHELSEA KUBEBA UBINGWA ENGLAND, IKIWEZA, BASI MAMBO KWA ULAINIIII Chelsea iko kileleni mwa Ligi Kuu England kwa tofauti ya pointi dhidi ya Liverpool wanaoshika nafasi ya pili. Lakini hiyo bado si sababu ya kuamini tayari wao wana nafasi ya kuwa mabingwa na hasa kama utazungumzia mechi za vigogo sita. Vigogo sita wa Premier League ni Manchester United, Liverpool, Arsenal, Chelsea, Manchester City na Tottenham. Hakuna ubishi hizi ndiyo timu sita zinazowania ubingwa na lazima bingwa atatoka miongoni mwao. Kama utaangalia mechi tano kwa kila timu baada ya kukutana na kigogo mmoja mara moja, Liverpool ndiyo haikupoteza dhidi ya kigogo yoyote. Lakini Chelsea ilipoteza mechi mbili, moja ikichapwa mabao 4-0 na Arsenal. Man City ilipoteza mechi tatu na zilizobaki zote zilipoteza mechi mbili. Katika mechi tano dhidi ya vigogo wenzake, kama utatengeneza msimamo wa vigogo tu, Liverpool ndiyo inaongoza kwa kukusanya pointi 11 katika mechi hizo tano ikifuatiwa na Chelsea yenye pointi 9. Man Cityi imekusanya 6 huku Arsenal, Spurs na Man United kila mmoja imekusanya pointi 5 ikiwa ni wastani wa pointi moja kwa kila mechi sawa na sare 5. Hii inaonyesha bado kuna ugumu wa juu kwa Chelsea na analazimika kufanya vema katika mechi 5 dhidi ya vigogo wenzake ili kujihakikishia ubingwa. MECHI ZIJAZO ZA VIGOGO SITA: Jan 4: Tottenham v Chelsea Jan 15: Man United v Liverpool Jan 21: Man City v Tottenham Jan 31: Liverpool v Chelsea Feb 4: Chelsea v Arsenal Feb 11: Liverpool v Tottenham Feb 26: Man City v Man United Mar 4: Liverpool v Arsenal Mar 18: Man City v Liverpool Apr 1: Arsenal v Man City Apr 5: Chelsea v Man City Apr 15: Man United v Chelsea Apr 29: Tottenham v Arsenal May 6: Arsenal v Man United May 13: Tottenham v Man United

Jumamosi, 31 Desemba 2016

Naona niwe wa kwanza kama sio wa tatu kukutakia mema katika mwaka unaosogea kwa kasi, Nahofia msongamano wa msg za heri ya mwaka mpya inabidi nikutumie ujumbe huu mapema... Tunaposogea kuanza mwaka mwingine 2017 ina maana tunazimaliza Mbio za mwaka 2016 haikuwa safari rahisi, Vikwazo navyo havikuwa haba lakini TUMSHUKURU MUNGU KWA YOTE! Siku hazikuganda ndo maana tunahesabu masaa kuumaliza mwaka, Ni masaa machache yalobakia kuufungua Mwaka 2017... Umejifunza nini kwa mwaka 2016? Hiyo ibaki kuwa siri yako na uzitumie changamoto ulizopitia kwa mwaka 2016 kuwa chachu ya UKOMBOZI katika mwaka ujao wa 2017. Mungu wetu si muongo hata ashindwe kukufanya uwe kichwa na kukuondosha katika mkia, Kama kuna nzige, Mandumandu na palare wamekula miaka yako MUNGU ANAKWENDA KURUDISHA MIAKA HIYO! Mwaka 2017 uwe mwaka wa mavuno na ghara zako zijae na kufurika hata kumwagikia, Uwe mwenye afya njema pamoja na BARAKA TELE... Udumu katika NEEMA ZA BWANA zitakazokupa wepesi katika mipango yako mwaka 2017.

CHELSEA YASHINDA MECHI YA 13 MFULULZO LIGI KUU ENGLAND Wachezaji wa Chelsea wakishangilia ushindi wao wa 13 mfululizo katika Ligi Kuu ya England baada ya kuilaza 4-2 Stoke City leo Uwanja wa Stamford Bridge. Mabao ya Chelsea yamefungwa na Gary Cahill dakika ya 34, Willian dakika ya 57 na 65 na Diego Costa dakika ya 85, wakati ya Stoke City yamefungwa na Bruno Martins-Indi dakika ya 46 na Peter Crouch dakika ya 64

POGBA AIFUNGIA LA USHINDI MAN UNITED YAUA 2-1 ENGLAND Paul Pogba akiwaongoza wachezaji wenzake wa Manchester United kushangilia baada ya kufunga bao la ushindi dakika ya 86 katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Middlesbrough kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Old Trafford. Bao lingine la United lilifungwa na Anthony Martial dakika ya 85 kufuatia Grant Leadbitter kuwafungia wageni bao la kuongoza dakika ya 67

ISLAM SLIMANI AING'ARISHA LEICESTER CITY Mshambuliaji Islam Slimani akiruka kuifungia kwa kichwa Leicester City dakika ya 20 bao pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya West Ham United kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Kings Power

Ijumaa, 30 Desemba 2016

Taifa Jangombe imefanikiwa kupata ushindi kwenye uzinduzi wa Mapinduzi Cup Seif Hassan ‘Banda’ amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao kwenye michuano ya Mapinduzi Cup msimu huu baada ya kuifungia timu yake bao pekee la ushindi wakati wa mchezo wa ufunguzi kati ya Taifa Jang’ombe dhidi ya Jang’ombe Boys mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Amaan, Zanzibar. Banda aliifungia bao Taifa Jang’ombe dakika ya 83 na kuifanya timu yake iongoze Kundi A kwa kuwa na pointi moja mkononi baada ya kucheza mchezo mmoja. Mechi hiyo ilikuwa na upinzani mkubwa kutokana na timu zote kutoka mtaa mmoja hivyo kukamiana na kutambiana nje na ndani ya uwanja kulisababisha mechi hiyo kuwa ya upinzani mkali. Baada ya mchezo huo, Kesho (Jumamosi) hakutakuwa na mechi, Jumapili ratiba ya Mapinduzi itaendelea lakini mechi inayosubiriwa kwa hamu ni kati ya Taifa Jangombe dhidi ya Simba SC ambayo inatarajiwa kuwasili Zanzibar kesho (Jumapili).

Wenger aipa shavu Chelsea kubeba ndoo msimu huu. Manager wa Arsenal ambao na wao bado wapo kwenye mbio za kukimbiza ubingwa na kuacha tabia yao ya kuishia nafasi ya nne kila msimu, ameipa shavu Chelsea kushinda ubingwa wa ligi msimu huu. Wenger alikua kwenye mkutano na waandishi wa habari ambapo alisema kwa sasa anaipa nafasi kubwa Chelsea kushindwa ubingwa kwa mwenendo wao,“Kwa sasa Chelsea wana nafasi kubwa kwasababu wametengeneza utofauti mkubwa sana” Wenger aliendelea,“Lakini bado wanaweza kupoteza kama tunavyojua hapa England. Kwasasa wanaonekana kwamba wanaenda kushinda lakini wanaweza kupoteza hapo baadae. Wamejua matatizo yao vizuri na utampa sifa Conte kwa kutatua hayo matatizo”. Kesho Dec 31 Chelsea watakutana na Stoke City na kujaribu kuendelea kuvuna points muhimu ili wajiweke kwenye nafasi nzuri. Mechi kubwa kwa kesho ni kati ya Liverpool Vs Manchester City